Bilioni 185 za DOWANS ni hela chache sana kwangu - Rostam Aziz

Ndiyo hifyo babaake,ukishangaa ya musa utaona ya firauni sasa mshajua firauni ni nani halafu ndiyo asili yake bado ni muheshimiwa wa jimbo asiloishi,hata TRA wanamwogopa sembuse JK:sleep:
 
Willie,
Kwa mara ya kwanza leo umechangia kishujaa, au kuna mtu ameiba ID yako...(si na maana ya kukandia posti zako)..chukua thanks..:music:
Vipi utarudisha kadi ya kijani lini?
Salimia huko Dom..

- Heshima yako mkuu wangu, mimi bado ni CCM hope kuna siku tutaweza kuisafisha from within Rome haikujengwa in one day ninaamini kwamba matokeo ya huu uchaguzi ulioisha umetoa mwanga mkubwa sana kwa chama changu kuhusu yanayokuja kama hakuna mabadiliko na kuna watu kama mimi tumeusikia huo ujumbe na tunajaribu sana kuwafahamisha wenzetu huku CCM kwamba zile enzi za kama kawaida sasa zimeisha,

- Otherwise, mkuu wangu huwa ninaangalia na kuchambua ishus kwa makini sana na kujali ukweli wa siasa zetu na mazingara, kuliko emotions na kufuata upepo wa bendera, au kutafuta cheap umaarufu, karibu sana ndugu yangu wewe saidia taifa kutoka huko uliko na mimi kutokea ndani ya CCM, kuna siku tutafika tu panapotakiwa!

Mungu Aibariki Tanzania.


William.
 
Hahaha! Kweli hapa amedhihirisha mawazo ya watu wengi kuwa yeye ndiye kiongozi wa serikali ya Tanzania, amepata wapi guts za kusema haya? Kama anakwenda nje kutafuta wawekezaji kama Dowan bora serikali impige marufuku kuwaleta nchini. Huyu dogo anafanya anachoamua ndani ya nchi hii bila uangalizi wowote, kuna siku kicha atamchapa risasi halafu ajisalimishe afungwe lakini Watanzania tutamuona shujaa sana. Hajui watanzania wangapi wanalala na njaa leo halafu yeye anatamba namna hiyo.
 
haya wee acha aseme na azidi kula kwani wanaokula nae bado wanachaguliwa na kuendelea kutawala nchi
 
Mnakumbuka kuwa REV MTIKILA naye yumo ktk payroll ya RA???sijui kama zile 3m mchungaji amezirejesha au naye fisadi tuu!
 
Usemi wa chenge kuziita oneBILLION vijisent unaendelea KUTIMIA. U ken c nao, Rostam anaona 185 billion iz jast a smal amaunt of pesa. Mind u dat makusanyo yaTRA kwa mwezi ni araund hizo pesa(180)
 
Asante RA kwa kutuambia ukweli. kuna mtu siku moja aliwahi kusema kuwa uchumi wa nchi hii uko mikononi mwa familia 9. Kwa hiyo uwezekano wa RA kukusanya mapato zaidi ya TRA ya Tz siyo kitu cha ajabu. Kama asingekuwa na fedha hizo asingeweza kununua serikali ya Tanzania.

Hatuna sababu ya kumlaumu RA kwa sababu katuambia ukweli bali tupiganie kuhakikisha kuwa nchi hii inakuwa na serikali iliyo huru na inawajibika kwa wananchi siyo kwa watu kama RA
 
ikiwa alishiriki kuleta kampun ya kitapeli. Dowans. Bado anatafuta nyingine waje watumalizie kabisa.kwao pakstan wangeshamfanya k2 mbaya
 
Wajanja wameshakata sehemu ya ile video aliyosema kwamba dola milioni 20 za kagoda kwake ni nyingi sana, miezi saba iliyopita pale Kempinski kama sijakosea alipokuwa akijibu swali la Saed Kubenea.
 
ikiwa alishiriki kuleta kampun ya kitapeli. Dowans. Bado anatafuta nyingine waje watumalizie kabisa.kwao pakstan wangeshamfanya k2 mbaya

Dowans walitapeli nini? au waliovunja mkataba ndio walitaka kuwatepeli Dowans? lakini wamekwaa kisiki? Dowans kosa lao nini? Hebu kaa ufikiri kidogo.
 
Asante RA kwa kutuambia ukweli. kuna mtu siku moja aliwahi kusema kuwa uchumi wa nchi hii uko mikononi mwa familia 9. Kwa hiyo uwezekano wa RA kukusanya mapato zaidi ya TRA ya Tz siyo kitu cha ajabu. Kama asingekuwa na fedha hizo asingeweza kununua serikali ya Tanzania.

Hatuna sababu ya kumlaumu RA kwa sababu katuambia ukweli bali tupiganie kuhakikisha kuwa nchi hii inakuwa na serikali iliyo huru na inawajibika kwa wananchi siyo kwa watu kama RA

Kama huna hoja kwa aliyoyasema RA bora ukae kimya, inaonyesha una chuki binafsi, na hizo hazisaidii kwako wala kwa nchi hii.

Tanzania Matajiri ni wengi sana kuliko hao tisa unaowasema wewe, tena kwa sasa, matajiri hata wa nje tunawaona wakimiminika na hata maandamano ya Chadema yalim time Ambani ambae kafatana na matajiri zaidi ya 50 kuja Tanzania.
 
Back
Top Bottom