Foundation
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 1,421
- 596
Siku za karibuni nimekuwa nikipita barabara inayounganisha barabara ya Kawawa na bararabara ya Shekilango maarufu kama barabara ya Tandale. Hii barabara imeanza kuharibika kwa kasi sana,ina mashimo mengi,Ikinyesha mvua maji yanajaa barabarani hadi kwenye majumba.
Inakoelekea bararbara hii itakuwa kama ilie ya shekilango ilivyokuwa kero kwa watumiaji wa barabara miaka ya nyuma, kwa juhudi za Lowasa ile barabara ikatengenezwa ( Simpigii debe ila ndio ukweli ) na hadi sasa ni nzuri ingawa huwa inaelemewa na msngamano wa magari.
Najiuliza na majibu sipati, je Mamlaka husika hawajaona huo uharibifu au wanasubiri iharibike kabisa. Mamlaka husika iwe Manispaa ya Kinondoni au TANROAD wafanye utaratibu wa kuifanyia matengenezo ili kuepusha usumbufu wa watumiaji na upotevu wa pesa ya kufanyia ujenzi mpya hapo baadae.
Ukitoa hiyo kero, nashauri serikali ipanue barabara za shekilango na Tandale ili ziweze kumudu ongezeko la watumiaji wa barabara. Kuna msongamano wa Magari huwa unatokea mara kwa mara. Pia itasaidia kupunguza msongamano kwenye bararbara za Kawawa na Morogoro.
Nawasilisha
9