Barua ya wazi kwa Rais mstaafu Benjamin Mkapa.

Nyakageni

JF-Expert Member
Feb 1, 2011
15,045
5,093
Imeandikwa na Elias Mhegera

Ubabe, vitisho na kutukana siyo suluhu ya matatizo ya Watanzania!

Kwanza kwa heshima kubwa nakusalimia shikamoo, na baada ya hapo nakuomba urejee madhara yaliyowahi kusababishwa na tabia zako za ukatili na ubabe.

Kwanza hii tabia ya kutukana watu hujianza leo, nakumbuka mnamo tarehe 24 Novemba mwaka 2004 tukiwa Mwanza siku ulipozindua bara bara jijini humo ulitutukana wanahabari kwamba ni waandishi uchwara tunaoandika ujinga!

Lakini pia kulazimisha vitu ni tabia yako ya kudumu. Mwaka 2000 ulilazimisha mgombea fulani ndiye apitishwe na chama chako kugombea urais Zanzibar. Mtu huyo alikuwa kapata nafasi ya tano katika wagombea wa kura za maoni CCM. Na wala hakuwa na shahada ya chuo kikuu kwani ninyi CCM mlikubaliana mgombea wa chama chenu ni LAZIMA walau awe na shahada ya kwanza.

Wajanja tukafahamu mlimlenga Augustine Mrema kwani alikuwa na ndoto kubwa ya urais na alikuwa ni tishio kubwa kwenu ndipo na yeye akakimbilia NCCR-Mageuzi na akaruhusiwa kugombea (1995). Nakumbuka mwaka 2000 Mzee Mkapa ulisema, ?ni kweli mgombea (uliyemtaka wewe) hana shahada, isipokuwa uzoefu wake unamzidi hata huyo mwenye shahada moja? ukampitisha mtu wako.

Mwaka mmoja baadaye yakatokea mauaji ya kinyama ya zaidi ya watu 20 wafuasi wa chama cha CUF. Hatujajua nini kina kuja, na wala hatuiombei mabaya nchi yetu, bali tunakumbusha tu kwamba historia ina tabia ya kujirudia?
Kwa asili mimi ni Mzinza, natokea Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza.

Wakazi wa wilaya hiyo hususani wa Jimbo la Sengerema ambalo kwa sasa lipo mikononi mwa Mhe. William Ngeleja wanaweza kuwa wasimuliaji wazuri zaidi wa nini kiliwapata siku zile ulipokuwa ukitumia mabavu ili kulazimisha yule ?bingwa wa matunguli? ambaye pia ndiye aliamuru watu wafukiwe wakiwa hai Dk. William Shija ambaye kwa sasa naye anaitwa ?marehemu?.

Walatini wanao usemi kwamba wafu tusiwaseme kwa mabaya bali mema tu, lakini hata Biblia naamini na vitabu vingine vya kiroho ndivyo vinatutaarifu juu ya watawala na watu wengine katili kabisa waliowahi kutokea hapa duniani kama akina Goliath, Nebuchadnezzar n.k.

Nakumbuka jinsi ulivyohakikisha Dk Shija anamshinda Dk. Fortunatus Masha kwa njia za kikatili na kibabe kabisa ikiwamo kuwapiga watu, kuwakamata bila hatia, kuwahamisha na mambo mengine ya kinyama kabisa. Ukatili huo pia mlimfanyia Dk Masha mwenyewe na mwanae Lau Masha na hatimaye Mzee Masha alifungua kesi mahakamani na kushinda na akalipwa fidia ya shilingi milioni 50.

Nakumbuka uluvyotumia gharama za serikali na kuwapeleka maafisa Uslama wa Taifa wawili Sengerema kwa nyakati tofauti ili wakuletee yale yaliyokuwa yakilalamikiwa dhidi ya Dk Shija lakini bado uliendelea kumlinda.

Nakumbuka kwamba Dk Shija aliwahi kuleta malalamiko katika chama akidai kwamba mwenyekiti wa CCM wilaya kwa wakati huo Mzee George Mulanda alikuwa anambeba mgombea wa UDP, Dk Masha katika chaguzi katika misingi ya ukabila ?abazinza twimanye tulibache? yaani Wazinza tusaidiane kwa sababu tupo wachache.

Nakumbuka ulidhamiria kumsaga saga Mzee Mlanda kama ilivyo tabia yako, kwa kutumia taarifa za majungu lakini salama yake ikawa ni Mzee Philip Mangula kwani aliwahi kufanya kazi Mwanza akiwa Katibu wa CCM katika mkoa huo.

Akasema kabla ya kumuadhibu basi na yeye (Mlanda) apewe nafasi ya kujieleza na hatimaye Mzee Mlanda akayasema yote pale Dodoma wewe ukiwa mwenyekiti wa kikao.
Akasema ?nashindwa kumkampenia mbunge wangu si kwa sababu ya ukabila, bali kwa sababu hata akifika Sengerema huwa hanitafuti mimi kwanza bali huwachukua ?wasimbe? waliopo ofisini kwangu na kwenda kufanya nao ngono kwenye maguest house ya Nyamazugo road?.


Kwa neno wasimbe alimaanisha akina mama poa ambao walizoea kushinda kwenye ofisi za CCM na kukubali kutumika kwa ?mapumziko? ya wazee. Baadhi walikuwa na nyadhifa kichama na wengine walikuwapo kuwapo tu.
Mzee Mkapa nakumbuka wewe pia ulishiriki vilivyo kutumia njia za kikatili kabisa ili kuhakikisha kwamba mgombea wa CHADEMA Dk Walid Kaborou kwa wakati huo hafurukuti mbele ya Azim Premji wa CCM huko mkoani Kigoma.

Mzee umekula posho nyingi na mafao yako ya urais mstaafu tunakuomba utuachie nchi yetu katika hali ya usalama kwani wewe si baba wa taifa, bali ni rais mstaafu, usilazimishe kuvaa joho lisilo lako!

Kwa vile mmedhamiria na mnaendelea kutumia vitisho vya kidunia siye tutaendelea kwenda kiroho, na muda si mrefu mtakaa mezani na siye tena kwa kuheshimiana kabisa ?AS EQUAL PARTNERS IN THE NEGOTIATION PROCESS!?

Mwanzoni tuliambiwa wewe ni ?Bwana Msafi? tukaaminishwa hivyo na tukajua tuna mengi ya kujifunza kutoka kwako kumbe la hasha!, hakuna lolote bali ubabe na ukatili mtupu! Turejee 2Timotheo 1:7, ?wanapenda kuwa waalimu wa sheria, lakini hawaelewi maneno yao wenyewe au mambo wanayoyasisitiza?

Na hilo la ukatili tumeambiwa na Mungu mwenyewe kwamba lipo kimbilio letu wanyonge na tuyarejee maisha ya Shadrack, Misheki na Abedinago katika Biblia, kitabu cha Daniel 3:16-18 kama ifuatavyo ?16 Ndipo Shadraka, Meshaki, na Abednego, wakajibu, wakamwambia mfalme, Ee Nebukadreza, hamna haja kukujibu katika neno hili. 17 Kama ni hivyo, Mungu wetu tunayemtumikia aweza kutuokoa na tanuru ile iwakayo moto; naye atatuokoa na mkono wako, Ee mfalme.

18 Bali kama si hivyo, ujue, Ee mfalme, ya kuwa sisi hatukubali kuitumikia miungu yako, wala kuisujudia hiyo sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha.?
NINAKUTAKIA MAPUMZIKO MEMA YA UZEENI.
BUT WHERE THERE IS A WILL, THERE IS ALWAYS A WAY!
 
wanasheria nisadieni huyu jamaa awez kupelekwa ICC kwa alichokifanya zanzbar mwaka 2000 ?
 
na nyie ukawa kwa ngojera hamjambo!!!!! hamtofautiani na chura akiwa mtoni iseeeee haaaaaa!!!!!!
 
Hivi mkapa anamsikiliza kweli huyo?


dawa ni kuitoa CCM madarakani

hauwezi bila kuwa na strong and strategic opposition, sio kupagawa tu
 
SIJAONA TATIZO LA MZEE MKAPA HATA KIDOGO, Tatizo watz tumezoea maneno mengi na UNAFIKI km hao waliokuwepo, watu kama huyu mzee wa kutoa jibu straight, KAVU, La moyoni, HAMUWATAKI.

Pili Utawala sio mchezo kila mmoja na mbinu alizojaliwa nazo ili mradi tu kufikia malengo wa waliowengi
HAKIKA Utawala wake ulikuwa na mapungufu bUT NI BORA SANA KULIKO WENZIO HASA ECONOMICALLY

NI NYAKATI ZA " UWAZI NA UKWELI" BRA BRA HATUTAKI ' HUO NDIO UUMBEA
 
Zanzibar ikichafuka Lord Lofa apelekwe The Hague ICC akaungane na kina Rutto.
 
Hivi mkapa anamsikiliza kweli huyo?


dawa ni kuitoa CCM madarakani

hauwezi bila kuwa na strong and strategic opposition, sio kupagawa tu

Ni vigumu sana kuitoa CCM wakiwepo wazee kama Mkapa. Mkono wa chuma
 
Mkapa alikuja mwanza akaongoza jopo la ccm kumdhurumu wenje kura...akamtishia kumpiga kofi pale halmashauri....
 
Tangu nianze kujitambua kama binadamu, sijawahi kuhisi uwepo wa rais TZ. Naona kila mtu anafanya mambo yake tu!
 
SIJAONA TATIZO LA MZEE MKAPA HATA KIDOGO, Tatizo watz tumezoea maneno mengi na UNAFIKI km hao waliokuwepo, watu kama huyu mzee wa kutoa jibu straight, KAVU, La moyoni, HAMUWATAKI.

Pili Utawala sio mchezo kila mmoja na mbinu alizojaliwa nazo ili mradi tu kufikia malengo wa waliowengi
HAKIKA Utawala wake ulikuwa na mapungufu bUT NI BORA SANA KULIKO WENZIO HASA ECONOMICALLY

NI NYAKATI ZA " UWAZI NA UKWELI" BRA BRA HATUTAKI ' HUO NDIO UUMBEA

Kwani matusi aliyoshusha kuhusu wanaume, malofa na wapumbavu alikuwa bado madarakani?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom