Basi la NAJMA lapata ajali kwenye Daraja la Mkapa

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,894
20,372
Bus la kampuni ya Najma linalofanya safari zake kati ya Dar es salaam na Nachingwea, limepata ajari kwenye daraja la Mkapa, Ikwiriri baada ya kugonga pikipiki na kusababisha vifo vya watu wawili hapohapo.

Chanzo cha ajali hiyo ni moshi mkali uliotanda kwenye eneo la ajali kutokana na moto uliokuwa unaunguza majani yaliyopo pembezoni mwa barabara ya kusini mara baada ya kumaliza daraja la mkapa.

Basi hilo lilikuwa linatokea Nachingwea kwenda Dar es salaam. Watu waliofariki ni walewaliokuwa kwenye pikipiki. Ajali hiyo imetokea majira ya saa 6:40 mchana. Hata hivyo gari hilo halikupinduka isipokuwa imeharibika vibaya sehemu ya mbele.

Baada ya ajali hiyo, dereva alisogeza gari kwenye kituo cha polisi cha Ikwiriri na baada ya kutoa maelezo, polisi wameenda eneo la tukio kuchukua maiti. Mtoa habari hii ni miongoni mwa watu waliokuwa abiria kwenye basi hilo.

Namba ya gari ni T 599 CBL aina ya YUTONG.
 
Poleni sana wote mlioguswa na ajali hiyo.
Mungu Awalaze Pema wenzetu waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo.
Mungu Awatangulie kwenye safari yenu kwa kuwa bado hamjafika muendako.
Hivi haya majanga ya ajali mpaka lini???
 
pikipiki zinatumaliza jamani zimesajiliwa 10000 tra, ajali january 2013 mpaka sasa zimeua watu zaidi ya 1000.
 
Poleni sana wafiwa na majeruhi wa ajali. Mwenyezi awajalie nguvu ya kukabiliana na hiyo hali na kupona haraka!
 
pikipiki zinatumaliza
jamani zimesajiliwa 10000 tra, ajali january 2013 mpaka sasa zimeua watu
zaidi ya 1000.

sure mkuu. maana hawa jamaa hawako makini sana wawapo barabarani na hawachukui hatua za kiusalama
 
View attachment 102254

Hapo pikipiki inaonekana ikiwa na baiskeli. Kutokana na maelezo ya wenyeji wa hapa Ikwiriri ni kwamba, mmoja wa marehemu ni mkulima ambaye anaishi kando ya hapa ikwiriri. Alikuja Ikwiriri leo asubuhi kuuza maboga. Baada ya biashara yake kukamilika na wakati akijiandaa kurejea nyumbani, aligundua kuwa baiskeli yake ina hitilafu. Akaenda kwa fundi baiskeli kuitengeneza. Baada ya matengelezo aliamua kukodi hiyo pikipiki ili arudi haraka nyumbani akachukue mzigo mwingine. Inadaiwa pia kuwa dereva pikipiki huyo ni mzoefu na alishawahi kupata ajali na kukatwa kidole kimoja. Kutokana na ajali hiyo, aliacha kuwa dereva bodaboda. Hata hivyo aliamua kurejea tena na kazi hiyo takriban mwezi mmoja uliopita.

bodaboda hiyo ilikodiwa kwa shilingi 2000. Walipofika eneo la tukio, wakakuta huo moshi ukiambatana na moto mkali. Dereva bodaboda akaamua kuhama upande wake ili kujinusuru na moto na moshi huo. Inadaiwa kuwa tendo hilo lilifanyika kwa haraka ili dereva huyo alikwepe gari ambalo lilikuwa linakuja mbele yake ambalo ndiyo gari la Najma. Kutokana na hali hiyo madereva wote walikosa namna ya kunusuru ajali hiyo kutokana na eneo la ajali kuwekewa kingo za chuma ambazo zimeunganishwa na daraja la mkapa. Kwa kweli hali inasikitisha sana na abiria wa basi bado wapo hapa kituo cha polisi Ikwiriri na baadhi yao wanaendelea kutoa maelezo polisi
 
Inasikitisha sana,unakwenda kutafutia watoto riziki unarudishwa maiti!!Pumzikeni kwa amani marehemu,poleni wafiwa.
 
Dereva bodaboda ambaye ni marehemu kwa sasa alikuwa anajulikana kwa jina la Dulla
 
Basi limeruhusiwa kuendelea na safari sasa baada ya kukaa takeiban masaa mawili hapa Ikwiriri. Amechukuliwa dereva wa basimla kampuni ya SOMEA kwa vile dereva wa basi lililopata ajali anaendelea kushikiliwa na jeshi la polisi hapa Ikwiriri
 
Back
Top Bottom