Barua kwa Rais Samia Suluhu

Melki the Storyteller

JF-Expert Member
May 3, 2022
5,701
9,779
U hali gani mama? Nahisi hu buheri wa afya na unaendelea vyema na majukumu ya hapa na pale katika ujenzi wa taifa hili lililokuwa kwenye sintofahamu za kusikitisha na kustaajabisha kipindi cha nyuma

Mama yetu mpendwa, nichukue muda huu kukufikishia salamu zangu za shukurani na upendo kwa niaba ya watanzania wote na wale ambao si watanzania ndani na nje ya mipaka yetu. Natumai unausoma uzi huu huku ukitabasamu ilihali ukisubiri comments zetu za bashasha na upendo ili uzisome huku unacheka

Sina mengi zaidi ya kukutakia majukumu mema katika utendaji wako wa kazi licha ya kusongwa na vikwazo vya hapa na pale bila kusahau vijembe vya wenye chuki dhidi ya utendaji kazi wako. Mama yangu mpendwa, kazana, pigania taifa letu tusonge mbele, kamwe usiyumbishwe na mijadala yao, piga kazi mama

Sisi wana jamiiForums wote tunakupenda na kukuheshimu, pia kuheshimu kazi yako mama. Sio sisi wana jf pekee, hata wageni wetu wanakupongeza kwa utendaji kazi wako, sio tu wageni wetu, bali watanzania wote kwa ujumla na watu mbalimbali kutoka mataifa tofauti tofauti bado wanakusema kwa mazuri mama yetu. Kama ulivyo ushabiki wangu kwenye mpira wa miguu, haiwezi pita siku ya hotuba yako nikashindwa kuhudhuria hata walau kukutazama tu kwenye runinga. Mama, piga kazi

Najua sistahili hata kuzifunga kamba za viatu vyako mama, lakini ningeomba kushauri tu

Mama, barabara zinatosha. Sasa ni muda wa kukaa na kutafakari ni kwa namna gani tunakiokoa kizazi hiki cha vijana wasio na ajira ambao hawaijui hata ramani ya maisha yao ya kesho. Sio waliosoma wala sio wasiosoma, wote wanatapa tapa mama. Ma-casino yanajaa vibinti vya chuo tena tuzuri tuzuri mama. Mama, fanya juu chini ukiokoe kizazi hiki, walau watafutie connections hata huko nje ya nchi mama

Natamani hata siku nikipata muda nije nyumbani kukuona mama yangu, nina mengi ya kuzungumza kwa ajili ya taifa hili mama

Lakini yote kwa yote, utendaji kazi wako sio mbaya mama. Nikutakie tu majukumu mema, na Mola akubariki

Wana JF wote tunakupenda na kukuheshimu mama yetu mpendwa
 
IMG_20230319_194616_426.JPG
 
Back
Top Bottom