Bilionea kumkabili Putin katika urais Urusi

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,271
Bilionea mkubwa nchini Urusi ametangaza kukabiliana na Vladimir Putin katika uchaguzi mkuu wa rais wa mwaka ujao. Mikhail Prokhorov amesema ataunda chama kipya cha siasa ambacho kitawalenga watu wa kawaida nchini Urusi. Tajiri huo anamiliki timu ya basketbali New Jersey Net, pamoja na biashara kubwa zinazomfanya ashike nafasi ya tatu kwa utajiri nchini humo. wakati huohuo, waziri wa zamani wa fedha Alexei Kudrin ametoa wito wa kuundwa kwa chama cha kipya huru baada ya kutokea maandamano makubwa ya kupinga serikali, kutokana na tuhuma za wizi wa kura katika uchaguzi wa bunge uliofanyika mapema mwezi huu.
 
Back
Top Bottom