Balali alishakufa hatukuambiwa?

Simple

Familia kama wanajua hajafa si wamese? Au Balali mwenyewe si ajitokeze, hata kama yuko kwenye mapango ya torabora? Vinginevyo kimya chote wakati akijua kuwa hana kosa, sisi tutaendlea kuamini tunayoyasikia sasa kuwa tayari hatunaye tena.

Kwani si ameisha sikia kuwa hakuna mwenye shida naye?
 
Hivi hamjui kuwa ni bora lawama kuliko fedhea, Balali arudi kuja kufedheesha wakuu, hili haliwezekani hata kidogo, serikali inajua alipo na inawezekana bado mpaka leo analipwa malipo furani na serikali kwa ajiri ya kulinda masirahi ya wakubwa. Hivi mnafikiri mkuu wa polisi aliposema nchi imekamatwa na magaidi alikosea, serikali iliyopo madarakani si ya kikwete bali kikwete ana serikali kivuri inayojulikana kwa watu lakini ukweli ni kwamba kuna serikali nyingine ambayo ndo yenye maamuzi kwenye mambo yote ya nchi na kikwete anatekeleza tu.

Kwa JK ni bora watanzania tumlaumu kuwa kashindwa kumrudisha balali kuliko balali kurudi nchi hii na kuja kuwafedheesha serikali ya pili ambayo ndo iko active kuliko serikali kivuri ya JK. kwenye hili hakuna cha balali wala nini watanzania lazima tukubali kuwa balali hawezi kurudi kwa ajiri ya masirahi ya wakubwa na wala hawezi kusema chochote huko aliko.

Situation kama hizi tulikuwa tunazisoma kwenye noval lakini naona zinakuwa reality kwa tanzania na zinaanza kuchukua maisha ya kawaida ya mtanzania.
 
Mkuu MKJJ,

Yaani hapo umechokonoa penyewe kabisa...bado kuongezea kachumvi na pilipili tu pakianza kuwasha watasema wenyewe...wametugeuza kama vinyamkera wao kuwa mtu wao haalafu hawajui aliko....Lazima watakuwa hamnazo kabisa si bure..
 
Mkuu MKJJ,

Yaani hapo umechokonoa penyewe kabisa...bado kuongezea kachumvi na pilipili tu pakianza kuwasha watasema wenyewe...wametugeuza kama vinyamkera wao kuwa mtu wao haalafu hawajui aliko....Lazima watakuwa hamnazo kabisa si bure..

huo ni upupu mzee jk akilogwa akakaa kwenye ile kiti basi hizo kelele mimi sina lakuongeza
 
Balali lina kula kuku wake Argentina,hajafa wala nini,mmelala sana wabongo.

Mkuu hakuna cha kula kuku kutoka ugavana mpaka kuanza kukimbia kimbia dunia nzima ndo kula kuku? au hiyo ni laana kutoka kwa watanzania.


Anaye kula kuku ni yule ambaye anaweza kutembea kifua mbele bila kumwogopa binadamu mwenzake.
 
Mkandara, ni katika kufuatilia habari ambazo zimekuwa zikiminywa kwa muda mrefu; katika kujiuliza uliza ndiko nimehitimisha kuwa Balali alishakufa, kwani ushahidi wa kimazingira unaonesha kuwa haiwezekani akawa hai; tatizo ni kuupata mwili.
Kwa uhakika kwa kutumia mantinki ya kikawaida tu, akili haikubali kwamba kwa mtu ambaye SERIKALI inamtuhumu kwa hujuma kubwa na nzito kama hizo, eti mpaka sasa wanapata hata nguvu za kutuambia hawajui alipo. Akili hata ile ya kawaida haikubaliani na ukweli kama huu. Nadhani labda kwa kujiuliza kwako huko mwanakijiji, inawezekana akili ikatengeneza mantiki kidogo. Lakini tuna jadi ya marehemu..bila ya kujali alikufa katika hali gani..kumuenzi kitaifa..labda tungeona taifa likienzi mazishi au msiba wa mtu huyu. Inatatiza kichwa!!
 
Mi nakwambia Balali na yeye lazima yuko hapa kwenye hii thread!

My take: Balali ni mzima na nafikiri serikali inaweza ikawa imepoteza sight tu ya mahali alipo!
Inawezekana jamaa amefanikiwa kuwatoka kiaina na sasa hawajui alipo!
Sasa hizi rumrours...Balali hatathubutu kuwasiliana na ndugu zake hovyo hovyo kwasababu unaweza kuta hao ndugu zake nao wako chini ya uangalizi kuona kama kutakuwa na any communications btn the family members especially kutoka kwa Balali! ie simu etc
Kwa upande mwingine hii pia inaweza kuwa ni propaganda ya serikali!
Lakini wamekosea...we will make sure him together with the rest faces justice!
 
Kakindomaster,umelala sana,kwani balali alikuwa anaishi Tanzania kabla ya kuwa gavana?Amka kaka,Balali hakuwa loyal kwa nchi yetu,yeye alikuwa ni mtu wa matawi ya juu na leo yupo Argentina ana kula kuku wake,akae Bongo vumbi tupu na Malaria?babali hamuogopi mtu wala nini,kaamua tu kwenda kula maisha huko,mbona hujiulizi,pesa zina rudi na woooooooooooooooooote waliohusika hawaja kamatwa?Why Balali akamatwe?Balali anaweza akarudi anytime na isiwe chochote wala lolote.Amka weweeeeeeeeeeeeeeee
 
Hivi kwa hatua aliyokuwa amefikia balali kwa kutosikika mpaka sasa, na jinsi alivyokuwa kuwa anapenda kutoa ushirikiano na waandishi wa habari mbali mbali na kwa maswala yaliyotokea tangia alipo ugua kweli mtu akisema sasa amekufa mimi sioni cha ajabu hata kidogo.

Huyu bwana anajua kujieleza sana ni either alipokuwa anaumwa ndo basi ilitoka au kuna kikubwa kilicho msibu zaidi ya tunayoyaona. Nafikiri Balali atakuwa na Mtandao, kwa hizi post karibia 70 ambazo bado zinatafuta zinamtafuta huku na huko kama kweli ni mzima angalau arushe tu neno BBC au chombo chochote cha habari vinginevyo tukubaliane kuwa ndo yamekwisha.
 
Balali hawezi kukamatwa!
Serikali haitathubutu kufanya hivyo kwani kitakachofuata ni serikali nzima kujiuzulu! Hilo wako aware off...Na sisi pia tuko very aware that kumhoji Balali ni sawa na kitendo cha serikali kusimamia na ku prepare its own political execution and/or demise!
 
Hivi kwa hatua aliyokuwa amefikia balali kwa kutosikika mpaka sasa, na jinsi alivyokuwa kuwa anapenda kutoa ushirikiano na waandishi wa habari mbali mbali na kwa maswala yaliyotokea tangia alipo ugua kweli mtu akisema sasa amekufa mimi sioni cha ajabu hata kidogo.

Huyu bwana anajua kujieleza sana ni either alipokuwa anaumwa ndo basi ilitoka au kuna kikubwa kilicho msibu zaidi ya tunayoyaona. Nafikiri Balali atakuwa na Mtandao, kwa hizi post karibia 70 ambazo bado zinatafuta zinamtafuta huku na huko kama kweli ni mzima angalau arushe tu neno BBC au chombo chochote cha habari vinginevyo tukubaliane kuwa ndo yamekwisha.
Balali hana haja ya kufanya hivyo,why?wake yeye anajipumzisha na mijipesa yake?Why aanze malumbano ya mimi na wewe?
 
Balali has an ace in his hand, and it is the power of disclosure! Sasa ameamua kukaa kimya and that is his main power. Amepotea na kabla hajapotea aliwaambia waheshimiwa " Don't look for me" and they comply, not for any other reason then the fact that they don't want problems. Kama vipi, si ungeona watoto, ndugu na jamaa zake wanabanwa na serikali? but they are all well na wanaendelea na shughuli zao. That is the pact, na ndiyo maana Balali hawezi kuongea au hata kuonyesha sura. Hajafa wala nini lakini anafurahi sana kuona uzushi kama huu maana anajua watu watamsahau na kumzika rohoni, hivi after 5 years he will walk down Samora avenue and nobody will pay attention, watafikiri tu "Duh amefanana na marehemu ex-gavana Balali!".
Lakini Mwkjj usije ukasikia kesho watu wanasema labda wewe ndo ex-gavana, maana uzushi umezidi!
 

Mafisadi wa serikali ya awamu ya 3 na ya 4 wamefungamana na kuungana kama nervous system ya mwanadamu. Ni vigumu sana kuwatofautisha. Wana JF tunatakiwa kuelewa kwamba serikali ya JK haina uwezo wowote wa kusimamia matatizo ya uhujumu uchumi ambayo yamelikumba taifa letu kwa kipindi cha Mkapa na sasa JK aliyekuja kukiendeleza. JK alisema mara kadhaa kwamba hana jipya analolileta kwa watanzania. Isipokuwa atayaendeleza ya Mkapa kwa nguvu mpya, ari mpya na kasi mpya. Aliyasema hayo akijua fika kilichoendelea kwenye serikali ya Mkapa yeye akiwa sehemu muhimu kwa miaka 10.

Mafisadi watashitakiwa na serikali tofauti kabisa down the road. Ndio maana ni muhimu sana wana JF kuliangalia swala la muelekeo wa taifa letu kwa jicho la huruma na la tafakari ya wapi itakuwa turning point nyingine. Tuache kujifurahisha kwamba kuna mtu yeyote sasa anaweza kuwashitaki hawa watu hata kama wako hai.

Balali ni sehemu muhimu sana (nasisitiza tena: sehemu muhimu sana) ya himaya ya Mkapa. Awali Mkapa alitaka kupinga JK kuchukua ticket ya CCM ili awape mafedhuli wa karibu zaidi. Akaonywa kwamba ataingia mkenge na athari yake ingekuwa kubwa sana kwa CCM. Akaamua kuingia deal na JK (kidogo afanye kama Putin).
Wakakubaliana na wakamchotea vijisenti pale BoT akahonga na kujiwekea network safi.
JK kaingia madarakani akasema Mkapa asiguswe ng'o. Usipomgusa Mkapa hutamgusa Balali wala Yona wala Mramba (Baba Mwenza) wala Kigoda wala mwinyi wala Mgonja and the list goes on and on and on....
Usanii huu wa muda usikieni tu. Hakuna cha Pinda wala Luhanjo wala Mwansheria mkuu wa serikali. Hawana uwezo kufukua uozo wa mafisadi hao.As far as Mkapa is concerned anatafakari tu uwezekano wa kuyeyusha kesi ya Mhalu (sehemu nyingine muhimu ya himaya yake) na kutuliza hizo kelele za Kiwira na Epa. Mwisho wa mchezo.

Kama kweli Balali angekuwa mwovu kama tulivyoonyeshwa na serikali, juzi tumeambiwa kwamba bado anahodhi nyumba ya Gavana wa BoT aliyokuwa akitumia fedha nyingi sana za BoT kuikarabati kila wakati alipojisikia. Prof. Ndulu alidiriki kuuambia umma wa watanzania kwamba kuna taratibu zake za kumtoa kwenye nyumba ya serikali as if sheria za ajira na kustaafu, kuacha au kuachishwa kazi na kufukuzwa kazi watanzania wengine hatuzijui. As if sheria za ajira ya serikali na mashirika ya umma ni siri kama fedha za epa. Kumbukeni ni serikali hii hii ambayo inawalipa wafanyakazi hewa mamillion ya fedha za walala hoi. Serikali hii inasemekana kuwa inamlipa Balali mafao yake yote na kumlipa pension kila mwezi mpaka kifo kiwatenganishe. Baadhi yenu mnamwita huyo Balali Dr. Sijui hata aliupata wapi huo udaktari wake.

Lakini ukweli mmoja ni bayana kwamba iko siku historia itawahukumu watu hawa. Tunahitaji tu kizazi kipya kupenyeza. Na dalili ni nzuri. Kizazi kipya kinajiandaa vizuru. Siku zao zinahesabika. Kwa wakati huu uhuru wao ni mkubwa sana na wanaweza kufanya mbwembwe zote. Waache wakodi ndege, wapokelewe na misafara ya magari mikubwa kama ile ya mazishi ya baba wa taifa, lakini siku zao zinahesabika na si nyingi sana.

Naomba kuwakilisha
 
Hivi kweli hatuwezi kuongea na serikali ya marekani hapa sisi kama wadau wa Taifa la Tanzania?

Tunajua kuwa si ombi kwa marekani kutupa Balali!

Ni makubaliano na kwasababu serikali imeshasema haimuhitaji then who cares about these rumours eti kafa?
Propaganda TUU!! Tunamtaka BALALI DEAD OR ALIVE!
Na tunataka Wamarekani watukabidhi sisi wananchi na si kusema eti serikali haimuhitaji!

Serikali itamuhitaji vipi shahidi wa ku iangamiza kama hawa wamarekani na wao hawatuletei za kuleta?
 
Halafu haya mambo ya kusema mtu kafa hapa marekani sio siri mtu akifa kwa hiyo hii habari haijaelezea upande huo!
Hakuna siri hapa marekani inapokuja kwenye kuoa pamoja na vifo!

Sasa Mkjj rumours za kifo?
 
Balali hana haja ya kufanya hivyo,why?wake yeye anajipumzisha na mijipesa yake?Why aanze malumbano ya mimi na wewe?

Inajulikana kuwa Balali alikuwa mtalii tanzania hii inaeleweka Mkuu. Hila kuwa mtalii haimpi ruhusa ya kushirikiana na majambazi kuibia nchi anayoitalii.

Halafu Mkuu argentina isikutishe siyo mbali mkuu, kwa mfano ni rahisi kutoka bongo kwenda argentina kuliko kwenda ktk baadhi ya wilaya Tanzania.
 
Hivi mumemuelewa Mkjj? Someni katikati ya mistari yake mtaona anachomaanisha ni nini
 
Back
Top Bottom