Trust None
JF-Expert Member
- Feb 12, 2018
- 1,260
- 4,418
Mchezo unaoendelea kwa sasa ni wa kuangaliwa kwa jicho la tatu. Tume huru inaandaliwa lakini kwa manufaa ya CCM. Wapinzani tafakari kama mnaweza kuishinda CCM katika mazingira haya:
Iwapo Membe ataenda ACT, basi wana CCM wasiompenda Magufuli na wana CHADEMA wasiokipenda chama chao, watakuwa upande wake.
Iwapo uchaguzi utacheleweshwa ili katiba mpya iandaliwe, basi Membe anaweza kugombea kama Mgombea binafsi (ili azigawe kura kama nilivyoeleza hapo juu).
Kwa mazingira kama haya, Tume huru itakuwepo na mshindi atatangazwa kihalali na atakuwa JPM.
Ikumbukwe kuwa CCM bado ina mtaji mkubwa wa wapiga kura miongoni mwa wananchi wa vijijini na wazee. Vijana wote na wasomi watajigawa kwa Membe na kwa Lissu, hivyo kumpa Magufuli nafasi kubwa ya ushindi.
1. BENARD K MEMBE (ACT/PRIVATE CONTESTANT) ...X
2. JOHN J.P MAGUFULI ...√
3. TUNDU A.M LISSU ...X
Lengo si Membe kuwa Raisi bali CCM kubaki madarakani.