Beki wa Simba SC, Che Malone apata ajali ya gari Mikocheni karibu na Feza School

1979Magufuli

JF-Expert Member
Feb 20, 2023
438
1,752
Nimepata taarifa beki wetu kisiki kapata ajali maeneo ya Mikocheni, alipokwenda kumpokea ndugu yake usiku wa kuamkia leo, Septemba 24 ambaye amekuja kumtembelea.

Sikusudii kuleta taharuki isipokuwa nimewasikia watu wakisema katika daladala, pole ukuta wa Yericko kama ni kweli.

UPDATE
Taarifa za awali zinadai hakuumia wala kupata majeraha, lakini abiria mmoja aliyekuwa pamoja nae ndie aliumia. Hata hivyo, amepatiwa matibabu na kuruhusiwa kuondoka hospitalini asubuhi hii.
 
TAARIFA YA CHE MARLONE KUPATA AJALI MBAYA MIKOCHENI...

Asubuhi ya leo wakati nikienda mazoezini nimekuta gari ikiwa imepata ajali mbaya eneo la Mikocheni pale Fezza....

Nilijiuliza na kuwaombea waliokuwemo sababu gari limeharibika vibaya.

Baadaye nimepewa taarifa beki Che Marlone wa Simba ni kati ya wahanga wa ajali hiyo na alikimbizwa hospitali kuangaliwa na nimeelezwa hakuumia ila dereva kaumia sana.

Chanzo: Adventure-360

Pole yake
 
Anatoa taarifa kama nani??yeye ni msemaji wa Simba?
Duh mkuu umeamka na hasira zako au jamaa ulikuwa unamtafuta kwa muda mrefu leo kaingia kwenye anga zako?
Humu kuna taarifa ngapi zinatolewa na wadau na watu wanazipokea na mwisho zinakuja kudhihirika ni za ukweli. Na taarifa nyingi zinaletwa humu sio zote zimetokea kwa msemaji au kwa ukurasa rasmi wa timu lakini zinakuja kama tetesi na zingine zinakuwa ni sahihi na zingine sio sahihi. JF ni moja ya chombo cha habari mkuu
 
Sasa itakuwaje mechi na Dynamos? Maana Inonga nae ameumia na atakuwa nje kwa siku 14...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom