Bashe anajua kucheza na akili za watu nchi hii

BLACK MOVEMENT

JF-Expert Member
Mar 11, 2020
2,712
6,517
Nilimsikia Bashe anasema mazao ya wakulima sio mali ya umma ni mali yao binafisi na faster wajinga wakaunga Mkono hoja.

Bashe hajui kwamba swala la kulisha raia ni jukumu la Serikali yoyote ile Duniani? Bashe analijua hili ila vilaza hatujui hili.

Swala la Chakula ni swala sensitive kwa Serikali zote Duniani isipo kuwa hii ya Tanzania ambayo inajua fika ina raia wa aina gani. Katila vitu ambavyo Serikali nyingi Duniani ziko makini nalo ni swala la Chakula hasa kile chakula kikuu ambacho kina liwa na mamilion ya Raia, kuna baadhi ya nchi huwa ngano ndio chakula kikuu, kwa Africa sana ni mahindi na Mchele.

Serikali nyingi zinajua fika kabisa kupanda kwa bei ya chakula kunaweza pelekea misuko suko mikubwa sana ya kisiasa na sana maandamano na hata Serikali kuangushwa na ndio maana zinaogopa sana swala la bei ya vyakula kupanda

Kwa Tanzania kwa bahati nzuri Raia hawajawahi jitambua kwa hilo ni neema kwa wakina Bashe, na Serikali inajua fika kwamba hata Chakula kikifikia kuuzwa Sh 20, 000/ kilo ya Mchele bado raia wanatanunua tu na watalalamika mchana usiku watalala.

Bashe wanakwepa jukumu kuu la kuhakikisha raia wanapata chakula cha kutosha na kwa bei ya chini kabisa, hilo hutamsikia Bashe anazungumzia hata siku moja.

KUHUSU WAKULIMA

Ukienda mfano pale Mang'ota Karatu wanalima sana vitunguu lalini wale wakulima hakuna hata mmoja anajua Mpaka wa Namanga unafananaje, na Vitunguu vinauzwa saba Kenya, Bashe aseme ni mkulima gani ana export mahindi mkulima sio wafanya Biashara/Madalali.

Bashe ashukuru kwamba Tanzania ina raia walio lala sana.

Wakenya hadi wameagiziwa Meli ya mahindi na ni kwa ajili ya binadamu na mifugo, Kenya hata Pumba ikianza kuadimika Serikali huagiza wafanya biashara walete mahindi kwa kutolipa kodi.

Wakenya Chakula kikipanda sana bei huwa Nairobi pape hapakaliki na Serikali inaogopa sana hilo wakati wowote huwa raia wanaweza lianzisha.

Bongo huku tuendelee kulala na tuendelee kumuona Bashe ni Geneous.
 
Chukua jembe kalime boss , mashamba mengi tuu unakodi 50000 ekari , mvua zinanyesha , ekari moja hukosi gunia 10 za mpunga , unakula nearly mwaka mzima .... Sasa Nani akulimie alaf akuuzie Kwa bei unayotaka Mzee .... Serikali kazi yake ni kufacilitate kilimo , eg kutoa pembejeo n.k , na kuhamasisha watu walime mana ndo ajira namba moja nchini , sasa ajira namba moja inakuwa na mawenge ya kupangiana bei kisa wajinga wachache wapo mjini kwenye sofa wanasubir uivishe alaf wakupangie bei
 
Chukua jembe kalime boss , mashamba mengi tuu unakodi 50000 ekari , mvua zinanyesha , ekari moja hukosi gunia 10 za mpunga , unakula nearly mwaka mzima .... Sasa Nani akulimie alaf akuuzie Kwa bei unayotaka Mzee ....
Maadam Bache ni machichiemu hawezi kuwa na akili
 
Serikali imechujua tahadhari za kutosha juu ya kubabiliana na njaa ndio maana alisema tunavyo vituo vya mauzo ya mahindi kwa bei ya chini, ukiona bei kubwa mtaani nenda kwenye hizo center kanunue kwa bei ya chini kasage ule la sivyo huna hoja

Unajua wengi mnafanya kilimo kama sio kazi ya maana, pembejeo(mbolea ilipanda ktk sokonla dunia) hakuna aliyemtetea mkulima leo mazao yanapanda mnaanza kelele.

Mnakuja mtandaoni kupiga mayowe muacheni Bashe afanye transformation kilimo kionekane Ni biashara vijana wavutike mipaka ifunguliwe masoko yapatikane
 
Nilimsikia Bashe anasema mazao ya wakulima sio mali ya umma ni mali yao binafisi na faster wajinga wakaunga Mkono hoja.

Bashe hajui kwamba swala la kulisha raia ni jukumu la Serikali yoyote ile Duniani? Bashe analijua hili ila vilaza hatujui hili.

Swala la Chakula ni swala sensitive kwa Serikali zote Duniani isipo kuwa hii ya Tanzania ambayo inajua fika ina raia wa aina gani. Katila vitu ambavyo Serikali nyingi Duniani ziko makini nalo ni swala la Chakula hasa kile chakula kikuu ambacho kina liwa na mamilion ya Raia, kuna baadhi ya nchi huwa ngano ndio chakula kikuu, kwa Africa sana ni mahindi na Mchele.

Serikali nyingi zinajua fika kabisa kupanda kwa bei ya chakula kunaweza pelekea misuko suko mikubwa sana ya kisiasa na sana maandamano na hata Serikali kuangushwa na ndio maana zinaogopa sana swala la bei ya vyakula kupanda

Kwa Tanzania kwa bahati nzuri Raia hawajawahi jitambua kwa hilo ni neema kwa wakina Bashe, na Serikali inajua fika kwamba hata Chakula kikifikia kuuzwa Sh 20, 000/ kilo ya Mchele bado raia wanatanunua tu na watalalamika mchana usiku watalala.

Bashe wanakwepa jukumu kuu la kuhakikisha raia wanapata chakula cha kutosha na kwa bei ya chini kabisa, hilo hutamsikia Bashe anazungumzia hata siku moja.

KUHUSU WAKULIMA

Ukienda mfano pale Mang'ota Karatu wanalima sana vitunguu lalini wale wakulima hakuna hata mmoja anajua Mpaka wa Namanga unafananaje, na Vitunguu vinauzwa saba Kenya, Bashe aseme ni mkulima gani ana export mahindi mkulima sio wafanya Biashara/Madalali.

Bashe ashukuru kwamba Tanzania ina raia walio lala sana.

Wakenya hadi wameagiziwa Meli ya mahindi na ni kwa ajili ya binadamu na mifugo, Kenya hata Pumba ikianza kuadimika Serikali huagiza wafanya biashara walete mahindi kwa kutolipa kodi.

Wakenya Chakula kikipanda sana bei huwa Nairobi pape hapakaliki na Serikali inaogopa sana hilo wakati wowote huwa raia wanaweza lianzisha.

Bongo huku tuendelee kulala na tuendelee kumuona Bashe ni Geneous.
Mmezoezwa kutofanya kazi mpewe chakula cha msaada. Acheni wakulima wale jasho lao, wewe nani kakupangia matumizi ya mshahara wako.
 
Back
Top Bottom