Bunge linaloendelea na vikao vyake mjini Dodoma, leo katika kikao chake cha jioni limelazimika kuahirishwa kutokana na mahudhurio hafifu ya wabunge hususani wa CCM. Tatizo hili limekuwa sugu, halirekebishiki. Wananchi wamekuwa wakilalamika juu ya mwenendo huu wa bunge. Wananchi wamesahau ghafla na mapema mno kwamba wabunge wa CCM (takribani wote yaani 100%) waliununua ubunge huo na hawakutumwa bungeni na wananchi.
Wabunge wa CCM waliununua ubunge huo kwenye kura za maoni ili chama chao kiwapendekeze kugombea ubunge; waliununua ubunge huo kwenye kamati kuu ya chama chao ili majina yao yapitishwe kugombea ubunge kwa tiketi ya chama chao; waliununua ubunge huo wakati wa kampeni za uchaguzi; waliununua ubunge huo wakati wa kuhesabu kura; waliununua ubunge huo wakati wa kutangazwa matokeo.
Kwa mantiki hiyo, hakuna mbunge wa CCM atakayewajibika kwa wananchi wa jimbo lake. Wabunge hawa wanawajibika kwa chama chao kwa kuwa chama ndicho huwajengea mazingira ya kuununua ubunge.
Hivyo basi, mwananchi uache kuwalaumu wabunge kwa kutokukuwakilisha bungeni. Jilaumu mwenyewe kwa kukubali kununuliwa na wabunge hao kwani, ninapomlipa mpiga zumari uchaguzi wa wimbo wa kuchezwa uko kwangu. Tujifunze kwa watu wa kusini kuanzia vijana hadi ajuza pasipokujali itikadi za vyama wala dini wameonesha kugutuka. Sauti ya radio Ujerumani inasema "VIJANA TUGUTUKE". Mwaka 2015 sio mbali tuchangamkie daftari la kudumu la wapiga kura. Duniani kote, ukombozi huanza na kutimilizwa na vijana, HAKIKA VIJANA TUGUTUKE!