Mwiba
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 7,607
- 1,744
Mwanafunzi aliwa na simba
2008-09-01 09:13:16
Na Futuna Selemani, Mkuranga
Mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya Msingi, Mwanzega katika Kata ya Mbezi, Tarafa ya Shungumbweni wilayani Mkuranga, Ali Athmani Mbotoni (10), amefariki dunia baada ya kuliwa na simba.
Akizungumza na Nipashe jana, Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Bw. Henry Orauya Clemens, alisema mwanafunzi huyo alikumbwa na mkasa huo, wiki iliyopita saa 12.00 jioni nyumbani kwao katika kijiji cha Mwanzega.
Bw. Clemens alisema alipewa taarifa hiyo na wazee wa kijiji hicho, mara bada ya kutokea kwa tukio hilo.
Alisema mtoto huyo alikumbwa na mkasa huo wakati akirejea nyumbani kwao kutoka dukani kununua vitu alivyotumwa na wazazi wake.
Mkuu huyo wa wilaya alisema aliwaagiza askari wa wanyama pori, ambao walikwenda eneo la tukio lakini giza lilikuwa limeshaingia hivyo walilazimika kusubiri hadi kesho yake ili kufanya msako katika pori lililopo kijijini hapo.
Alisema kuwa askari hao waliendesha msako na walifanikiwa kumuua simba huyo jike anayesadikiwa kuwa alikuwa na watoto wawili, ambao walikimbia.
Alisema fuvu la kichwa la mtoto huyo lilikutwa kichakani na mwili wake ukiwa umeliwa wote na mnyama huyo mkali.
``Juhudi za kuwasaka watoto hao wa simba zinaendelea,`` alisema Clemens na kutoa wito kwa wakazi wa wilaya hiyo kutoa taarifa mapema pindi wanapoona wanyama wakali kwenye maeneo yao.
SOURCE: Nipashe
Tumsaidieni waziri wa mali asili na Utalii ,hii ni aibu hadi leo bado kuna watu wanaliwa na wanyama pori tena ,kama huyu ni katoto kadogo ambako kalienda dukani kununua pipi.