Barcelona yaishangaza PSG

bitare

Senior Member
Jul 13, 2023
197
598
Katika mechi ya Klabu bingwa Ulaya maarufu kama UEFA, iliyo chezwa leo tar 10/4/2024 Klabu ya Barcelona imeishangaza PSG Kama si Dunia Kwa ujumla.

Hii Inathibitishwa hata na wataalamu wa soka wenyewe, ambao kabla ya mchezo huo iliwapa PSG %49 ya kushinda huku Barcelona wakipewa %26.

Kikubwa nilicho jifunza nikua Team ya Barcelona licha ya kuwa na wachezaji wenye umri mdogo wengi katika kikosi, ila karibu wote ni wachezaji wenye vipaji, huku PSG Wakitegemea wachezaji kama wa tatu tu wenye majina makubwa, huku wengine wakiwa ni wachezaji wenye uwezo wakawaida.

PSG 2-3 Barcelona.
 
Mzee mbona mna over rate Sana mambo😀.
Wadogo ni wangapi humo??

Lewandowiski??
Raphinha
De jong
Cancelo
Kounde
Gundogan
Au nao Hawa ni wachezaji wadogo ehh😂🤣
Screenshot_20240411-014302_2.jpg
 
Kwahiyo Barcelona waishangazaje PSG?

Ni kama unajadili na wana baada ya kuangalia game pamoja!
 
Yani binafsi imeniuma PSG kufungwa hii mechi sijui kama huko Ugenini watafanya maajabu yoyote, si kwamba ni shabiki wa hiyo timu ila namuonea tu huruma Mbappe, naona ndoto yake ya kuisaidia timu yake ya Nyumbani kuchukua ubingwa kwa mara ya kwanza inaenda kufa na ndio basi tena
 
Aende Madrid akatiimize ndoto zake
 
PSG Hawajawahi Kuwa Serious Tena PSG Imewahi Kumiliki Wachezaji Bora Zaidi Ya Hao Na Hupoteza Hivyo Hivyo Hivyo.
 
Aende Madrid akatiimize ndoto zake
Huko Madrid anahofia hataacha historia yoyote ya maana Sababu kwanza ni timu yenye mafanikio mengi, na ndio inaongoza kwa kubeba makombe mengi ya UCL yeye alitaka abebe hilo kombe na PSG kwanza, ili aache historia kwamba hiyo timu ilibeba hilo kombe kwa mara ya kwanza ikiwa na yeye
 
Katika mechi ya Klabu bingwa Ulaya maarufu kama UEFA, iliyo chezwa leo tar 10/4/2024 Klabu ya Barcelona imeishangaza PSG Kama si Dunia Kwa ujumla.

Hii Inathibitishwa hata na wataalamu wa soka wenyewe, ambao kabla ya mchezo huo iliwapa PSG %49 ya kushinda huku Barcelona wakipewa %26.

Kikubwa nilicho jifunza nikua Team ya Barcelona licha ya kuwa na wachezaji wenye umri mdogo wengi katika kikosi, ila karibu wote ni wachezaji wenye vipaji, huku PSG Wakitegemea wachezaji kama wa tatu tu wenye majina makubwa, huku wengine wakiwa ni wachezaji wenye uwezo wakawaida.

PSG 2-3 Barcelona.
Labda we ndio ulishangazwa na hayo matokeo. Kwa yoyote anaefuatilia mpira anajua psg hawajawahi kuwa siriaz uko uefa.
 
Ndiyo! Ni MAKINDA kama CLEMENT MZIZE!
Mzize yule aliepaisha Mpira goli la wazi dhidi ya Mamelodi? Mungu akupe nini? Goli ambalo Musonda angefunga!! Mzize yule asiejua kutoa assist? Ye anachojua ni kupiga tu Mpira ujae au usijae mguuni ilimradi goli liwe mbele yake! Hajali goli liwe mbali au karibu , kushoto au kulia ye anapiga tu kama mwehu hata hageuki kuangalia wenzake walio kwenye nafasi nzuri ya kufunga!!

Mwambieni anaboa sana mashabiki kutukosesha magoli mengi, sijui ana shida Gani, huwa hana utulivu akifika kwenye penati box ni kama anakumbwa na majini na mapepo anahamanika na kupaparika kama kichaa.

Siku Mzize akiweza kuwa na utulivu na ukomavu wa akili ndani ya penati box, Yanga itakuwa ni kicheko tu daily!! Maana ameshawin jinsi ya kujiposition bado utulivu tu ambao ni zero , Mzize papara kibao kama kichaa, aangalie na kujifunza utulivu ukoje kupitia goli alilofunga juzikati Rodrygo wa Madrid dhidi ya Man City Santiago Bernabeu.

Ila goli la Mzize dhidi ya Dodoma Jiji lilikuwa fantastic!
 
Back
Top Bottom