Baraza la Mawaziri halifanyi vikao siku hizi?

Gurtu

JF-Expert Member
May 15, 2010
1,247
342
Kauli zinazotolewa na mawaziri na hasa kuhusu Dowans linaiaibisha serikali. Ngeleja ameshasema vya kwake, Sitta tumeshamsikia na hatimaye Chikawe naye amezungumza hivi karibuni. Katika suala la Dowans kumejitokeza pande mbili zinazopingana katika hoja ya kuilipa Dowans. Mh. Sitta alituambia kuwa hawajazungumza suala la kuilipa Dowans katika baraza la mawaziri.

Jk uko wapi? kwanini huitishi kikao cha baraza la mawaziri na suala la Dowans likawa moja ya ajenda za kikao? Au ndiyo kusema sasa hivi upo likizo? Mawaziri wa serikali moja wanapopingana hadharani ni aibu ya aina yake. Siku hizo kumeibuka aina mpya ya viongozi wa serikali ambao hujitetea pale wanapoona mambo yanawageuka kwa kusema "yale yalikuwa maoni yangu binafsi". Tunaomba maoni ya serikali kwani majukumu yenu kufanya hivyo.
 
Back
Top Bottom