Benki hii ya Tanzania hovyo sana

eddy

JF-Expert Member
Dec 26, 2007
15,079
10,032
Jamaa yangu mmoja alihitaji kupeleka watoto wawili shule na mke wake, watoto walipaswa kwenda kuchukua shahada ya kwanza na mkewe shahada ya pili maarufu kama masters, watoto wenyewe ni hawanasifa/wazaziwanauwezo na hawakuweza kupata mkopo wa Ndalichako.

Jamaa yangu akaona isiwe tabu kaamua kwenda Bank kusaka mkopo kwani kamshahara kanaruhusu kukopa Bank, kufika Bank walimwambia asiwe na shaka na atapata mkopo ndani ya wiki moja, jamaa haraka haraka akajaza form na kuziwakilisha kwa wakati, hadi leo hii miezi miwili imepita hakuna cha mkopo wala jamaa yake mkopo. mabinti zake na mkewe wote wako nyumbani wanasubiri ada.

Jamani Mabenki kama hamna hela semeni kuwa hela hamna na sio kuhangaisha watu, mungemwambia tangu mwanzo kuwa mikopo hamtoi angeuza hata shamba apeleke wanae shule.

Jirani yangu nae yale yale alifiwa na mumewe mwezi wa tano haya kijana anatakiwa aende chuo kaambiwa bila ada hamna udahili na mwisho wa udahili wiki hii,mkopo wa bodi nao kaambiwa eti babake anauwezo sijui huo uwezo hakuzikwa nao! imebidi auze gari la babake kwenye chuma chakavu angalau kapata nusu ya ada.

Hebu tuondoe mawazo ya kubomoa nyumba kando kando ya barabara tuingize mawazo mapya yenye tija kwa ustawi wa watanzania. Nanyie maafisa mikopo kama hamna hela semeni hamna hela basi, itafika wakati itabidi tuwapeleke mahakamani kwa uongo kazini.
 
Ungetaja bank sasa unasababu gani kama hutaki kuitaja?
Tulia tu naendelea kukusanya ushahidi wa kutosha lazima tuwafikishe kisutu kwa pilato, kama kuna mwingine kafanyiwa ushenzi huu tuwasiliane, hawa watu washachuma faida za kutosha washaanza kutuletea madharau.
 
kisa cha kwanza unasema walikosa mikopo (loan board) zaidi ya miezi 2 iliyopita,hivi unajua majina ya loan board yametoka takriban mwez 1 tu uliopita?
 
Moes, jamaa yangu alifanya mchakato mapema akijua akikosa mkopo wa bodi basi atapata mkopo wa benki apeleke wanae shule sasa vyote kakosa, mkopo wa benki na bodi na huko kote aliahidiwa angepewa wamemchomolea dakika za mwisho, sasa kama serikali inapesa za kutosha siwawapatie na wanafunzi wote?
 
Back
Top Bottom