Bandeko Nangai Ya Kabila

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,526
1,529
Wakati sisi tunafanya ziara za dunia kutafuta umaarufu na win win situation, huku tukiuza mashirika na viwanda kila kukicha, kijana wa Baba Josefu anaanza vitu vyake!

Miezi kadhaa nilianzisha thread kuhusu Congo kuanza kufanya mapinduzi ya maendeleo taratibu, lakini watu wakaona kuwa hilo halitoshi.

Sasa najiuliza ni lini Mwankupuli ataamka na kuanzisha mapinduzi mapya ya maendeleo kwa Taifa letu?

Congo wametuwashia indiketa kwa muda sasa karibu watatupita, Rwanda nao washatuacha kama lile Scania la Riziki kwa Mungu, Msumbiji wala tusifikirie kuwagusa huku Zambia na Malawi wakipetesha ngano na kuona kuwa Namibia ni bora kwao kimaendeleo kuliko Tanzania.

Hivi tunakwenda wapi jamani? mbona tunaendelea kuzubaa?

Kabila wants DRC to become "China of Africa"‏MARY GWERA
Daily News; Friday,October 17, 2008 @21:00
TWO ships containing 702 tonnes of construction equipment from China and Belgium are expected to be offloaded at the Dar es Salaam port, and then be transported by road to the Democratic Republic of Congo (DRC).

An official from the DRC President’s office, Mr Kazimil Kamba Wakambala told the 'Daily News' in Dar es Salaam on Thursday that the equipment includes tractors, tippers, and some agricultural equipment.

Mr Wakambala said that they had expected that they would receive the goods on Wednesday, but it was not possible due to ship congestion at the port. He said that the idea of ordering such equipment was put forth by DRC President Joseph Kabila who wants to revolutionise the country by improving agriculture and infrastructures.

“The president wants to reconstruct DRC to be like China, he wants the country to be identified as China of Africa,” Mr Wakambala explained.

He added that the equipment were mainly focused on the reconstruction of roads and improvement of agriculture in provinces of Katanga, Kasai, Eastern Manyema, Eastern Kivu, Western Kivu and Kisangani.

A 10-people delegation sent by President Kabila to Dar es Salaam to receive the consignment include five officials from the president’s office, one from Congo Road agency identified as (Office’ de Route),one from Congo Revenue Authority (OFIDA) and three journalists.

Mr Wakambala said there would be a short ceremony of receiving the equipment to be held at the port, the function which will also be attended by the DRC Ambassador to Tanzania, Mr Juma Alfani Mpango.
 
Rev. Kishoka,
Mkuu unampiga mbuzi gitaa!..nani anataka kulima ikiwa kila kitu imported ndio mali?...
Utachukua muda mrefu sana kuwafahamisha viongozi wetu ambao wakienda Mlimani city wanaona maendeleo ya Ulaya yakija Tanzania..
Tunakula kama Ulaya vile..
 
Rev. Kishoka,
Mkuu unampiga mbuzi gitaa!..nani anataka kulima ikiwa kila kitu imported ndio mali?...
Utachukua muda mrefu sana kuwafahamisha viongozi wetu ambao wakienda Mlimani city wanaona maendeleo ya Ulaya yakija Tanzania..
Tunakula kama Ulaya vile..

Mkandara,

Hilo swala la kila kitu imported linaleta swali, tunapata wapi pesa za ku-import vitu?
 
Mkandara,

Hilo swala la kila kitu imported linaleta swali, tunapata wapi pesa za ku-import vitu?
Rev.
Unataka jibu kwa swali lako? Jaribu ufisadi. Hivi yule mama aliyenunua (kujitwalia) nyumba 12 kule Mbeya alipata wapi fedha za mtaji?
 
Wakati Bi. Salma alipokuja kutibiwa Unyamwezini, nilikuwa na maongezi na mkulu mmoja, nikamuliza inakuwaje kuwa Tanzania inaacha kuwa wabunifu na kutumia fedha kwa ajili ya faida za muda mrefu na kuishia kununua kila kitu ikiwa ni pamoja na vitu ambavyo tungeingia gharama kuvijenga na kuviendeleza, Tanzania ingeweza kujijenga na kujitosheleza kwa vizazi vijavyo?

Chukulia mfano, badala ya kujenga hospitali za kutosha na kununua vifaa vya kisasa na kugharamia vyma masomo ya Watanzania kuwa madakitari bingwa, sisi tunaona huko ni kuingia gharama sana na suluhisho ni kupeleka watu India, Afrika Kusini, Marekani na hata Uingereza.

Sasa likija gonjwa baya kushambulia watu elfu kumi, tutawagharamia wote kwenda Ulaya kutibiwa?

Njoo kwenye Chakula, haieleweki kuwa Tanzania inaona ni bora kuagiza chakula badala ya kubadilisha mfumo wa kilimo na kuwa na uwezo wa kujitosheleza kwa chakula iwe ni nafaka, matunda, mboga hata mifugo na uvuvi.

Kwa nini tukimbile kuagiza chakula kutoka Malaysia kila siku huku Shinyanga, Rukwa, Rufiji, Mbarali, Kyela na hata Pemba zinaweza kutuzalishia mpunga wa kutosha? Mahindi na maharage wala usiseme! Ukija mafuta ya kupikia kule Singida mializeti na ufuta unaharibika lakini tuko tayari kuagiza Korie na mafuta mengine kutoka nje ya nchi!

Sasa ni ujinga na ujuha kama tunashindwa kuhamasisha uzalishaji mali ndani ya nchi kukidhi mahitaji na kukimbilia kuagiza.

Hivyo vijisent vya kuuza mashirika au mapatu finyu ya madini yana mwisho wake, tukishauza viwanda na dhahabu kukauka serikali itapata wapi fedha? au sasa tutakuwa tegemezi wa misaada kwa 100%?

Vitu vingine havileti maana hata kidogo!
 
Katika kipindi kilicho baki cha miaka 2 kwa Mh. Rais tusitegemee mapinduzi ya kiuchumi kutokea. Sasa hivi Rais atakuwa busy kufanya propaganda na ku-deal na watu wachache ambao anaona ni threat kwake kuwania tena uras 2010.

Ameshapoteza mwelekeo, hivyo kataika kipindi cha miaka 2 ijayo maisha yatazidi kuwa magumu sana. Kumbuka ni katika kipindi ambacho pia wanataka kukusanya fedha kwa ajili ya uchaguzi.
 
Jasusi na Mkandara,

Kuna hii sehemu iliyoko ndani ya Azimio la Arusha ambalo inazungumzia mambo ya fedha.

Ni muhimu kuirudia na kujipima kama kweli tunakwenda kuliko kwema au ndio tunazidi kukongoroka!


Fedha kutoka nje ya Tanzania, Je?

Njia moja tunayotumia kujaribu kuepukana na lazima hii ya kukiri kodi zaidi ikiwa twataka fedha zaidi ni kutilia sana mkazo fedha za kutoka nje ya Tanzania. Fedha hizi za kutoka nje ni za aina tatu:-
(a) Zawadi: Yaani Serikali ya nje iipe Serikali yetu fedha za bure tu kama sadaka kwa ajili ya mpango fulani wa maendeleo. Wakati mwingine shirika lo lote la nje liipe Serikali yetu au Shirika jingine katika nchi yetu msaada fulani kwa ajili ya maendeleo.
(b) Mkopo: Sehemu kubwa ya fedha tunazotazamia kupata
kutoka nchi za kigeni si zawadi au sadaka, bali ni mkopo.
Serikali ya nje au Shirika la nje, kama vile Benki, hukopesha
Serikali yetu fedha fulani kwa ajili ya kazi zetu za
maendeleo. Mkopo huu huwa una masharti yake ya kulipa,
kama vile muda wa kulipa, na kima cha faida.
(c) Raslimali ya Kibiashara: Aina ya tatu ambayo pia ni kubwa
kuliko ya kwanza, ni ile ya fedha za watu au makampuni
yanayotaka kuja katika nchi yetu kuanzisha shughuli mbali
mbali za uchumi kwa manufaa yao wenyewe. Na sharti
kubwa walitakalo jamaa hawa wenye fedha zao ni kwamba
shughuli yenyewe iwe ni ya faida – kwao – na pia kwamba
Serikali iwaruhusu kuondoa faida hiyo Tanzania na kuipeleka
kwao. Hupenda pia kwa jumla Serikali iwe na siasa
wanayokubaliana nayo au ambayo haihatarishi uchumi wao.

Hizo ndizo njia tatu kubwa za kupata fedha kutoka nje ya
nchi yetu. Kuna mazungumzo mengi ajabu juu ya jambo hili
la kupata fedha kutoka nchi za kigeni. Serikali yetu na
viongozi wetu wa makundi mbalimbali hawaachi kufikiria njia
za kupata fedha kutoka nje. Na tukizipata au japo tukipata
ahadi tu ya kuzipata mara magazeti yetu, au radio zetu na
viongozi wetu hutangaza jambo hilo ili kila mtu ajue kuwa
neema imekuja au iko njiani inakuja.

Tukipata msaada hutangaza; tukipata mkopo hutangaza; tukipata kiwanda kipya hutangaza; tukiahidiwa msaada, mkopo au kiwanda kipya hutangaza. Japo tukianza mazungumzo tu na nchi au shirika la kigeni juu ya msaada, mkopo au kiwanda, mara hutangaza japo hatuna hakika ya matokeo ya mazungumzo hayo. Na kisa? Ni kuwajulisha wananchi kwamba, tunaanza mazungumzo ya neema!

TUSITEGEMEE FEDHA KULETA MAENDELEO

Ni jambo la kijinga kuchagua fedha kuwa ndiyo chombo chetu
kikubwa cha maendeleo na hali tunajua kuwa nchi yetu ni maskini.
Ni ujinga vile vile, kwa kweli ni ujinga zaidi, tukidhani kuwa tunaweza kuondoa hali hii ya unyonge wetu kwa kutegemea fedha za kutoka nje badala ya fedha zetu wenyewe. Ni ujinga kwa sababu mbili.

Kwanza, hatuwezi kuzipata. Ni kweli kwamba zipo nchi ambazo
zaweza na zapenda kutusaidia. Lakini hakuna nchi moja duniani ambayo iko tayari kutupa misaada au mikopo au kuja kujenga viwanda katika nchi yetu kutimiza shabaha zake zote za maendeleo.

Nchi zenye dhiki ni nyingi sana duniani. Na hata kama nchi zote zenye neema zingekubali kuzisaidia nchi zenye dhiki, bado ingekuwa msaada huo hautoshi. Lakini nchi zenye neema hazitakubali. Hata katika nchi ile ile, matajiri huwa hawatoi fedha zao kwa hiari ili zisaidie Serikali kuondoa dhiki.
Njia ya kuzipata fedha za matajiri ili zisaidie umma ni kuwatoza
kodi wakipenda wasipende. Hata hivyo huwa hazitoshi. Ndiyo
maana japo tungewakamua vipi wananchi na wakazi wa Tanzania, matajiri na maskini, hatuwezi kupata fedha za kutosha kutimiza mipango yetu ya maendeleo.

Wala duniani hakuna Serikali ambayo yaweza kuyatoza kodi mataifa yenye neema, yakipenda yasipende, ili kusaidia mataifa yenye dhiki. Hata hizo zisingelitosha. Hakuna Serikali ya Dunia nzima. Fedha ambazo nchi zenye neema hutoa huwa kwa wema wao, au hiari yao au kwa manufaa yao wenyewe.
Haiwezekani basi, tupate fedha za ktuosha kwa njia hiyo.

MISAADA NA MIKOPO VITAHATARISHA UHURU WETU

Pili, japo kama tungeweza kuzipata; hivyo ndivyo tunavyotaka
kweli? Kujitawala ni kujitegemea. Kujitawala kwa kweli
hakuwezekani ikiwa Taifa moja linategemea misaada na mikopo ya Taifa jingine kwa maendeleo yake. Hata kama pangetokea Taifa au mataifa ambayo yako tayari kutupa fedha zote tunazohitaji kuendesha mipango yetu ya maendeleo isingekuwa sawa kwa nchi yetu kuipokea misaada hiyo bila kujiuliza matokeo yake yatakuwa nini kwa Uhuru wetu na uzima wetu.

Msaada ambao ni kama chombo cha kuongeza juhudi, au
nyenzo ya juhudi, ni msaada ambao una manufaa. Lakini msaada unaoweza ukawa sumu ya juhudi si msaada wa kupokea bila kujiuliza maswali.

Kadhalika mikopo. Kweli mkopo ni bora kuliko misaada ya
“bure”. Mkopo nia yake ni kuongeza jitihada au kuifanya jitihada itoe matunda mengi zaidi. Sharti moja la mkopo huwa ni kuonyesha jinsi utavyoweza kuulipa. Maana yake ni kwamba sharti uonyeshe kuwa unakusudia kuufanyia kazi itakayoleta manufaa ya kukuwezesha kuulipa.

Lakini hata mikopo ina kikomo. Sharti upime uwezo wa kulipa.
Tunapokopa fedha kutoka nje mlipaji ni Mtanzania. Na kama
tulivyokwisha sema Watanzania ni watu maskini. Kuwabebesha watu maskini mikopo ambayo inawazidi kimo si kuwasaidia bali ni kuwaumiza. Na hasa inapokuwa, mikopo hiyo ambayo wanatakiwa walipe haikuwafaidia wao, bali ilifaidia watu wachache tu.

Na Viwanda vya wenye raslimali zao je? Ni kweli tunavitaka.
Hata tumepitisha katika Bunge sheria ya kulinda raslimali ya wageni wanaoanzisha mipango mbali mbali ya uchumi katika nchi yetu. Nia yetu na matumaini yetu ni kuwafanya waone kuwa Tanzania ni nchi inayofaa kuingiza raslimali zao. Kwani raslimali yao itakuwa salama italeta faida. Na faida hiyo wenyewe wataweza kuiondoa bila vipangimizi. Tunayo matumaini ya kupata fedha za maendeleo mbali mbali kwa njia hii. Lakini hatuwezi kupata za kutosha. Lakini hata kama tungeweza kuwaridhika kabisa Wageni hao na Makampuni
hayo mpaka yakubali kuanzisha mipango yote ya uchumi tunayohitaji katika nchi yetu, hivyo ndivyo tunavyotaka kweli?
Kama tungeweza kushawishi wenye raslimai wa kutosha kutoka Amerika, na Ulaya kuja kwetu na kuanzisha Viwanda vyote, na mipango mingine yote ya uchumi tunayohitaji katika nchi hii, hivi kweli tungekubali bila kujiuliza maswali? Tungekubali kweli kuacha uchumi wetu wote uwe mikononi mwa wageni kwa ajili ya kupata faida na kuipeleka katika nchi zao?
Hata kama wasingedai kuhamisha faida na kupeleka makwao, bali faida yote watakayopata wataitumia hapa hapa Tanzania kwa maendeleo zaidi. Hivi kweli tungekubali jambo hili bila kujiuliza hasara zake kwa Taifa letu?
Huu Ujamaa tunaosema kuwa ndiyo shabaha yetu tungeujengaje? Twawezaje kutegemea nchi za nje na Kampuni za nje kwa misaada na mikopo na raslimali kwa maendeleo yetu bila kuhatarisha uhuru wetu?

Waingereza wana methali isimayo “Amlipaye mwimbaji
ndiye huchagua wimbo”. Tutawezaje kutegemea nchi za kigeni na Makampuni ya kigeni kwa sehemu kubwa ya maendeleo yetu bila kuzipa nchi hizo na makampuni hayo sehemu kubwa ya uhuru wetu wa kutenda tupendavyo. Ukweli wenyewe ni kwamba hatuwezi.

Tukariri basi. Tumefanya makosa kuchagua fedha, kitu
ambacho hatuna, kiwe ndicho chombo kikubwa cha mipango yetu yamaendeleo. Tunafanya makosa kudhani kuwa tutapata fedha kutoka nchi za kigeni. Kwanza, kwa sababu kwa kweli hatuwezi kupata fedha za kutosha kwa maendeleo yetu. Na pili, hata kama tungeweza, huko kutegemea wengine kungehatarisha uhuru wetu na siasa nyingine za nchi yetu.
 
Sasa sisi tunafanya nini na Mwankupuli wetu?

Rev:

Amani iwe kwako pia. Nadhani kuna makosa makubwa tuliyofanya. Ukiangalia bajeti ya Tanzania mfuko wa hazina unachukua sehemu kubwa. Kwanini mfuko huu unachukua sehemu kubwa ni kwa sababu miaka Ujamaa ulipopamba moto serikali ilipanuka sana, nafasi nyingi za kazi zilianzishwa ambazo zinatumia sehemu kubwa ya pato la nchi.

Rwanda na DRC nazo zilipanua serikali zao. Lakini vita vya wenyewe kwa wenyewe vilisababisha muundo mzima wa serikali kubadilika. Na kuna uwezekano mkubwa sana kuwa serikali ya Kabila ina watumishi wachache kuliko serikali ya Mobutu.

Tanzania hivyo vitu vinawezekana lakini tupo tayari kubadili mfumo mzima wa serikali hili uwe wa wafanyakazi wachache na wenye kuleta ufanisi.

Uwezi kufungua shule za sekondari kwa kila kata na baadaye ununue matrekta wakati kwa ajili ya kuendeleza kilimo. Muhimu wa shule za sekondari hupo lakini gharama za kuendesha shule hizo ni kubwa na inachukua muda mrefu kuleta matokeo.

Kwa maoni yangu tatizo letu, tulichemsha toka tumepata uhuru kuelewa ni vitu gani vya kuanza. Elimu, Kilimo, Siasa, Afya na mambo mengine ni muhimu sana kwa maisha ya binadamu. Lakini kama resource zako ni ndogo ni lazima uchague.

Tujiulize ni kitu gani tulitakiwa kukiweka mbele. Juzi naongea familia yangua Tanzania wanasema katika heka 5 za mahindi wamepata gunia 20. Hii inaonyesha kuwa hata kwa standard ya Afrika, watanzania bado ni wakulima primitive.
 
Inawezekana vipi nchi kama Rwanda na Congo kuweza kujenga jamii ya kisasa baada ya vita vya wenyewe kwa kwenyewe? Nchi kadhaa ambazo zimewahi kuwa na machafuko ya wenyewe kwa wenyewe ndizo ambazo kwa kiasi kikubwa zinajitahidi sana kujenga jamii bora; Marekani, Indonesia, Rwanda, Angola n.k je kuna somo ambalo tunatakiwa kujifunza?
 
Wakati sisi tunafanya ziara za dunia kutafuta umaarufu na win win situation, huku tukiuza mashirika na viwanda kila kukicha, kijana wa Baba Josefu anaanza vitu vyake!

Miezi kadhaa nilianzisha thread kuhusu Congo kuanza kufanya mapinduzi ya maendeleo taratibu, lakini watu wakaona kuwa hilo halitoshi.

Sasa najiuliza ni lini Mwankupuli ataamka na kuanzisha mapinduzi mapya ya maendeleo kwa Taifa letu?

Congo wametuwashia indiketa kwa muda sasa karibu watatupita, Rwanda nao washatuacha kama lile Scania la Riziki kwa Mungu, Msumbiji wala tusifikirie kuwagusa huku Zambia na Malawi wakipetesha ngano na kuona kuwa Namibia ni bora kwao kimaendeleo kuliko Tanzania.

Hivi tunakwenda wapi jamani? mbona tunaendelea kuzubaa?

Apewe muda zaid ataonesha kali zake bado wakati ano wakufanya mengi kwani hata kipindi kimoja haja maliza tusubiri mwishowe mwakipindi cha pili tutaona mzao yake naimani nae ataleta mapinduzi ya kimaendeleo na ulimwengu utashangaa
 
Apewe muda zaid ataonesha kali zake bado wakati ano wakufanya mengi kwani hata kipindi kimoja haja maliza tusubiri mwishowe mwakipindi cha pili tutaona mzao yake naimani nae ataleta mapinduzi ya kimaendeleo na ulimwengu utashangaa

Hapa unamzungumzia Kabila au Mwungwana?
 
Inawezekana vipi nchi kama Rwanda na Congo kuweza kujenga jamii ya kisasa baada ya vita vya wenyewe kwa kwenyewe? Nchi kadhaa ambazo zimewahi kuwa na machafuko ya wenyewe kwa wenyewe ndizo ambazo kwa kiasi kikubwa zinajitahidi sana kujenga jamii bora; Marekani, Indonesia, Rwanda, Angola n.k je kuna somo ambalo tunatakiwa kujifunza?

Hili swali linaogopesha, halafu sidhani kama kuna mtu anapenda twende huko. Ila watu wakishachoka ndio hivyo tenaa wanaweza kuanza hayo mambo. nadhani umeona watu walimwanzishia Chief mwankupili Mbeya. Tuombe Mungu.
 
Inawezekana vipi nchi kama Rwanda na Congo kuweza kujenga jamii ya kisasa baada ya vita vya wenyewe kwa kwenyewe? Nchi kadhaa ambazo zimewahi kuwa na machafuko ya wenyewe kwa wenyewe ndizo ambazo kwa kiasi kikubwa zinajitahidi sana kujenga jamii bora; Marekani, Indonesia, Rwanda, Angola n.k je kuna somo ambalo tunatakiwa kujifunza?

Hata mageuzi ya uchumi na civilization ulaya yalianza baada ya vita ya pili ya dunia. antibiotics pia ziligunduliwa baada ya vita ya pili ya dunia.Vita zinafanya watu wakumbuke kuwa maisha sio tu "tambarare" kama wanavyosema bongo, hivyo basi watu huanza kutafuta utatuzi wa matatizo mbalimbali. Hata hivyo, no one in their right mind would consider to start wars just that they can get to think better!!!
 
Kwa nini basi nasi tusiepuke vita na kuwa kama Botswana lakini tunataka tushikane mashati kwanza patashika bin kuchanika ndipo tuamke na kuanza kuijali nchi yetu?

Wenzetu wanatupita kwa kasi ya ajabu. Nitawaambieni hili na kuwa muwazi, kwa mwaka mmoja akiwa Raisi, Kikwete anatumia takribani si chini ya Dola Millioni saba ($7,000,000.00) kuzunguka dunia kwa safari ambazo hazina matunda ya maana. Hizo pesa japo zaonekana ni kidogo, zidisha mara tatu halafu jiulize, zingejenga hospitali ngapi au shule ngapi? au kulipia wanafunzi wangapi? au kuongeza mishahara ya watumishi wa Serikali wangapi?

Udhaifu wa Kikwete na Serikali yake si ajabu umezidisha uchochezi wa uhujumu kutoka kwa Wananchi wa Tanzania kwa kuona hamna maana ya kuchacharuka na kujituma, hivyo tunasubiri damu imwagike.

Majaribio tumeyaona Mwanjelwa na Chunya, yalianza mawe....
 
Kwa nini basi nasi tusiepuke vita na kuwa kama Botswana lakini tunataka tushikane mashati kwanza patashika bin kuchanika ndipo tuamke na kuanza kuijali nchi yetu?

Wenzetu wanatupita kwa kasi ya ajabu. Nitawaambieni hili na kuwa muwazi, kwa mwaka mmoja akiwa Raisi, Kikwete anatumia takribani si chini ya Dola Millioni saba ($7,000,000.00) kuzunguka dunia kwa safari ambazo hazina matunda ya maana. Hizo pesa japo zaonekana ni kidogo, zidisha mara tatu halafu jiulize, zingejenga hospitali ngapi au shule ngapi? au kulipia wanafunzi wangapi? au kuongeza mishahara ya watumishi wa Serikali wangapi?

Udhaifu wa Kikwete na Serikali yake si ajabu umezidisha uchochezi wa uhujumu kutoka kwa Wananchi wa Tanzania kwa kuona hamna maana ya kuchacharuka na kujituma, hivyo tunasubiri damu imwagike.

Majaribio tumeyaona Mwanjelwa na Chunya, yalianza mawe....

Rev,

Hiyo kwenye red ni very sad but true, wakati mwingine inaumiza sana moyo kuujua ukweli. Inaumiza kiasi cha kutamani usingejua chochote kile ambacho viongozi wa nchi yako wanafanya.

Kwa mambo kama haya, giza linazidi kutawala ujao (future) wangu zaidi sana sasa kuliko miaka mitatu iliyopita.
 
Back
Top Bottom