Kutakuwa na kitabu kinachoelezea manabii kama super man, wonder woman, the flash, hulk, captain america, iron man, huku taifa la USA litatajwa kama Taifa teule, na uhakika kizazi kijacho kitaaminishwa haya mambo, huku movies za hollywood zikiwa kama refference ya watu kuamini hayo mapokeo na sehem zao ibada itakuwa kumbi za starehe za viwanja vya maonesho ya sinema kama theaters.Tunaogopa tu miaka ya 2500 huko wasije wakaandika kitabu kuwa kulikuwa na nabii akiitwa Spider man alikuwa anaruka kwenye maghorofa.
Nimejifunza muda mrefu sana kuhusu madhehebu ya kikristo lakini Kila dhehebu linakuwa kivyake na lijiongoza kivyake ukiuliza unaambiwa imeandikwa inanipa ugumu sana kuielewa hiki kitabu Cha biblia Ina maana hakuna mwongozo mmoja Kwa dini zote!Labda nina ufinyu wa fikra au ujinga wangu umefunika. Lakini mjinga kugundua na kukubali ujinga wake si ni hatua ya mwanzo ya kuacha ujinga na kuerevuka?
Nasema hivi kwa sababu sielewi, hivi, mtu anaposema Ukristo au Uislamu huwa anamaanisha nini? Je, kama Wapentekoste ni Wakristo, Wakatoliki nao ni Wakristo?
Mfano ; Wakatoliki wanaamini ubatizo wa mtoto mdogo na Kristo ndiye anawaongoza kufanya hivyo wakati Wapentekoste wanaamini ubatizo ni kwa mtu wazima tu tena kwa kuzamishwa ndani ya maji mengi kama alivyobatizwa Yesu (mwasisi wa Ukristo) katika mto Jordan.
Sasa inawezekana ukatoliki ni upentekoste vikawa ni Ukristo kweli?
Je, wale Wa-Adventista Wasabato wanaoamini kuwa siku takatifu ya ibada ni Jumamosi tu ni Wakristo sawa na Walutheri wanaoabudu siku ya Jumapili?
Je, Mashahidi wa Yehova wasioamini utatu mtakatifu kuwa ni Mungu Baba, Mungu Mwana na Roho Mtakatifu ni sawa na wanaoamini utatu mtakatifu kama mafundisho ya kweli ya Biblia?
Kama wote ni Wakristo, kwa nini wengine waamini kuwa Yesu ni mwana wa Mungu na wengine wadai Yesu ni Mungu? Kwa nini wengine waamini Yesu alitumwa duniani kuwaokoa wanadamu na wengine waamini alijituma binafsi kumwokoa mwanadamu aliyepotea?
Inawezekana vipi mitizamo hii miwili inayokinzana yote kuwa ya Kikristo ilhali wote wakitumia msaafu wa Biblia?
Yapo madhehebu yanayoruhusu wanawake kuwa wachungaji, wainjilisti, wahubiri: yapo mengine yanayokataza, yapo madhehebu yanayoruhusu ndoa za jinsia moja lakini wote wanapunga mapepo kwa jina la Yesu Kristo, Je, huyo Kristo hana falsafa moja inayoongoza dini yake?
Kama ndio hivyo,neno “Ukristo” linaweza kuwa na maana moja huku wafuasi wake wakitofautiana kiteolojia, kifalsafa, matendo, tambiko na tafsiri ya maandiko?
Leo kila kona ya nchi yetu hasa maeneo yenye mwamko wa kiuchumi kumeoteshwa madhehebu lukuki kila moja ikiwa na staili yake ya kuwahadaa wafuasi wake kwa jina la Yesu Kristo.
Kwa sababu pombe ndo imeandikwa hizo burger au chips sijawahi kuona kama zimekatazwa au kukubaliwa. AhsanteeNimeshuhudia vyakula vikiwapa watu ulemavu wa kudumu kama KISUKARI, PRESURE, SHINIKIZO LA MOYO, KIRUBA TUMBO, FIGO n.k
Mavyakula kama Bugger, pizza, mavyakula ya sukari sana, UNYWAJIBWA MASODA, MAJUICE YA SUKARI yamewapa watu matatizo makubwa na wengi wamepoteza maisha, tunaona saiv kijana miaka 30 ana tumbo kama kifutu, akiumwa utasikia ana presha, kisukari, sio pombe bali mavyakula.
We umeona pombe tu,
Je, unaelewa Yesu kwanini alikufa?Sawa
"Fanya chochote" ukiwa unamanisha hata kuua,kuzini kufanya lolote kisa huchangaia kitu katika wokuvu!?Je, unaelewa Yesu kwanini alikufa?
Agano 1 - TORATI
Agano 2 - Neema na Kweli
Leo hii Tupo agano la 2, soma zaidi kuhúsu Kristo Yesu.
Hauzuiliwi na chochote, kuwa huru kufanya chochote.
Kwani umeokolewa bure kabisa, huna ulicho changia na hauwezi kuchangia wokovu. Wewe amini aliye kuokoa.
Jibu swali kwanza, unaelewa Yesu kwanini alikufa?"Fanya chochote" ukiwa unamanisha hata kuua,kuzini kufanya lolote kisa huchangaia kitu katika wokuvu!?
Inamaana Agano la kale hamlitaki Tena? Ndo nazidi kutokuelewana zaidi Kwa maana hata Amri kumi.zipo agano la kale manake tuachane nazo?
Alikufa Kwa ajiri ya dhambi zetuJibu swali kwanza, unaelewa Yesu kwanini alikufa?
Umeokolewa nini? Umeokolewa wapi? Kwanini uokolewe na nani alikuingiza huko mpaka uje uokolewe? Ninani aliesababisha wewe kuhitaji kuokolewa? Au yesu yupo kama wamarekani anakugonga kwanza vita anahakikisha njaa inawashika vyema then analeta misaaada anatangaza kuwa nimewaokoa, kwahyo yesu alituletea shetan duniani jamaa akatupaka madhambi weeee then yesu akashuka akampiga,sijui katupa silaha then kasema katuokoa, huyu yesu nimsanii sanii pia kama ni hivyo, kama utapinga hoja yangu utatuambia sasa, kwann atuokoe amekuokoa na nn amekuokolea wapi na kwann?Je, unaelewa Yesu kwanini alikufa?
Agano 1 - TORATI
Agano 2 - Neema na Kweli
Leo hii Tupo agano la 2, soma zaidi kuhúsu Kristo Yesu.
Hauzuiliwi na chochote, kuwa huru kufanya chochote.
Kwani umeokolewa bure kabisa, huna ulicho changia na hauwezi kuchangia wokovu. Wewe amini aliye kuokoa.
Je sasa waamini kuwa huna dhambi kwa sababu Yesu alikufa?Alikufa Kwa ajiri ya dhambi zetu
Je wewe ni mtu wa mataifa(yani tofauti na taifa la Mungu) au wewe ni mmoja wa kabila 12 za Israel...Umeokolewa nini?
Uliokolewa kwa sababu Mungu alikupenda hakutaka uangamie yani Ufe bali aliamua akupe uzima wa milele.Kwanini uokolewe na nani alikuingiza huko mpaka uje uokolewe? Ninani aliesababisha wewe kuhitaji kuokolewa?
Bila shaka nimejibu.kwann atuokoe amekuokoa na nn amekuokolea wapi na kwann?