Baraza la Maadili ya Utumishi wa Umma lashindwa kumuhoji Andrew Chenge

aye

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
2,102
708
Baraza la maadili ya utumishi wa umma limeshindwa kumuhoji Mh Endrew Chenge baada kuwasilisha zuio la mahakama kuu lililozua kutokuendelea kujadili miamala ya Escrow huku wanasheria wa sekretarieti ya baraza hilo wakipingana naye kwa madai kuwa wao wanajadili ukiukwaji wa maadili na siyo miamala ya escrow.

Chanzo: ITV

DSCN9001.jpg

Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge akijianda kutoka nje ya ukumbi wa Karimjee ausbuhi ya leo.

Maamuzi magumu kutolewa kesho Februari 26

LISAA limoja lililopita Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), Andrew Chenge amepandishwa kizimbani katika kikaango cha kukiuka maadili ya viongozi wa umma, chini ya Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Baraza la Maadili lililoketi, jijini Dar es Saalam asubuhi ya leo.

Katika shauri linalomkabili Chenge ni dhidi ya kukiuka vifungo hivyo vya sharia ya maadili ya viongozi wa umma, ambapo ilielezwa kuwa, Miongoni mwa makosa anayokabiliwa nayo ya ukiukwaji wa sharia ya maadili ya viongozi wa umma, ni pamoja na alipokuwa Mtumishi mkuu wa serikali kwa wadhifa wa mwanasheria Mkuu wa Serikali AG, alipitisha mikataba mbaalimbali dhidi ya IPTL, na baadae alipostaafu nafasi hiyo ya Mwanasheria Mkuu alikuwa miongoni mwa Washahuri wakuu wa kampuni ya V.I.P Engineer.

Ambapo ilielezwa kuwa, Chenge hakuwahi kueleza tume hiyo ya Maadili kama ana madai ama ana hisa na kampuni hiyo ya V.I.P ambayo iliingia ubia na IPTL Katika uuzwaji wa hisa hali ambayo moja kwa moja ilipelekea kukiuka vifungu vya sharia.

Hata hivyo, Chenge aliweza kujitetea ambapo aliwasilisha oda maalum ya utetezi wake dhidi ya madai anayodaiwa.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza la Maadili wa Baraza hilo anayeshughulikia mashahuri hayo Mhe Balozi Jaji (Mst.) Hamisi Msumi alisema wataenda kukaa na kupitia oda hiyo ya Chenge na kisha watatoa maamuzi siku ya Februari 26 mwaka huu yaani , (kesho) Alhamisi.

"Tunaenda kupitia vielelezo vyote na maamuzi yatatolewa Februari 26." Alisema Balozi Msumi.

Hata hivyo baada ya kuahirishwa kwa baraza hilo ambalo litaendelea tena kesho, Chenge alifuatwa na wandishi wa habari ambapo alikataa kata kata kuongea nao huku akiwaambia waende kuandika wanavyo jua wao.

"Mnataka nini. Nyie nendeni mukaandike munavyojua … nendeni mkaandike sasa. Siwezi ongea chochote" alikuwa akitamka Chenge huku akitoka kwenye ukumbi wa Karimjee yanakofanyika mashitaka ya baraza hilo la Maadili.

Baraza hilo la Maadili bado kesho litaendelea tena na shauri hilo la Chenge pamoja na viongozi wengine wa umma.
===================
Hati ya malalamiko (chini ya fungu la 22), lalamiko la kwanza la mwaka 2015 dhidi ya Andrew Chenge lilisomwa leo kwenye kikao cha Baraza la Maadili ndani ya ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
DSCN9042.jpg

DSCN9043.jpg

Chanzo:dewjiblog
 
Nchi ya kitu kidogooo,
Nchi ya watu wadogoo,
Ukitaka chai ewe baba kunywa TATEPA.

Tuhuma dhidi ya Chenge

Tangu sakata la escrow lianze, haikuwahi kuelezwa kuhusika kwa Chenge kwenye sakata hilo.

Lakini jana, akisoma hati ya malalamiko dhidi ya mbunge huyo wa Bariadi, mwanasheria wa Sekretarieti ya Maadili, Hassan Mayunga alisema mlalamikiwa, akiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) mwaka 1995, aliishauri Serikali kuingia mkataba wa miaka 20 na IPTL wa kuongeza uzalishaji wa umme.

"Mlalamikiwa baada ya kustaafu wadhifa wa AG, Desemba 24 mwaka 2005, mwaka 2006 aliingia mkataba wa kuwa mshauri mwelekezi wa kampuni ya VIP Engineering and Marketing Limited iliyokuwa inamiliki asilimia 30 ya hisa za IPTL," alisema Mayunga akikariri hati hiyo ya malalamiko.

"Kitendo cha mlalamikiwa kuingia mkataba na VIP Engineering and Marketing Limited iliyokuwa na asilimia 30 ya hisa kwenye kampuni ya IPTL ni ukiukwaji wa fungu la 6 (j) la Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ambalo linamzuia kiongozi wa umma kujinufaisha na utumishi wake uliopita kwa kutumia taarifa alizozipata alipokuwa anatekeleza majukumu yake kwa manufaa binafsi.

"Kitendo cha mlalamikiwa kuendelea kuwa mshauri mwelekezi wa kampuni ya VIP Engineering and Marketing Limited akiwa na wadhifa wa ubunge ni ukiukwaji wa fungu la 6(e) la Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ambalo linamzuia kiongozi wa umma kujiingiza katika mgongano wa maslahi."

Mwanasheria huyo aliendelea kusema kuwa mkataba ambao mlalamikiwa aliingia na kampuni ya VIP Engineering and Marketing Limited ulimpatia manufaa ya kifedha ya Sh1.617 bilioni kinyume na fungu la 12(1)(e) la Sheria ya maadili ya viongozi wa umma. Aliongeza kuwa mlalamikiwa hakutamka maslahi aliyokuwa nayo katika mkataba wa Tanesco na IPTL kinyume na fungu 14 la sheria ya Maadili.

Aliongeza kuwa mlalamikiwa hakutamka madeni yake aliyokuwa anaidai kampuni ya VIP Engineering and Marketing Limited kwa Kamishna wa Maadili kinyume na matakwa ya fungu la 9(6)(b) la sheria hiyo.

"Malalamiko dhidi ya Chenge yanawasilishwa mbele ya Baraza la maadili lenye mamlaka ya kisheria ya kufanya uchunguzi wa kina na kumtaka mlalamikiwa kutoa maelezo bayana kuhusu mwenendo wake kabla ya hatua nyingine kuchukuliwa kwa mujibu wa sheria," aliongeza.

Baada ya kusoma tuhuma hizo, Chenge alitoa amri hiyo ya zuio la Mahakama Kuu ambayo pia iliwasilishwa kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano kulizuia kujadili ripoti ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kuhusu sakata hilo la escrow, lakini ikagonga mwamba baada ya wabunge na spika kulinda muhimili wao.

"Kwa kuwa amri hii ya mahakama nilikuwa sijaipata na ninyi (wanasheria wa sekretarieti) mlikuwa mmeipata mapema ngoja nikaisome na wenzangu," alisema Jaji Msumi ambaye alikuwa akisaidiana na wajumbe wawili, Selina Wambura na Hilda Gondwe.

"Kama kweli mahakama imezuia vyombo vyote, suala hapa ni kuangalia amri hiyo. Tupeni muda tukaangalie na kesho (leo) tutatoa uamuzi kama tutaendelea au la."

Mvutano ulivyokuwa

Kabla ya kuahirisha shauri hilo ulizuka mvutano mkubwa wa kisheria kuhusu amri hiyo ya zuio la mahakama.

"Suala hili ninavyofahamu mimi liko mbele ya Mahakama Kuu, hivyo tusubiri uamuzi wa mahakama kwani amri ya mahakama ilizuia vyombo vyote vya Serikali na hiki (Baraza la Maadili) ni chombo cha serikali. Mwenyekiti, mimi nataka kupata mwongozo wa suala hili, tukiendelea bila kupata mwongozo na mimi kama mwanasheria litanisumbua sana," alisema Chenge ambaye alikuwa Mwanasheria wa Serikali kati ya mwaka 1972 na 1973.

Lakini Mayunga alisimama na kusema: "Mheshimiwa mwenyekiti, hii amri ya mahakama ambayo mlalamikaji (Chenge) ameitoa hapa, si Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma inayohusika kama mlalamikiwa alivyotaja.

"Tuhuma ambazo zimeletwa hapa ni tuhuma za uvunjifu wa maadili ya viongozi wa umma na wala siyo suala lililoonyeshwa katika hii amri... ni tofauti kabisa."

Mayunga, katika kujenga hoja, alisoma Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 Ibara 132 (1) ya inayosema kuwa "kutakuwa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ambayo itakuwa na mamlaka ya kuchunguza tabia na mwenendo wa kiongozi wa umma yeyote kwa madhumuni ya kuhakikisha kwamba masharti ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma yanazingatiwa ipasavyo".

Pia alisoma fungu la 18 (2) (c) la sheria hiyo linaloipa Sekretarieti ya Maadili mamlaka ya kuchunguza tuhuma yoyote ya kuvunjwa kwa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma na viongozi wote wa umma, wanaopaswa kuwajibika chini ya sheria hiyo.

"Kutokana na sheria hii, Sekretarieti haizuiwi kuendelea na shauri hili. Madai dhidi ya mlalamikiwa ni ya jinai na rushwa. Hapa tunajikita katika maadili wala sisi hatuzungumzii escrow, hapa ni maadili kuwa amepokea fedha kutoka VIP Engineering," alisema Mayunga

Jaji Msumi alisema hati hiyo aliipitia haraka haraka na akahoji kama ina amri inayozuia suala hilo kujadiliwa.

Chenge alijibu, "mheshimiwa mwenyekiti, hoja ambayo nimeileta mbele yako ni zuio la mahakama. Kueleza kwamba chombo hiki kiko juu ya mahakama bila..."

Kabla ya kumalizia sentensi hiyo alisimama mwanasheria wa Sekretarieti hiyo, Filotheus Manula na kusema: "Kauli anayoisema mlalamikakiwa kuwa chombo hiki kiko juu ya mahakama siyo sahihi. awali Mayunga alishaelezea. Katiba na Sheria ya Maadili na iko wazi."

Lakini Chenge akasema: "Ni vizuri vijana wakajifunza... amri hii ya mahakama siyo maoni yangu, hivyo ni vyema ikaheshimika. Itanisumbua mimi, mamlaka ya chombo hiki isitishwe siyo kwamba haina mamlaka, mnaweza kuendelea sawa, lakini hili ni ombi langu.

"Utawala wa sheria ni bora ukaheshimiwa na masuala ya siasa tuache tukapige siasa majukwaani."

Mayunga alisimama na kusema: "Mheshimiwa mwenyekiti ukiruhusu hiki anachokisema au uhalisia wa kuzuia kinachoendelea, siyo sahihi."

Chenge alijibu, "mheshimiwa mwenyekiti amri ya mahakama ni (inahusu) taarifa ya ukaguzi wa miamala ya akaunti ya Tegeta Escrow ya (Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali) CAG, na malalamiko yanayoletwa dhidi yangu ndiyo ambayo yamezuiwa... mimi ninachoomba ni ufafanuzi au mwongozo kwa hili."

Lakini Manula alipinga akisema: "Penal Code (Sheria ya Kanuni ya Adhabu) haitumiki hapa. Mlalamikiwa ndiye aliyekuwa AG, alisimamia kuitunga... madai, jinai na rushwa, lakini hapa tunajadili maadili na siyo escrow."

Chenge, aliyekuwa amesimama wakati wote, aliendelea na msimamo wake wa kuomba mwongozo, hali iliyomfanya mwanasheria mwingine wa sekretarieti hiyo, Getiruda Cyriacus kusimama na kunukuu fungu la 18 (4) la sheria hiyo linalosema sekretarieti itakuwa na mamlaka ya kuanzisha na kufanya uchunguzi wowote kuhusu ukiukwaji wa maadili yaliyotajwa katika sheria hiyo.

Vituko vya Chenge

Chenge aliingia kwenye viwanja vya Ukumbi wa Karimjee saa 3:02 asubuhi akiwa katika gari aina ya Toyota Land Cruizer akiongea na simu na aliposhuka, aliwaambia waandishi wa habari waliokuwa wakimpiga picha akisema: "Nendeni mkauze magazeti na sura ya Chenge."

Alipotaka kuingia ukumbini, aliambiwa asubiri kwenye viti, lakini aligoma na badala yake alishuka chini na kuanza kuzungumza na simu huku akizungukazunguka takribani dakika 10 kabla ya kutakiwa kuingia ukumbini saa 3:13 asubuhi.

Mara baada ya Jaji Hamis kuahirisha baraza hilo saa 3:55, waandishi walianza tena kumpiga picha na kama kawaida alisema: "Nendeni mkaandike mnavyoona... mnataka na mgongo muupige picha?"

Waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari walipotaka kufanya naye mahojiano ya suala hilo alijibu, "siwezi kuzungumzia chochote kuhusu yaliyopo katika maadili" na kupanda gari, kisha akaondoka.

Chanzo: Mwananchi
 
Baraza la maadili ya utumishi wa umma limeshindwa kumuhoji Mh Endrew Chenge baada kuwasilisha zuio la mahakama kuu lililozua kutokuendelea kujadili miamala ya Escrow huku wanasheria wa sekretarieti ya baraza hilo wakipingana naye kwa madai kuwa wao wanajadili ukiukwaji wa maadili na siyo miamala ya escrow.Source ITV

Sidhani kama watamweza huyu nyoka mwenye makengeza msaka pesa kama alivyojitabainisha. Nyoka ni ishara ya shetani yabidi kufanya kazi ya ziada ya maombi na kufunga ili kuweza kumshinda.
 
Kwa kweli inasikitisha kusikia mambo yanavyoendeshwa hivi nchini kwetu.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mwandaaji wa katiba pendekezwa, kwa nini asijiwekee vifungu vya kulinda ufisadi!!!!!
 
Tanzania ni zaidi ya uijuayo,huu mchezo anaucheza huyu nyoka mwenye makengeza,I hope magogoni wanajua wazi!
Zingekua nchi zenye kufuata sheria sasa hv angekua segerea!
Kuna siku tulikutana na Mwigulu Nchemba,Kunduchi Mtongoni kuna baa flani inaitwa Galawa!
Joko lenye makengeza lilimpigia simu Mwigulu,likamwambia aache kabisa kulizungumuzia suala lake la kuchota mpunga wa escrow,na akamwambia hakuna kodi kwenye hizo pesa,mpaka sasa hv Mwigulu kakaa kimya
 
Huyo naye ni kati ya wahusika wakuu wa bunge maalumu la katiba, ndio maana waliondoa kipengele cha maadili ya viongozi na wananchi kuwa na uwezo kuwawajibisha viongozi. Naenda kupiga kura ya HAPANA kwenye katika iliyopendekezwa.
 
Anajua kucheza nayo na watu kama hawa haitakiwi kumpeleka kuhojiana ni kumchukulia uamuzi tu sababu atakushinda Ana trick nyingi
 
Sidhani kama watamweza huyu nyoka mwenye makengeza msaka pesa kama alivyojitabainisha. Nyoka ni ishara ya shetani yabidi kufanya kazi ya ziada ya maombi na kufunga ili kuweza kumshinda.
Kweli kabisa mkuu,ikumbukwe ni huyu huyu alinaswa na kamera za bunge akirusha vitu kwenye
ukumbi wa bunge usiku wa manane kipindi hicho mr six alikuwa bado ni spika.M
aadamu amejiita nyoka yeye mwenyewe, inaonekana kuna maombi yanafanya kazi
hivyo wanamaombi waendelee lazima atatoka pangoni,na ndo hapo atakutana na mafuta ya taa.
 
Tume haijadili miamala ya Escrow bali inajadili uadilifu wake kutokana na kupokea fedha hizo:

Hoja hapa ni kuwa Chenge akiwa katika utumishi wa umma amepewa fedha hizo kama:
  1. Zawadi kwa urafiki wake na Ruge?
  2. Malipo ya kazi aliyomfanyia huyo Ruge?
  3. Amemuuzia mali Ruge?
  4. nk
Katika hili zuio la mahakama halijakiukwa!!!
 
Huyu bwana kawasilisha zuio la mahakama kuu la kuzuia asihojiwe na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi...Radio One.

Sasa tumfanye nini?
 
SAKATA LA ESCROW: Tume ya Maadili yahairisha kusikiliza suala la A. Chenge kujipatia Sh1.6bn za escrow baada ya mbunge huyo kuwasilisha zuio la korti leo, Dar. Chezea sheria ww?
 
Back
Top Bottom