Bi Maunda Plantan ndiye mwanamke wa kwanza kutangaza radioni

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
21,142
30,493
BI. MAUNDA PLANTAN NDIYE MWANAMKE WA KWANZA KUTANGAZA SAUTI YA DAR ES SALAAM

Bi. Khadija Said ni mama yangu nafungua macho namuona akiishi Mtaa wa Narung'ombe na huku Swahili na huku Sikukuu na katikati ni Mtaa wa Gogo.

Mtaa wa Gogo kulikuwa na nyumba yetu halikadhalika Mtaa wa Swahili na Mtaa wa Sikukuu.

Mwanae Bi. Khadija Said, Said Albati alikuwa umri wangu na tukicheza pamoja.

Baadae Bi. Khadija Said alihama Narung'ombe akahamia flat za NHC Morogoro Road.

Hapo zilipojengwa hizo flat za NHC katika nyumba zilizovunjwa kupisha ujenzi wa nyumba hizo ni nyumba ya akina Madohora - Madohora kaka mkubwa alikuwa mpiga picha maarufu Dar-es-Salaam, Abdallah na Haidar.

Haidar yeye alikuwa umri wangu na alikuwa na marafiki wengi Mtaa wa Gogo na akija kucheza mpira na sisi siku za likizo ya shule.

Haidar aliinukia akawa mlinda mlango wa kutegemea Dundee Club iliyokuwa Mtaa wa Livingstone jirani sana na nyumbani kwao hapo Morogoro Road.

Katika wachezaji watoto wa Dar-es-Salaam ambao walikuwa na kipaji kikubwa cha mpira alikuwa Omar Issa akicheza mbele katikati Dundee.

Miguu ya Omari Issa ilikuwa imeangalia nje sijui kama ni kwa haya maumbile au nini Omar akishika mpira huwezi kumnyang'anya na endapo beki atatumia nguvu matokeo yake ni kusababisha penalti.

Mwaka wa 1998 nilikuwa pamoja Hijja na mama yangu Bi. Khadija Said chini ya Tanzania Hajj Trust.

Lakini ukweli ni kuwa Khadija Said si mwanamke wa kwanza kutangaza.

Mwanamke wa kwanza ni Bi. Maunda Plantan aliyekuwa Sauti ya Dar-es-Salaam mwanzoni kabisa kilipofunguliwa kituo hicho mwaka wa 1952.

Bi. Maunda akitangaza upande wa Kiingereza.

Picha ya kwanza ni Bi. Maunda Plantan na ya pili ni Bi. Khadija Said.

1659638700278.png
1659638723830.png
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom