Bibi Harusi afariki Saa moja Kabla ya Kufunga Ndoa

LIKUD

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
15,121
27,128
BIBI%20HARUSI%2010.JPG



Bibi harusi kabla ya kufariki dunia na bwana harusi wakipata chakula siku ya send off yao iliyofanyika Jumatano iliyopita jijini Tanga.




MAREHEMU.JPG



Sanduku lenye mwili wa marehemu Mwalimu Levina,pembeni sanduku la mtoto wake ambae alifariki siku moja baada ya kifo cha mama yake.



Tanga, Tanzania.
Bibi harusi, mkazi wa Chanika mjini Handeni, Mkoa wa Tanga, Levina Mmasi (23) amefariki dunia saa moja kabla ya ndoa kufungwa kanisani na kuilazimu kamati ya harusi kushughulikia shughuli za msiba.


Mwanamke huyo alifariki Jumamosi iliyopita na msimba huo umekuwa gumzo kubwa mjini Tanga huku wananchi wakisema kuwa ni tukio ambalo halijawahi kutokea.


Msemaji wa familia, Firmin Mrimasha amesema chanzo cha kifo cha Levina ambaye alikuwa mjamzito alijifungua siku moja kabla ya ndoa na ilibainika kwamba alikuwa na malaria baada ya kupelekwa Hospitali ya Wilaya ya Handeni.


Baada ya vipimo vya daktari, mwanamke huyo alikutwa na malaria na kulazwa kwenye hospitali hiyo kwa matibu.


"Huyu bibi harusi alijifungua Alhamisi mtoto wa kiume baada ya kubeba ujauzito wa miezi saba, lakini ghafla Alhamisi alipata homa tukampeleka hospitali ambako alilazwa, akakaa Ijumaa na Jumamosi saa 8.05 alikafariki dunia wakati akisubiriwa kwenda kanisani kufunga ndoa ambayo ilikuwa ifanyike saa 9.00 alasiri siku hiyo.


“Inasikitisha sana ila imeshatokea yaani marehemu amefariki siku moja kabla ya ndoa yake, ndoa ilikuwa ifungwe saa 9:00 naye akafariki saa 8:00 na mtoto wake naye alifariki muda mfupi baada ya mama yake kufa,"amesema Mrimasha.

Akizungumzia tukio hilo Mwenyekiti wa kamati ya harusi hiyo Abdi Kipacha amesema tukio hilo ni la kwanza kwake tangu kuzaliwa na kamwe hawezi kulisahau.


Amesema kamati zote zilishamaliza maandalizi ya harusi ila ghafla wakapewa taarifa kwamba bibi harusi amefariki dunia.


“Nilipanga kamati zangu zote na kuzipa majukumu yao, tulichokuwa tukisubiri kuambiwa kama bibi harusi ataweza kuja, lakini ghafla tukapewa taarifa kwamba amefariki dunia, ilikuwa ni vigumu kuamini, lakini ni kweli imetokea na inasikitisha kwani si jambo la kawaida,”amesema Kipacha.


Marehemu alikuwa Mwalimu wa Shule ya msingi mkoani Lindi. Mwili wa bibi harusi huyo ulisafirishwa jana kupelekwa Machame mkoani Kilimanjaro kwa mazishi ambayo yatafanyika leo Jumatato.

Kwa habari zaidi kuhusu masuala yanayo husiana na imani pamoja na ulimwengu usio onekana, afadhali tembelea : Blogsop.com: The Leading Internet Site on the Net
 
Malaria is an avoidable and curable disease.
Alazwe pema peponi Biharusi.
 
Malaria is an avoidable and curable disease.
Alazwe pema peponi Biharusi.
Mwali Tanga unapasikia au ? haya mambo yenu ya Pwani ukiingiliwa koloni lako unammaliza yeyote
Huyo Mwanaume aseme ukweli alikuwa na nhusiano na mwanamke gani? maana hata km ni Bibi kizee huwa hakiachiki
Namuonea huruma Manka Levina Mmasi MUNGU AMUWEKE MAHALI PEMA PEPONI na awape ujasiri Familia yake kwa kumpoteza Bint AMEN
 
Last edited by a moderator:
Hicho ni kifo cha kawaida kutokana na Malaria na kila siku vinaendelea kutokea wala hakuna cha juju wala ishirikina hapo. Tatizo hapa ni 'Timing' ya kifo hicho ambacho kilitokea siku na saa wasiyoitarajia watu.
Malaria ni hatari kabisa haswa kwa watoto na waja wazito kama ilivyotokea kwa huyu Binti aliyempoteza mtoto wake na yeye mwenyewe kufariki.
Hii ndiyo sababu kuu ya kampeni kubwa zinazoendelea hapa na duniani kote dhidi ya ugonjwa huu hatari.
 
huyo mwanaume atakuwa anahusika kama alikuwa hana mwanamke aliyemtenda akamwacha ndio akamwoa huyu basi ndio kafanya haya .si bure wala malaria hiyo .wanaume wanaume
 
Haya sasa ndiyo MAJANGA!!! Pole kwa wana ndugu na Bwana Harusi ambaye kapoteza mke-to be!!
 
Hicho ni kifo cha kawaida kutokana na Malaria na kila siku vinaendelea kutokea wala hakuna cha juju wala ishirikina hapo. Tatizo hapa ni 'Timing' ya kifo hicho ambacho kilitokea siku na saa wasiyoitarajia watu.
Malaria ni hatari kabisa haswa kwa watoto na waja wazito kama ilivyotokea kwa huyu Binti aliyempoteza mtoto wake na yeye mwenyewe kufariki.
Hii ndiyo sababu kuu ya kampeni kubwa zinazoendelea hapa na duniani kote dhidi ya ugonjwa huu hatari.
Wewe mtoto mdogo kakojowe ukale, this is too big for you, hakuna ulijuwalo Dunia hii.
 
Hiyo ni mipango ya mungu.
Ujinga huu hata shetani ana mipango....

Huyo labda ni Mungu wako peke yako ambaye anaweza kumchukuwa mama na kichanga siku moja, Mungu wangu mimi anawachukia sana binadamu wazembe na wavivu wa kufikiri kama wewe.
 
Poleni sana wafiwa. Mwenyezi Mungu apumzishe roho zao kwa amani. Ila ndugu zangu nilichogundua hapa ni kwamba bibi harusi hakuwa na nguvu ya kuhimili mikiki ya sherehe kwa sababu alikuwa ni mzazi wa wiki 1 tena pre-mature, bado na malaria juu,ni kwamba bado alikuwa mgonjwa maana alikuwa kalazwa. Sina hakika alivyoruhusiwa alikuwa kapona au ni nguvu ya ndugu ili awahi kwenda kujiandaa na sherehe. Hapo alitakiwa awe amejipumzisha na mtoto sherehe haikuwa na ulazima kwa wiki hiyo. Ila yote tumwachie Mungu kwani kazi yake haina makosa
 
Ujinga huu hata shetani ana mipango....

Huyo labda ni Mungu wako peke yako ambaye anaweza kumchukuwa mama na kichanga siku moja, Mungu wangu mimi anawachukia sana binadamu wazembe na wavivu wa kufikiri kama wewe.

Mungu wako yeye anapatikana wapi?
 
Tanga kwa uchawi noma kuna jambo hapo waingie kwenye Maombi co bure kuna mkono hapa.
 
Back
Top Bottom