KiwandaniTz
Member
- Jan 8, 2019
- 44
- 38
Asante mkuu, ubarikiweWazo lako la kupanua wigo wa kibiashara ni zuri
Nimewahi kuifanya hii biashara miaka 5 iliyopita kwa Dar, haikunipa matunda sana nikaamua kuacha.
Sababu kubwa ilikuwa udalali kama kawaida zilivyobiashara nyingi za Dar.
Sababu ya pili ni soko jinsi unavyonunua na kuuza ni tofauti.
Mwanza utanunua kwa debe ila Dar utauza kwa kilo soko halitambui kipimo cha debe.
Changamoto inakuja kwenye aina ya dagaa na uzito utakaotoa, kuna uwezekano mkubwa sana wakukupoteza mtaji.
Unakonunua unakutana na madalali lazima wakupige unakoenda kuuza pia unakutana na madalali lazima ule nao, hapo unategemea utapata nini? mbaya zaidi uwe mgeni kabisa katika hii biashara na dagaa hauwajui vizuri.
Kwa upande wa Tunduma ndipo ninapopatikana ila sijawahi kuifanya huku, lakini nimewahi kufatilia jinsi soko lilivyo ikohivi;
Tunduma wananunua na kuuza kwa debe kama ilivyo Mza, bei ya sasa sifahamu mpaka niulizie.
Unatafuta mtu wa kufanya nae biashara unamtumia mzigo anauza kisha anakutumia pesa kulingana na makubaliano yenu
Wafanyabiashara wengi huku wanamiliki stoo ila mtaji wa mzigo hawana, wenye mitaji mikubwa wanafata wenyewe na kuwasambazia wenye stoo wasiyokuwa na mtaji kwa mali kauli.
Kwahiyo usiwe na matumaini makubwa sana kwamba utapiga hela kwa muda mfupi sababu tayari kuna watu wameshatengeneza falme zao katika biashara hii, labda uje na mbinu na mawazo mapya.
Biashara ya dagaa hapa haijachangamka sana na wanunuzi wakubwa wa hii bidhaa ni jirani zetu Wazambia na Wakongo, lakini kwa upande wa Wazambia wanapendelea zaidi furu wale samaki wadogo wadogo wanaochambuliwa toka kwenye dagaa nafikiri unawafahamu.
Hivyo kama utakuja angalia soko la furu huko Mwanza na huku Tunduma, lakini ukiweza angalia pia soko la vibambara vya sangara havipo huku.
Aina ya dagaa wenye bei huku ni wale wa nyasi wanatoka Bukoba na wale wa mafuta waliyokaangwa
Kuhusu usafirishaji mwaka 2017 kwa gunia moja la dagaa toka Mwanza mpaka Tunduma ilikuwa 7000 kwasasa sifahamu, Utauliza huko Mwaloni(soko la dagaa) Mwanza.
Mwisho japo siyo kwa umuhimu;
Karibu Tunduma border ya wajanja lango kuu la nchi 8 za SADEC Tanzania.