Bajeti ya wizara ya maji kujibu hoja binafsi ya Mh. Mnyika?

assadsyria3

JF-Expert Member
Apr 9, 2013
6,904
4,050
Waziri wa maji anawasilisha bajeti yake huku kukiwa kuna kilio cha shida ya maji katika jiji la Dar es salaam. Je itaweza kujibi hoja nzito ya mh. Mnyika?

let us see.
 
Hivi Rais alikutana na wabunge wa Dar? tukisema MUONGO tutakosea?
 
Tatizo la maji kwenye jimbo la Ubungo limekuwa sugu. 2015 Mh. Mnyikaa ajiwajibishe akikataa wananchi watamuwajibisha kwenye masanduku ya kura.
 
Tatizo la maji kwenye jimbo la Ubungo limekuwa sugu. 2015 Mh. Mnyikaa ajiwajibishe akikataa wananchi watamuwajibisha kwenye masanduku ya kura.

Unapoandika uwe makini inaonekana wewe uko nje ya nchi labda, kwa faida yako kama Mhe. Mnyika aliwasilisha hoja binafsi kuhusu tatizo la maji Ubungo/dar ikatupwa afanye nini by the way si kazi ya Mbunge kuleta maji kazi yake ni kuisimamia serikali ili itatue tatizo hilo na kama hawataki awachape viboko! Ni uendawazimu ukisema kuwa Mnyika ataondolewa Ubungo, kamuulize Hawa Ng'humbi anajua jinsi kijana alivyo makini kimsingi ni moja ya hazina za Taifa vijana kama Mnyika. Iwapo itampendeza Mungu atatoka lakini sio kwa mpango wa Magamba!
 
Tatizo la maji kwenye jimbo la Ubungo limekuwa sugu. 2015 Mh. Mnyikaa ajiwajibishe akikataa wananchi watamuwajibisha kwenye masanduku ya kura.

Lazima utakuwa una mtindio wa ubongo hata kama ni kulipwa huwezi kuwa mjinga kiasi hiki, nani alikuambia kuwa jukumu la mbunge ni kutoa huduma za kijamii, mnyika anakusanya kodi wapi?
 
Ndugu wanajamvi,

Nikiwa ni mtanzania mwenye hamasa ya kujua mambo ya nchi hii nimejaribu kufuatilia hoja ya Bajeti ya Wizara ya Maji (leo trh 29/04/2013) ambapo waziri wa fedha kaanza kwa kuelezea kuwa serikali imetathmini umuhimu wa sekta ya maji na kuona kuwa maoni na ushauri wa wabunge katika bajeti ya awali yalikuwa na manufaa na yalistahili kufanyiwa kazi. Katika maelezo yake kaelezea kuwa serikali imeamua kuongeza fedha katika bajeti ya wizara ya maji kwa KUCHUKUA FEDHA kutoka sehemu mbalimbali za mafungu yake ya bajeti kwenye maeneo ya POSHO ambazo hata zikichukuliwa hazitaathiri utendaji wa SERIKALI.

Swali langu kwa wataalam wa uchumi, fedha na bajeti ambao ni imani yangu humu jamvini wamo, unapoondoa fedha iliyoandaliwa na wahusika katika hatua za uandaaji wa bajeti ya idara na taasisi mbalimbali za wizara na taasisi husika, na kuifanyia marekebisho ndani ya bunge kisha ukasema haitaathiri utendaji wa serikali hapa unamaanisha nini? Je, katika bajeti ya serikali kuna fedha huwa zinaandaliwa katika bajeti lakini hazina umuhimu wa kuwepo? na je, kama zinakuwa hazina umuhimu kwa kiasi kikubwa, huwa zinaandaliwa ili zifanye nini? Endapo fedha zilizoondolewa zimegusa eneo la POSHO ambalo limekuwa linapigiwa kelele, je, kuna umuhimu wa kuondoa POSHO zote maana hazioneshi kuathiri utendaji wa serikali?

Nawasilisha.
 
Inastupa wasiswasi sana juu ya mwenendo wa kuchukua ama wao wanavyoita kuokoteza sehemu mbalimbali za bajeti ili kujazilishia kwenye ufinyu mkubwa...kule wanakookoteza hawaweki ufinyu tena? Hili ndo naona tatizo na kwa serikali yetu na watendaji wetu wanaopenda POSHO zaidi ya MISHAHARA yao sijui kama tutafika mkuu Elinewinga
 
Kwa hiyo serikali imeamua kushughulikia tatizo sugu la maji kwa wananchi wake, ikitumia chenji za posho?!!! Posho hizo hizo ambazo wanaozipata mara nyingi huzitumia kunywea pombe, kuchoma nyama, na kununulia mala.ya, humo ndiko kunatafutwa vijichenji kwenda kuwapa walipa kodi maji?!!! Kweli????
 
Kwahiyo baada ya kusakura sakura chenji huko kwenye posho, serikali imefanikiwa kupata sh ngapi na zitatosha kuwapa maji wananchi wangapi?
 
Inawezekana vipi wizara muhimu kama hii ikawa haina strategic plan wala framework for transport services?

haijulikani pesa zao zinatumikaje na kwenye nini na kila mwaka wanaomba pesa.

Mtandao wao is even more embarassing kuliko Michuzi blog so dont expect to get anything meaning from the website.

wito. Nashauri mwakwembe and his gang close down the website kisha wajipange upya.
 
Back
Top Bottom