Barabara na miti kipi muhimu?

Kiby

JF-Expert Member
Nov 16, 2009
6,899
4,623
Binafsi mimi ni mtu ambae ninapenda sana manzari nzuri hasa pale inapopambwa na uoto wa asili au miti ya kupandwa pamoja na maua. Dar ilbadilika ghafla na kuwa jiji linalovutia katika barabara zake kwa sababu ya miti na bustani.

Leo hii katika barabara za jiji mh Magofuli ameanzisha kampeni inayoenda kasi ya kukwangua miti yote kando ya barabara ili ati kupanua barabara. Mimi sikubaliani naye kwa sababu siamini kama hizo barabara ni muhimu zaidi ya hiyo miti.

Wa jf tusaidiane ni nini kilsababisha hii miti kuoteshwa mahala ambapo imekuwa ni kwa mda mfupi na ilishindikana je kuoteshwa umbali ambao hata kama barabara zitapanuliwa mara mbili hazitaigusa?

Nimepita morogoro road leo na kwa jinsi miti ilivyokuwa inapukutishwa nimeshindwa kujizuia kuililia, tena nimelia kilio cha kwikwi.
.
 
nilipita jana pia na nilisikitika sana na kukumbuka jinsi KONOIKE walivyoijenga hii barabara miaka ya 90 na kuweka service roads ambazo zimepandwa miti kwa njia ambayo nilidhani ingekuwa mfano na funzo kwa watanzania katika ku-respond to the pollution inayotokana na magari.

Nilivyoona jinsi miti ilivyokatwa ndio nikajua kuwa tuna matatizo zaidi ya 100 na yote yapo mlangoni. Kwa hiyo badala ya TANROADS/STRABAG kuanza kukata hii iliyopo, ingelifanyika feasibility mpya ya master plans ya mji (pamoja na miji mingine nchi nzima) ili maeneleo yanayofanyika yaweze angalau ku-last kwa miaka 50.

Maana hapa ninachoona miti ni bora zaidi lakini unakuta watu wamejenga barabarani na inakuwa vigumu kuvunja hizo nyumba lakini miti wanakata tu kwa vile haina mtetezi!
 
Basically mimi siku zote Huwa nawashangaa Tanroads!! Nadhan Kuna Maengineer Majina Tu!! Hata wewe mleta mada nadhan Una Kibanda / Nyumba yako mahali fulani Hapa Dar!! Siku zote unashauriwa Miti ni Hatari sana Kwa foundation ya nyumba yako!! Na watu wengi Hukata Hii miti pindi inapokuwa karibu na Nyumba zao!! Kweli wanasema lisemwalo Lipo!! Ndivyo Hivyo ilivyo pia kwa barabara!! Miti ni Hatari sana kwa foundation za barabara na Nyumba!! Angalia barabara kutoka Ubungo hadi Magomeni!! Miti imeharibu Kabisa foundation ya Hii barabara!! Mizizi yake ni adui Mkubwa!! Hivyo nilikuwa nawashauri hawa Maengineer waamke na kuzuia Huu Upandaji wa miji Usiozingatia Mpamgilio na Madhara Yatokanayo!! Angalia Ubungo kwenda Kimara - Uharibifu wa service road sio Mkubwa kama Ubungo kwenda Magomeni!
Vile vile Miti Huzuia Visibility ya watumiaji wa barabara Hasa Kwenye Kutoka au Kuingia!! Miti ni Muhimu ila sio kwenye Highways!! Kwani ndio Maana Kuna avenue streets ambazo ndio huwa zimepambwa na miti pembeni na sio kila barabara ni avenue!! Tusiwe Tunaiga kwa Kudandia Train kwa Mbele!
 
Back
Top Bottom