BBC: Rais Kikwete aruhusu Majasusi kutoka nje kuja kuchunguza mauwaji ya Viongozi wa Dini Zanzibar

Status
Not open for further replies.
Je unauhakika kauwawa kwa sababu za kidini? kumbuka yeye ni binadamu tusihukumu tusubiri ripoti kamili.

je wewe mkuu unao uhakika kuwa hawakufanya kwa sababu za kidini?
je kama ni majambazi padri alikuwa na pesa gani za kuiba? au mali gani za kuibwa?
 
je wewe mkuu unao uhakika kuwa hawakufanya kwa sababu za kidini?
je kama ni majambazi padri alikuwa na pesa gani za kuiba? au mali gani za kuibwa?

Ndio maana tunatakiwa tungoje ripoti, kuuwawa si kwa ajili ya pesa tu kwani kamanda Barlow aliibiwa shilingi ngapi, Profesa Mwakyusa, Je? tusiwe na haraka zinazopelekea tuwe na Jazba tutukane na dini nyingine bila kuwa na uhakika. Kumbuka yeye alikuwa binadam na anaishi na jamii pia. Lolote linawezekana mwenyezi mungu atuongoze vyema kwa hilo hili tuvuke salama.
 
Mtu aliyetoa hili wazo la kuleta majasusi toka nje, na yule/wale waliolikubali hawakufikiria vizuri. Huhitaji kuwa brain surgen kugundua hii hatua italeta mtafaruku ndani ya taasis ya usalama. Hapa ni wazi wazi wamedharauliwa kwa sababu kila kitu kinajulikana, na kama ulivyosema tahadhari ilitolewa asubuhi na mapema. Sasa majajusi wa nje wanakuja kufanya nini kama si kuonesha madharau kwa wanausalama wetu?

Sambamba na madharau haya, wanausalama wanaweza kuasi na hapo ndipo wakubwa watajua nini maana ya 'busara'. Tanzania inao uwezo wa kutatua hii kero bila ya kuegemea majasusi wa nje. Gazeti la Mwanahalisi tu wangeweza kufanya upelelezi mzuri kabisa. Utani mbaya sana huu, ni bora watu wangejiuzulu.

Wadau kirusi cha udini ni hatari zaidi ya mnavyofikiri-ndani ya msukumo wa dini hata surbodinate wako huna uhakika atakavyotekeleza jukumu ulilompa.Jaribu kufikiria pale Nchimbi anapotakiwa kuunda kikosi cha uchunguzi composition yake iweje??akichagua wakristo watupu-majibu yake yakaonesha ni kikundi cha kiislamu kimeshiriki waislamu watachukulia vipi!au ukichanganya dini zote ndio itakuwa njia kusubotage ushahidi upotee?Hii ndio ile situation huwa tunalaumu polisi kujichunguza wenyewe,na kwa hili la dini kila mtu anaweza jikuta anachukua upande.
In reality situation iko very delicate ndio maana viongozi wametoa matamko mengi.Tulianza kuingia kidogo kidogo kwenye udini bila hatua kuchukuliwa kutokana na zile siasa zetu za kuridhisha kila upande hata kama mpaka mawe yanamjua mkosaji!!! sasa ni dhahiri tunaanza kufikiri na kutenda kidini.Udini huathiri kila kabila at once ingawa Ukabila unaweza usiathiri kila dini
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Ndio maana tunatakiwa tungoje ripoti, kuuwawa si kwa ajili ya pesa tu kwani kamanda Barlow aliibiwa shilingi ngapi, Profesa Mwakyusa, Je? tusiwe na haraka zinazopelekea tuwe na Jazba tutukane na dini nyingine bila kuwa na uhakika. Kumbuka yeye alikuwa binadam na anaishi na jamii pia. Lolote linawezekana mwenyezi mungu atuongoze vyema kwa hilo hili tuvuke salama.

sawa tungoje riport lakini ingekuwa ni kiongozi wa kiislamu nafikiri tusingengojea riport ya mtu yeyote ila ungeona kile ambacho kingetokea ila wakristo tungoje riport.
haya mkuu tungoje riport kutoka kwa majasusi.:shut-mouth:
 
Katika kile kinachoonekana jeshi la Polisi nchini kukosa imani tena kwa jamii serikali imeridhia uchunguzi wa mashirika ya kijasusi toka nje. Ili kujua nani yuko nyuma ya kadhia hiyo.

Concern
Hapa najua wanataka kuwatupia watu wa nje lawama nahakika wanajua nani anaendesha mauwaji lakini unafiki wa kukamatana ndo unawasumbua hawa serikali. Uchunguzi ukitoka utawasikis "kulingana na uchunguzi wa kijasusi toka nje umebaini.........." Ili wao waonekane sio walio watia hatiani watuhumiwa.

Wenje aliwahi kusema hawa watu ni narrow thinkerz wakadai anawatukana,Tz ina Usalama wa taifa,polisi,jwtz,vikosi vyasmz vyote vimeshindwa?Hakika nchi hii imekosa mtu wa kututoa hapa tulipo na tumekwama kwelikweli
 
Bila shaka hawa makachero watakuwa wanalipwa mshahara kwa kodi za walalahoi wa Tz. Watu wa usalama Watz wana kazi gani!? Au kazi yao ni kula bata na kunenepeana tu!! Uvumilivu utakapofikia kikomo, nchi hii patakuwa hapatoshi!! Dhaifu na wenzake wote watatimkia Ughaibuni wawaachie wenye uwezo waiongoze!!!
 
Sasa kwanini mauaji ya R.P.C mwanza hawakuitwa F.B.I ??? Au padre ni zaidi ya R.P.C? Au vipi?
Hata mimi nimeshangazwa,ni kama wamefanya uamuzi wa ghafla!Juzi taarifa ya ikulu ilisema Rais kayaagiza mamlaka ya juu kabisa ya jeshi la polisi kufanya uchunguzi.Na haukupita muda wakatoa taarifa ya kuwa tayari kuna watuhumiwa watatu wanaoshikiliwa,hata hivyo hawakutajwa majina yao.

Sasa leo limekuja hili la majasusi kutoka nje.Pengine serikali na vyombo vya usalama wanahisi kuwa imani ya wakristo kwao imepotea.

Pia pengine either hawana ujasiri wa kulishughulikia,ama wanataka kuiua issue katika mazingira kama yale ya EPA ama kubuy time ili ijifie,hilo halitawezekana kama udini hautakwisha.

Hata FBI ikitoa hiyo ripoti,bado serikali inaweza kuikalia tu.Hivyo ninaamini kuwa kusema vyombo vya nje vya kijasusi vitachunguza ni njia ya kuituliza issue pembeni kwani ni too hot.Ni sawa na ule usemi wa "ugali moto mboga moto"
 
TISS, CID na CMI ya kwetu imesomea kuiba kura, kudhibiti wapinzani na waandishi wa habari. Mambo ya kupeleza matukio kama haya hayakuwepo kabisa kwenye mtaala wao. Msiwaonee bure. Tanaza tender ya ku source out activity hii kama kazi za osafi maofisini. Si tumekubali mpango wa Private Sector Participation.
Hii ni aibu ina maana CID,TISS,CMI hakuna coordination yoyote ya kunusa na kuzuia hatari kizalendo?

Kuruhusu majasusi wa nje ni kukiri kwa serikali kuwa system imefeli!

Then tunachukua hatua gani maana hiyo ni 100% indicator hatupo salama tena!
 
Nchi hii haihitaji usaidizi toka nje, vyombo vya upelelezi na ujasusi vilivyopo
vina uwezo na weledi wa kufanya uchunguzi.
Vinginevyo viwe vinahusika kwa njia moja au nyingine na kadhia hii..
 
Hahahh! My ribs. Yaani unataka na Raisi pia atoke nje. Duh nimecheka sana. JF daima

Hebu, can you imagine, enzi za Nyerere na matatizo yote tuliyokuwa nayo ya kupigania uhuru Msumbiji na Zimbwabwe eti rais anaomba makachero kutoka nje? Mbona tuliweza kuwabana Makaburu na Wareno? Leo huyu rais omba omba anafikiria kila kitu chenye uwezo kinatoka nje. Ameharibu intelligencia yetu kwa kuwatumia kuwaulimboka watu sasa anaomba intelligencia ya nje. Hakuna laana mbaya kama kutawaliwa na taahira.
 
asante hiroshima. Huyu jamaa simpendi hasaa yeye tamaa zake za uraisi ndie aliwafata mashehe akiwa na mchawi mwenzie makamba. Wakawaingizia mashehe udini vichwani mwao leo hii anaropoka nini hapa. Kwann makachero toka nje inamaana usalama wa taifa hawaiwezi hii kazi?????pumbaf kabisa

tuko uchi tayari tutafunuliwa wee maskini tanzania u better rudi from mkwawa war then mirambo then majimaji ili muwe kwenye sense.
 
Zote porojo tu, binadamu tumeubwa na moyo wa kusahau, wanatoa matamko mengi ili tusahau baada ya mengine kutokea, Fastjet anaamini kuwa huo ni upepo, so utapita. Lakini kwenye hili hata wasipofanya uchunguzi naamini hata kanisa lina wajibu wa kufanya uchunguzi na kuiambia jamii kama serikali haitaki kuitimiza wajibu wake, naamini hilo linawezekana.
Hata mtu binafsi likikusibu jambo lazima uchukue hatua sitahiki, sembuse kwa taasisi kama kanisa Katoliki, hata kwa maombi inawezekana pia.

Kila la heri serikali, ila punguzeni sarakasi, maana taarifa zilizopo ni chanzo tosha kuanzia uchunguzi. Kusanya wote weka ndani watasema yote, wengine wametoa DVD na kuzisambaza kila kona ya nchi naamini hata pale kwenye jengo jeupe Magogoni zipo tena nyingi, waseme wametumwa na nani, nani anawafadhiri nk. Haiingii akilini intelijensia ya Tanzania iwe active kwa CDM & CUF tu, kwingineko inashuka hadi negative bila kujali wingi wa taarifa zilizopo mitaani hadi watu kama mimi wenye ujuzi ziro wa ulinzi nazisikia, je watalaamu waliobobea wanatuambia nini wao, inatia kinyaa kuwasikiliza hawa jamaa tuliowapa madaraka.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom