Bill Gates anywa maji ya Kinyesi

Mbona mitambo namna hiyo ipo miaka mingi tu, labda hii yake anaipigia debe kwa kuwa ni ya sadaka?
 
Hayo si mapya kwetu kanda ya ziwa kwani watu walishaanza kunywa product za kinyesi cha binadamu kwa kutumia kile kinywaji maarufu kinachopigwa vita na serikali maarufu kama gongo la m*vi

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Wakazi wa Mwanza, Shinyanga, Bukoba wanakunywa maji ya kinyesi miaka mingi tu.
 
150107223336_bill_gates_512x288_billgates_nocredit.jpg

Bill Gates akinywa maji yaliotengezwa kutokana na kinyesi

Mmiliki wa kampuni ya Microsoft Bill Gates amekunywa maji yaliotengenezwa kutokana na kinyesi cha binaadamu kama maonyesho ya teknolojia mpya itakayoweza kutoa maji safi katika mataifa yanayoendelea.

Mwanzilishi huyo wa Microsoft amesema kuwa ataisambaza mitambo ya teknolojia hiyo mpya kote duniani baada ya kuifanyia majaribio mwishoni mwa mwaka huu.

Teknolojia hiyo imeungwa mkono na shirika la WaterAid ambalo limesema kuwa itasaidia sana katika maeneo ya miji.

Kulingana na shirika hilo la hisani takriban watu millioni 748 hawana maji safi ya kunywa.

Katika kanda ya video iliyowekwa katika blogu yake, Bwana Bill Gates alishuhudia kinyesi cha Binaadamu kikiingizwa katika mtambo huo kabla ya kunywa maji yaliokuwa yakitoka kutoka kwa kikombe.

''Maji hayo ni mazuri sana ikilinganishwa na maji yoyote yale niliokunywa, na baada ya kusomea teknolojia hii nitayanywa kila siku''.

Maji haya ni salama kabisa'', aliandika katika blogu yake. Kulingana na mtengenezaji wa mtambo huo Peter Janicki, maji taka hayo huchemshwa kabla ya mvuke wa maji hayo kutengwa na taka ngumu.

Taka hizo ngumu baadaye huwekwa katika moto na kutoa mvuke unaoendesha mashine zinazotoa nguvu za umeme kwa mtambo huo na pia kwa wakazi wa eneo hilo.

Maji hayo baadaye hutiwa ndani ya mtambo wa kusafisha maji ili kutoa maji safi ya kunywa.

''lakini kwa nini mtu awe na wazo la kubadilisha uchafu kuwa maji ya kunywa na umeme'', aliuliza Gates.

Jibu aliloandika ni kwamba kwa sababu magonjwa yanayosababishwa na mazingira machafu huwaua watoto 700,000 kila mwaka na huwakinga wengine wengi dhidi ya kuathirika kiakili na kimwili.

Chanzo: BBC

Hivi hapa ishu ni huyo kibopa au ni maji au ni cheap techno....kama ni maji mbona kitambo tu watu wana recycle...naona hapa ni kibopa kufanya marketing ya hizo products. Wamefanikiwa kuzitangaza...
 
Hivi hapa ishu ni huyo kibopa au ni maji au ni cheap techno....kama ni maji mbona kitambo tu watu wana recycle...naona hapa ni kibopa kufanya marketing ya hizo products. Wamefanikiwa kuzitangaza...

Ila umemuona alivyokaza USO? chezea nnya...
 
download%2B(3).jpg


Ukistaajabu ya musa utayaona ya firauni, nani anayeweza kuamini hichi kilichotokea, mtu tajiri duniani kunywa maji ya kinyesi.


Bill Gates amekunywa maji yaliotengenezwa kutokana na kinyesi kwenye maonyesho ya teknolojia mpya itakayoweza kutoa maji safi katika mataifa yanayoendelea.


Taarifa kutoka shirika la WaterAid zinaeleza kuwa takribani watu milioni 748 hawana maji safi ya kunywa hivyo teknolojia hiyo itasidia sana maeneo mengi ya miji.

https://www.youtube.com/watch?v=bVzppWSIFU0
 
Yule mmoja kati ya matajiri Wakubwa huko Marekani ajulikanaye kama Bill Gates na ambaye ni mmliki wa Kampuni ya kutengeneza softwares iitwayo Microsoft, baada ya kufanikiwa kuwahasi watoto wa Afrika ikiwemo nchi yangu ya TanZania ili kupunguza idadi ya watu kwa kile alichokiita kama chanjo ya kuzuia magonjwa kama Polio safari hii amekuja na lingine jipya ameweza kwa kutumia Utajiri wake kufadhili utengenezwaji wa mashine ambazo zitakuwa zinageuza Kinyesi cha Binadamu (Mavi) kutoka chooni na kuwa maji ya kunywa ambayo Waafrika ndio watakuwa wanakunywa hayo maji kinyesi!

Na ili kuthibistisha nia yake hiyo ya kishetani kama ilivyo ada yake amapiga Picha ya kisanii kama inavyoonekana hapo chini akijifanya kunywa Maji hayo yaliyotokana na kinyesi cha Binadamu ili kuwashawishi Waafrika kwamba maji yaliyotengezwa kutokana na Kinyesi ni salama na salimini!

Sasa swali langu, hivi Hapa TanZania tunahitaji kweli kunywa maji ya kinyesi wakati tuna Ziwa TanGanyika, Ziwa Nyanza, Mto Ruaha, Mto Rufiji, Ziwa Nyasa hata Kampuni ya TBL waliweza kugeuza Maji ya Bahari na kuwa baridi ambayo yanafaa kunywa sasa kwanini tunyweshwe maji ya Mavi?

 
Hayo mavi watayanywa viongozi wa ccm waliozoea u matonya,dunia haijaishiwa maji kiasi cha kugeuza mavi kuwa maji.
 
Back
Top Bottom