Elisha Ray
JF-Expert Member
- Mar 19, 2012
- 323
- 94
Wadau, mimi ninasikitika sana na mambo ya ulipuaji katika idara za hii serikali. Hii barabara ya Akachube (inayoanzia kijitonyama off Kajenge road, kuelekea upande wa Mwananyamala) imekwishaanza kuharibika hata kabla ya mwaka kuisha toka ijengwe!! sasa hivi lami yake ina mabonde mabonde na mashimo tayari yameshaanza kutokea. Sijui ni nani wanahusika na mambo ya quality katika idara hizi zinazohusika na barabara au hawaoni/wameuchuna? Barabara ina kiwango cha hali ya chini na kodi zetu ndo zishapotea pale.. Hata barabara ya Sam Nujoma walojenga wachina imeshaaza kuwa na mabonde!!!! Wahusika hawaoni haya mambo? au ndo wamechukua cha juu???