Baraka: Hebu Anzia hapa kwa leo. . .

Kongosho

JF-Expert Member
Mar 21, 2011
35,999
24,175
Leo tuanze kwa baraka kidogo.

Zab ya 19:
12. Ni ani awezaye kuyatambua makosa yake? Unitakase na mambo ya siri

13. Umzuie mtumishi wako asitende mambo ya kiburi, Yasinitawale mimi
Ndipo nitakapokuwa kamili, Nami nitakuwa safi, sina kosa lililo kubwa.

14. Maneno ya kinywa changu, Na mawazo ya moyo wangu, Yakapate kibali mbele zako,
Ee BWANA, Mwamba wangu na mwokozi wangu.

Endelea kidogo hadi Zab ya 20.

1. Bwana akujibu siku ya dhiki, Jina la Mungu wa Yakobo likuinue

2. Akupelekee msaada toka patakatifu pake, Na kukutegemeza toka Sayuni.

3. Azikumbuke sadaka zako zote, Na kuzitakabali dhabihu zako.

4. Akujalie kwa kadiri ya haja ya moyo wako, Na kuyatimiza mashauri yako yote.

5. Na tuushangilie wokovu wako, Kwa jina la Mungu wetu, tuzitweke bendera zetu.
Bwana akutimizie matakwa yako yote.

6. Sasa najua kuwa Bwana amwokoa masihi wake, Atamjibu toka mbingu zake takatifu.
Kwa matendo makuu ya wokovu, Ya mkono wake wa kuume.

Amina, na mbarikiwe sana.
 
Moyo wangu wamtukuza bwana ,na roho yangu inashangilia katika mungu mkombozi wangu
kwa maana tokea sasa vizazi vyote vitaniita mwenye heri

ubarikiwe kongosho
 
Ameni kwa sana Konnie...naamini hii itakua ni ijumaa ya baraka...na jioni tukutane kwa ajili ya SHUHUDA!
 
Kama kuiba acha nifanye kupitia njia zingine, si biblia jamani.

Nimepitia haya maneno asubuhi nikayaona yana maana sana
Nikaona bora kushare na wapendwa wengine.

au unataka kufungua ministry?
 
kama kuiba acha nifanye kupitia njia zingine, si biblia jamani.

Nimepitia haya maneno asubuhi nikayaona yana maana sana
nikaona bora kushare na wapendwa wengine.
kwani kufungua ministry ni kwamba wataka kuiba ?
 
Sio lazima uwe unaiba
Lakini dhamira yako na msukumo wa kwanini unafungua ministry ndo utakuhukumu.

Unajua unaweza fanya mambo makubwa kwenye jamii kw kuwa na ministry
Lakini kwangu sitakuwa na amani kama kilichonivutia kwa mara ya kwanza ilikuwa ni msukumo wa kupata pesa

Sikumbuki ni wapi lakini imeandikwa, injili itahubiriwa hata kwa HILA ili kila sikio likapate kusikia habari za wokovu.

Je nihubiri kwa HILA? Sina hakika kama nataka kuwa hapa.

aya my k nimekusoma ubarikiwe sana.hope leo umefunga kutuombea sisi wakosefu
 
Umenikumbusha Sunday School

Mafungu ya kukariri.

Haleluya, enyi mataifa yote msifuni BWANA
Enyi watu wote muhimidini
Kwa maana fadhili zake ni kuu
Na uaminifi wa BWANA ni wa milele.

Nani anajua hii zaburi ni ya ngapi?
 
Ubarikiwe sana Kongosho,

Kumcha Bwana ndio mwanzo wa hekima,
Wote wafanyao hayo wana akili njema,
Sifa zake zakaa milele.

Zaburi 111:10
Nawatatakia Ijumaa njema!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom