BBC Idhaa ya Kiswahili Wamechoka!

Ibrah

JF-Expert Member
Mar 22, 2007
2,729
528
Katika redio za kimataifa zinazopendwa nchini ni Idhaa ya Kiswahili ya BBC LOndon. Kwa kweli tangu aondoke Tido Mhando kama Mkuu wa Idhaa hiyo, viwango vyao vimeporomoka sana na ingawa husikiliza BBC Idhaa ya Kiswahili kila siku bado sivutiwi na utendaji wao wa kazi hasa Watangazaji wao wa siku hizi huko London na Nariobi.

Kuna baadhi ya watangazaji wa Idhaa hiyo ambao lugha yao ya kwanza si Kiswahili na hutumia Kiswahili kibovu (simaanishi lafudhi bali broken swahili). Kama ingekuwa ni Wawakilishi wao wa nchi za Uganda, Somalia au Kongo nisingeshangaa lakini ni baadhi yao ni Waajiriwa kabisa hapo HQ London!

Kero nyingine ni tabia iliyozuka siku hiozi ya Idhaa hii kuturushia matangazo yalliyorekodiwa siku moja au mbili. Mfano ni kipindi cha michezo siku moja kabla ya mechi ya Man Utd na Arsenal ambacho walikirusha tena siku ya jumatatu asubuhi!

Kwa kweli walini-bore sana. Yaani walishindwa kuandaa kipindi! Ni afadhali wasingekuwa na kipindi cha michezo siku hiyo kuliko kutuambia ati kesho kutakuwa na mechi kali baina ya Man U na Arsenal wakati mechi ilichezwa jana!
 
Mkuu,

Nadhani wewe ni "Gunners for Life"!

BBC bado iko juu SAAAAAAAAAAAAAANA
 
watangazaji wengi wnaboa ni kweli,hakuna msisimko km kina tido,ali salehe,ali adnan,vick ntetema etc!
 
Ibra upo ukweli kiasi kuwa BBC hii idhaa ya kiswahili ina mabadiliko makubwa ambayo yanashangaza ambayo huu mkurugenzi mpya ameyaanzisha akiwa na lengo la kuboresha , kumbe mengine anajikuta akiharibu zaidi.

Mimi ambacho kilinikwaza tangu miaka ya Tido ni harakati za kuhamishia idhaa hii hapo Nairobi, kuna wakati waandaaji hujisahau na kudhani kuwa hii ni redio ya Kenya kwa kutumia zaidi ya dakika kumi na tano kuzungumzia issues za Kenya ....hapa naizungumzia Amka na BBC.

Kipindi unachotaja cha michezo, lilikua kosa la kiufundi lakini si kweli kuwa BBC asubuhi huwa wanakuwa na michezo iliorekodiwa siku mbili kabla....

Otherwise naona bado iko juu, kulinganisha na idhaa zingine za kimataifa zitumiazo Kiswahili kama DW., VOA, Radio sauti ya Japan, Radio ya South Afrika nk.
 
Hili la kutumia muda zaidi kwa issue za Kenya ni kweli hasa kwenye amka na BBC.
 
you are right to the point, BBC is just all about Kenya! I stopped listening to AMKA na BBC!
 
Hili la kutumia muda zaidi kwa issue za Kenya ni kweli hasa kwenye amka na BBC.

Sasa ninyi mnataka BBC itangaze nchi yenu (TZ) au habari?

Mkiwa na habari mtatangazwa! Vinginevyo watatangazwa wanyarwanda, wakenya na hata waganda; kama majukumu yao yanatengeneza habari.

Men, be accountable; acha kulalama! Sidhani iwapo Karume au Vuai wanazo habari kwa ajili ya BBC kutangaza, labda waendelee kugombea mafuta yatakayopatikana Zanzibar mwaka 2500 na kuchimbwa mwaka 3000!
 
Hapa mkuu umeboa......
 
Mimi nina zaidi ya mwaka sasa sisikilizi idhaa ya kiswhili ya BBC,wanachofanya sasa ni zaidi ya kuboa!kitu cha kwanza hawajui kiswahili, kuna siku dada mmoja anaitwa Alice Muthengi kwenye amka na bbc alianza kuongea kikamba!!!Pili, hawana sasa hata ubunifu wa kuboresha vipindi vyao ukiachilia mbali upendeleo wa habari za kenya. Pia lipo tatizo la kutosoma sms za wasikilizaji hasa zile zinazowakosoa,this is a weakness so far!
 
nimekupata mkuu. BBC kuna watangazaji wasio na ustaarabu kabisa katika matamshi ya lugha yetu adhimu. pia vipindi vingi vya documentary huchukuliwa kenya. Halafu, kama Tido alikuwa nguzo pale BBC mbona huku TBC anashindwa kuiboresha?
 
Kama una malalamiko au unamapendekezo watumie ujumbe wa maandishi kwa email. Ni kweli kama hakuna habari hawawezi kutangaza. Ni kweli pia Kenya kuna reporters wengi kuliko TZ na habari nyingi hupatikana. TZ kuna reporters wachache ama waliopo pia wanatumia muda mwingi kufanya kazi zao badala ya kutafuta habari. Pia BBC hawatangazi habari za umbea ambayo hawajaweza kuthibitisha upande wa pili au source yake. Je lini mmesikiliza TBC mara ya mwisho?
 
Mkuu ukiona hao wanakuboa hamia radio Bonny Ujerumani utakutana na kina Sudi Mdete, Umiry Heth na wengineo....
 
kweli kabisa nami nimeaacha kuisikiliza kabisa, msishangae nilikuwa naisikiliza tangu nipo darasa la tatu mwaka 1993 hadi nikiwa varsity mwaka jana.
kuna dada mmoja huwa anasoma sms hawezi kabisa kutamka neno ukimwi hata alitaje neno hilo mwezi mzima, sijui anaongea kilugha chao au vipi?
KWA UFUPI WANABOA PIA SIKU HAWANA MADA NZURI HATA MOJA.
 
jamani kumbukeni KBC ina hisa nyingi BBC swahili, ndo maana wanalonga zaidi issues za kenya.
 
Kama una malalamiko au unamapendekezo watumie ujumbe wa maandishi kwa email. Ni kweli kama hakuna habari hawawezi kutangaza. Ni kweli pia Kenya kuna reporters wengi kuliko TZ na habari nyingi hupatikana. TZ kuna reporters wachache ama waliopo pia wanatumia muda mwingi kufanya kazi zao badala ya kutafuta habari. Pia BBC hawatangazi habari za umbea ambayo hawajaweza kuthibitisha upande wa pili au source yake. Je lini mmesikiliza TBC mara ya mwisho?

Uko sahihi, kama mtu una malalamiko basi tuma ujumbe kwao wenyewe ili waufanyie kazi. mimi binafsi nawaaminia sana BBC.
 
Mimi pia nafikiri BBC wanatusaidia sana kuliko hata TBC kwa sababuwana tafuta habari hadi vijijini kuliko maredio yetu ya kizembe. BBC ongezeni bidii na nawapongeza sana.
 
BBC has lost its charm after Tido left! I do noit listen to Amka na BBC but these days I find D WELLE kiswahili better my favourite is UM AL KHAEIR..Her voice is tantalizing!
BBC is gone finished it is concentrating more on PERSIAN SERVICE where thya ahve put all the money to overthrow IRAN and Kiswahili service is gettign a token ndiyo maana their Kiswahili is like CREOLE!!!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom