Basi gani nipande kwenda Mwanza?

uliza linalokimbia upande mengine kucheleweshana tu wanaendesha utafikiri wanaenda kuzika
 
Tatizo magari ya Mwanza barabara ni ndefu hivyo gari zuri kulijua mpaka upate taarifa ya watu walosafiri recently maana magari mengi huwa yanachoka kutokana na ukweli kila siku yapo barabarani yaani likiingia usiku wa saa tano kesho yake saa kumi na mbili linasepa na ndio maana mwezi huu unakuta gari flan9i linavuma alafu baadae yanavuma mengine. Zuberi sio baya sana japokuwa sijawahi safiri nalo ila kwa uzoefu ni zuri na jamaa ana magari mengi anabadilishabadilisha magari na madereva hivyo uhakika wa safari ni mzuri
 
Mwanza ipi hiyo? Nipo mwanza jua linawaka haswaa.

jumatatu nilikuwa huko, maeneo ya sahara,miti mirefu,asubuhi naamka nakuta barabara imeloa,nilianzia Lumumba road na bado kulikuwa na tumanyunyu.
hapo vipi bado huamini
 
city boy, kisbo safaris au kidia one

Wee! Kisbo, kisesa ni full ligi barabarani
Nadha speed na mashindano ni kpi yao kutoka kwa bosi.
Ukiweza tafuta DAR LUX
Ofisi zao ziko pale kituo cha mafuta mataa ya ubungo utaona tu bango lao la bluu bluu
Safari njema mkuu
 
Habari zenu wadau...

Nina safari ya Mwanza kikazi na ndio mara yangu ya kwanza kufika kwenye mji huo...

Ni basi gani ambalo lina huduma nzuri linalofanya safari zake Kati ya Dar na Mwanza..

Shukran za dhati kwa watakaonipa majibu ya swali langu

Precision Air.
 
Panda Princess Muro au Princess Shabaha wako vizuri sana kwa huduma zao ukikoswa kabisa chukua hata Isamilo. Safari njema mkuu


UKIKOSWA....!!!!!!! mi nilijua huwa mnaishia kwenye matamshi kumbe hadi maandishi!?
 
Back
Top Bottom