Lusungo
JF-Expert Member
- Jan 4, 2014
- 27,139
- 39,381
Hahahaaa lakini hebu tuache upuuzi kidogo...hivi kwani kuna tatizo gani watu wakiishi ughaibuni au wakiishi mavumbini? Yote si maisha tu? Kama yote ni maisha haya malumbano huwa yana tija gani zaidi ya kufurahisha jamvi tu?
Hao jamaa usiwashangae sana kwani ndivyo walivyo. Wako adventurous sana. They can't rest on their laurels. Ndo maana unawaona hawaachi kuzitafuta fursa. Huwezi kuendelea kama ukikaa tu na kuridhika na hali uliyonayo. Leo hii pengine Marekani isingekuwepo kama si ujasiri na uthubutu wa hao wazungu kutoka makwao na kwenda ku explore the New World.
Sasa wewe endelea kushangaa malengo, ujasiri, na uthubutu wao huku wenzio wakizidi kupiga hatua mbele kwenye maendeleo.
Hahahaa huruma ya nini tena?
Kwani hamuwezi kujitafutia hadi mtafutiwe?
Tukiacha utani, sioni hata kwa nini hili suala liwe ishu kihivyo kiasi cha kuweza kujitokeza mara kwa mara humu.
Tatizo ni nini hasa? Manake kila mtu ana maisha yake....sasa ya nini kuanza kuponda maisha ya watu ambao hata huwajui?
Kuponda maisha ya watu tena usiowajua kunamnufaisha nini mtu?
Ha ha ha ha Mkuu mie sijaponda nimetamani tu nikaushudue ulimwengu anaoishi mheshimiwa Kuveta ambao ktk utandawazi huu Una makochi na vitu vingine ambavyo bongo mavumbini hakuna.....
Teh teh teh mi naona hakuna tatizo MTU kuishi mbelez ila huku kwenye vumbi ndio shida huoni mamake Kuveta hataki kurudiii??
Ha ha haaa mkuu hopeful umemsoma Kuveta tangu mwanzo na thread zake zingine ameyaanzisha yeye haya mambo hata hivyo nashangaa wanaomkandia wakati mwenzao yupo kwenye raha tele....
Binafsi sioni tatizo MTU kuishi kwenye tambaralez labda haters hao mkuu....
Again tupeni michongo jamani na sie tuje kuyaona maghorofa ya yuropa
Last edited by a moderator: