Babu wa Loliondo sasa yuko hatarini...

Mediaman,

Mungu ni mmoja. Unataka amtaje Yesu ili iweje? Yeye amesema ameoteshwa na Mungu. Mungu alimuumba mwanadamu kwa mfano wake. Kutokana na kutenda dhambi Mungu alimtuma mwokozi Yesu ili aje kuwaepusha wanadamu na dhambi. Naam, vivyo hivyo Mungu alipoona binaadamu wanateswa na magonjwa na kwa kuwa Yesu alikufa na kufufuka na kupaa mbinguni na kuwa atakuja tena siku ya hukumu kuwahukumu wazima na wafu... akamtokea Ambilikile Mwasapile kule Samunge na kumpa maono ni jinsi gani anaweza kuwaponya wanadamu na magonjwa sugu yanayowasumbua.

Kwa hivyo basi, Yesu kazi yake kubwa ilikuwa ni kuwaokoa wanadamu dhidi ya dhambi. Ambilikile Mwasapile kazi yake ni kuwaponya wanadamu dhidi ya magonjwa yanayowasumbua. Kwanini basi usiamini kuwa kila mmoja ana kazi yake aliyotumwa na Mungu?

Ukuweza kwenda kwa Ambilikile Mwasapile ukapona maradhi yako na ukamfuata Yesu ukaacha dhambi zako utauona ufalme wa mbinguni siku Yesu atakapokuja kutoa hukumu.

Kumtibu mtu kwa kutumia jina la Yesu kwangu naona sio sahihi. Kwa kuwa Yesu kazi yake ni kukuondolea dhambi na magonjwa sio dhambi...

Elewa hivyo katika jina la Mungu.

Si vizuri kupotosha maneno ya Mungu. Soma injili utaona Yesu alisema nini kuhusu dhambi, alipomwambia yule mgonjwa 'Nenda umesamehewa dhambi zako' Waliokuwepo wakakwazika akawauliza mnashangaa nini? Je hamjui kuwa mwana wa Adamu aweza kusamehe dhambi? Je ni kipi rahisi kusema umesamehwewa dhambi zako au enenda umepona? Hapo alikuwa anamaanisha nini? Go back to Genesis; kabla ya anguko la mwandamu hakukuwa na ugonjwa wala kifo kwani roho ya Mungu ilikuwa ndani ya mwanadamu. Alipokosa utii dhambi (roho ya Ibilisi) iliingia ndani yake na roho ya Mungu ikaondoka na ndipo magonjwa adha na shida yakwa ndiyo matunda ya kazi ya roho ya Ibilisi ndani yake. Bila dhambi hakuna magonjwa na wala Mungu hata siku moja haleti magonjwa bali maovu yetu. Ndiyo maana Yesu anaweza kusame dhambi maana yeye ndiyo huo utakaso kwani damu yake aliyomwaga msalabani ndiyo yenye nguvu ya kutusafisha dhambi zetu zilizo nyekundu kama bendera kuwa nyeupe kama theluji na miyo yetu migumu kama jiwe kuwa laini kama sufi.

Unaongelea asitumie jina la Yesu je wajua kwamba hakuna njia kweli ama uzima pasipo Yesu? Jina la Yesu ndiyo jina kuu kuliko majina yote. Kwa serikali ya Tanzania Jina la Jakaya Kikwete ndilo jina kuu kupita yote siyo kwasababu ni mtoto Wa Kikwete no kwasababu ya authority aliyonayo ya kuamri majeshi yote nayo yakafanya kama atakavyo amuru kwa kufuata katiba ya Jamuhuri ya Tanzania. Basi na kwajinsi hiyo hiyo jina la Yesu ndilo jina pekee mbinguni na duniani lenye uwezo wa kuamrisha majeshi yote ya Mungu kufanya kama anavyoelekeza kwafuata wisdom ya Mungu (Roho mtakatifu). Ndiyo maana kwa jina hilo tunaujasiri wote maana tukilitumia twaweza fanya chochote kama tu tutafanya kufuatana kwa maelekezo ya roho mtakatifu ambaye anakaa ndani yetu; kwa hivyo kwa neno au kwa tendo twaenenda sawa sawa na mapenzi yake. Na mapenzi yake ni haya kila roho ya mwanadamu iirithi uzima wa milele ambao haupatikani katika jinsi yoyote isipokuwa kwa kuliamini hili jina.

Mimi nikisema kwajina la Yesu hakuna uponyaji utakao fanywa na Babu wa Semunge na ndani yake Mungu akaona nimefanya kwa sifa na utukufu wake na siyo kwaajili ya self motives kama kukosa wateja wa kanisa langu au mafungu yao ya kumi na sadaka; inakuwa hivyo no less or more. Maana kila malaika atafuata order yangu. Neno la Mungu linasema hatupati tuviombavyo kwasababu twaomba vibaya kwaajili ya tamaa zetu za kimwili na kuwa maovu yetu yametufarakanisha na Mungu hivyo hata tukiomba yeye hasikii. Ndipo akasema ninyi mkiwa ndani yangu na maneno yangu yakiwa ndani yenu ndipo sasa ombeni lolote kwa jina langu baba atawapeni; hata sasa hamjaomba lolote ombeni nanyi mtapokea ili furaha yenu iwe kamili. Kwa ufupi wengi wetu tunaomba kwa selfish motives, kwamba ili mimi ndiyo nionekane mtakatifu kuliko wote na watumishi wengine wawe second class; ili kuwaumiza wengine e.g mimi ni mkristo naomba nguvu za Mungu ziwe juu yangu ili waislamu na wale wasio wa dini yangu wakome; niwe na afya ili nistarehe na wanawake na ulevi bar; nipate cheo ili watoto wangu wasipate shida na mimi niukate. Nifaulu ili watu wote waniite mimi genious na hivyo nikiwa profesor basi wanikome hapo University hasa wale wanaojidai wao ndo vichwa; Nioe mke mzuri kupita wote ili watu wote wajue mimi pamoja na sura yangu mbaya ni mwanaume wa nguvu etc..Hatusemi hadharani lakini Mungu ajuaye roho ya mwanadamu ajua yote ndiyo maana kwa upendo wake hutunyima hizo zote ili hatimaye tubaki tukimtegemea yeye na kuurithi uzima wa milele.

Amri ya Mungu imekamilika katika upendo maana katika pendo hakuna awezaye kutenda dhambi. Ukimwadhibu mtu kwasababu hiyo tabia inamsababisha huyo kutenda dhambi na kuumiza wengine Mungu yuko pamoja na wewe na ndipo utashangaa binadamu wote watakuchukia lakini baraka zitakufuata na kupitiliza hata usiwe na sehemu ya kuziweka. Lakini ukiacha kuadhibu mtu kwasababu unajua ukifanya hivyo utavuruga mahusiano yako na deal zako za kifisadi basi hata kama ukijipa kila aina ya heshima zote zitageuka kukuzomea na hatimaye utajiona mpweke usiyependwa na yeyote na hatimaye kuishia kulipiza kisasi ambacho nacho hatima yake ni kukugeukia wewe na njia zote ulizotumia kukumaliza wewe mwenyewe huku wale uliowatuhumu pasipo sababu wakiendelea kuheshimiwa na kuinuliwa mbele ya macho yako.

Be blessed!
 
Umesema Dunia ina watu zaidi ya bilioni 6. Hebu sasa jaribu kuwaza, iwapo watu bilioni moja tu duniani kote wanaumwa magonjwa sugu, wakija Tanzania na babu akawatoza sh 500, mwisho wa siku atakuwa amepata sh ngapi? 500x1,000,000,000=???

Ndo shida yako kubwa labda ipo hapo!!!! Bilioni 500 inakunyima usingizi, ila zile ulizochotewa EPA n.k wala hazikunyimi usingizi. Halafu unasemaje wizi pale mtu anapofanya kazi na kulipwa. Ni sawa na wewe ugundue kitu leo, tuseme ugundue mseto ambao mtu akijipaka mara moja hatajipaka losheni wala mafuta tena na atanukia apendavyo daima, mfano tu, so ukianza kuuza kwa jelo, si lazima nawe utauza dunia nzima na kupata kama babu, kwani ugomvi?
Mbona Nokia zinauza sana mtaani haikunyimi usingizi, nahisi watu 20m wenye simu Tanzania tu walau 15m ni Nokia, sasa 15,000,000x30,000 (chukulia simu ni TZS 30,000 tu) mbona hapo hapakunyimi usingizi?

Babu angesema anafanya biashara ya dawa tungekaa kimya. Lakini kwakuwa anadai hiyo ni huduma aliyopewa na Mungu lazima tumpinge kadri tuwezavyo. Mungu hafanyi biashara ya uponyaji. Ni wapi katika Biblia Yesu aliwaponya wagonjwa baada ya kupokea senti? MTAIJUA TU KWELI NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU!!
 
Ungeanza kwanza na manabii, mitume, na maaskofu wa uongo waliojijengea mahekalu ya kufanyia biashara kwa kisingizio cha kuhubiri injili na kuponya na kufufua wafu.
Wapo wengine wenu tunaofahamu kuwa kisima cha kubatiza mlichojenga mbele ya kanisa lenu kina ushetani mkubwa, na inasemekana wanaoingia kubatizwa 'kwa maji mengi' wanaona humo joka, tumeamua kukaa kimya kuwasitiri, leo mnaona Babu kawanyima riziki ya siku chache, mnaanza kupagawa.
Hizo hoja hazinihusu mimi. Unapoteza muda wako kuziandika. Am not a Pastor, am not a Bishop. Am a mediaman, Sir. My job is to use media to tell people the truth.
 
Hv Mediaman ni mmoja kt ya waumini wa kanisa gani? Maana nahisi ni mmoja kt ya wale waliopungukiwa na waumini hapo kwake. Mmmm!
 
Sasa Babu si hataki jamani???? nenda ujaribu kumpa gari kama atakubali ...............amesema Mungu wake kamkataza!!!!!!!!!!! Mungu gani anayekukataza usifanikiwe????? Mungu wa Kweli anabariki na kuinua; anabadilisha maisha ....sasa anayemkataza Babu ni Mungu kweli au ni mungu yupi???? nauliza!!!

I am sorry this is a wrong quote; Your is okay!
 
<p>
..kulingana na Neno la Mungu katika kitabu cha Yeremia 23:25-32. Neno la Mungu (Biblia) katika mistari hiyo linasema hivi: </p>
<p>&quot.....Nabii aliye na ndoto, na aseme ndoto yake; na yeye aliye na neno langu, na aseme neno langu kwa uaminifu......

Hapo mtoa mada umepaona? Ama ni wale mnafanya biblia zenu kuwa mto wa kulalia? Je,babu ametoa ndoto yake kwa uaminifu ama la? Chunga sana usemayo kijana..ushuhuda uko wazi.walioponywa na ndoto ya babu wamerudisha shukrani kwa Mungu wala si kwa babu ama shetani!!!

Usikatize maneno ya Mungu mbona hujamalizia mpaka mwisho upate maana kamili? Kila panctuation kwenye neno la Mungu lina maana yake so reread that passage to get the context na pia revelation ya kimungu. Pia kila ushuda wa ndoto au maono lazima ushudiwe na vitu vitatu ndiyo ukamilike kuwa neno la Mungu. Huwezi ota tu wewe na asiwepo mtu mwingine yeyote hajashuhudiwa ukajia aminisha kuwa Mungu ndiyo kasema; hii ni principal ya Kimungu ndiyo maana neno la Mungu lina sema ushuhuda wa watu watatu ni kamili nami yuko anayenishudia baba na roho mtakatifu na sehemu nyingine inasema dunia yapo maji na moto na neno kama si kosei si kumbuki vizuri.

God is not the authour of confusion popote kwenye confusion roho ya Mungu haipo! Kuna mchungaji Mnaijeria alitokewa katika ndoto huyo mtu akampa a place hwere to go every day na kila alipoenda alikuwa anaongea na sauti ilikuwa inampa maelekezo ya nini cha kufanya. Akamwambia ninakubariki mikono yako yeyote utakaye mwombea atapona kwahiyo nakutuma kwenda kuponya na kuondoa shida za watu. It sounds biblical. Basi akaenda kama alivyotumwa akaanza huduma kweli akafanya sign and wonders kama alivyo amriwa. Lakini alikuwa anambiwa asiache kwenda kufanya maombi hapo kila mara ili aendelee kupata anointing. As days went na kanisa limekuwa na hundred thousands of believers then akawa anashindwa kufuata hayo masharti na alikuwa anaendelea kuongezewa masharti. Siku moja akasema no I am tired huyu Mungu kwanini ananipa masharti namna hii haoni kwamba ni mateso? Akasema I am not going today, akiwa anawaza kutokwenda mara sauti ikaanza kumwambia do you know where I took you from? Now that nakwambia unitumikie unaanza kuleta ubishi kwasababu all is well with you? Akashangaa what type of this God, is it the same God of love and mercy anaenishurutisha? Akasema God I am not going duu mara akashangaa yule mtu anamwambie then I will take my anointing and you would see what I can do to you. Basi yule mchungaji aka perceive rohoni mwake he is already in another spiritual realm (Already possesed) akatoka kwenda kwa Pr. mwingine nje na kanisa lake akamweleza yote. They entered into fast and prayers wakiwa wanaendelea siku moja aka manifest mbele ya yule Pr mwenzake ndo ikajulikana it was the Devil himself in operation. Afanyiwa deliverance na huduma yake ikaishia hapo ikabidi lile kanisa walivunje.

Quite few ministers wanaweza wakawa humble kiasi hicho once wakigundua tayari wako held in bondage. Akiangalia status yake sadaka anazopata na hali yake ya maisha basi anakubali yaishe. I had almost the same experience in the church where I am. Mchungaji wangu mmoja ambaye anajulikana kama nabii hapo kanisani, nikiwa mchanga kabisa kiroho siku moja something bad happened kwa senior pastor wetu alivyoenda kwenye huduma sehemu. Apata a kind of paralysis sitaiweka kihalisia maana some wansoma hapa watamjua. Then I dreampt of the whole setting and who is behind. Nikaogopa mimi ndo kwanza mchanga mmh nikaona shetani anataka kuniteka. Then nikaendlea tu kumwamini. Lakini siku zilivyokuwa zinaenda nami nikalijua neno la Mungu basi vikawa vituko vinatokea and no body was awere of whats the reason. Baadaye God started warning me nisishiriki katika mambo ya huyo pr siku moja nilikuwa nasafiri and God showed kwamba nikienda kanisani watakwepo Pr. watatu pale madhabahuni mmoja atakuwa huyo lakini yeye atainuka kuja kuniwekea mikono nami nikaambiwa nikatae na nimkemee then ata manifest and all will be clear to everybody. Nikaona atakuwa amevaa nguo gani na yule mwingine pia. So nikaogopa sana. Nika mfuata yule Pr. mwingine niliyeambiwa atakuwepo pia. Nikamweleza wha is going to happen na je nifanyeje? Yule Pr akanishauri kwamba inaweza kuwa shtani anakuchezea but let us wait and see. Then sunday came nami nikatoka kuaga kanisa, looh it was exactly as I saw, yule Pr. mwingine akaanza kucheka maana ilikuwa kama dramer vile. Mtihani ukawa kwangu sasa nitakataaje mbele ya kanisa zima? Uwogaukaniingia nikajikuta nakubali kuwekewa mikono; that actualy was a sin kwani nilikataa maagizo ya Mungu kwa kuogopa macho ya wanadamu. Then my friends what happended in my life only God knows hell broke loose na nusu ningepoteza maisha, kazi ndoa na watoto wangu. Then nikaamua sasa kuingia kwenye war fare na hayo majeshi, todate huyo nabii japo hawasemi hadharani almost everybody knows who he is! Mbaya zaidi wakagombana hadharani na mwenzake wakituhumiana uchawi.

Wapendwa shetani yupo katikati ya wana wa Mungu na hapo ndipo hasa anafanya kazi kwa nguvu zote maana wale wengine tayari wako upande wake so hana kazi kule. Shatani haendi bar wala kwenye madanguro maana yale ni magereza yake wote walioko huko ni miliki yake. Yeye kazi yake iko kanisani kuangusha makamanda wa majeshi ya miguu ya Mungu huku duniani. Anatafuta wale hasa wenye kutibua ngome yake usiku na mchana. Na kama ni experience basi yeye ni researcher aliyebobea kwenye kutafuta uovu ulio ndani ya mtu yeyote maana ndiyo authour hasa wa uovu na anajua sekunde moja utayotoka nje ya wigo wa protection ya Mungu hiyo ni kibali cha yeye kukushugulikia ipasavyo ili iwe fundisho kwa wengine wote wanaomsumbua katika ufalme wake. Lakini tuna neema kubwa kwa Kristo Yesu naye hasinzii wala hachoki siku zote ili mission yake itimie.
 
CRAP! CRAP! CRAP!!

Mbona husemi nabii wa ukweli tutamjuaje au ni wivu wa kiinjili? Kama kawaida yenu wahubiri wengi mmekuwa mkituchakachua mnalazimishia hisia zenu kuwa maono... sipati picha siku ya mwisho... nyinyi ni nani hata mtoe hukumu

Hebu tutumie lgic hii... hawa wahubiri wengine ambao tunaona kila ishara ya ,maisha ya ufahari wanatoa wapi hizo pesa? Magari ya ajabu ajabu na miradi mikubwa mikubwa... acheni bwana maana kila mtumishi atakula katika utumishi wake... yeye hapokei sadaka isiyo na kikomo kama wengine... hachangishi wala hahitaji zile mnazoziita mbegu... kinachowauma ni nini hasa? Msitizame ya mwili na kutuhadaa acheni

Kristo ni mmoja tu na atabaki kuwa yeye yule jana leo na hata milele sasa nyinyi wanadamu mnajipachika kila majina na makundi kedekede na wengine makundi hayo ya kikiristo ya 'kiroho' kama mngethamini kile alichosema mngekuwa mnaungana bila kuhangaikia utukufu, kwani kanisa likiwa na manabii hamsini kuna ubaya gani?

Wacha Crap zako mpendwa unatukwaza sana
 
Mtakitukana sana Kibabu na mifano kibao na kujifanya mnajua sana Biblia kuzidi hata watu wa Roma walioitangaza Biblia dunia hii.

Mtabwabwaja na kuchonga sana nye watu wa roho Mbaya ..............

Ila ukweli ni kuwa KIBABU kinadunda na Mia yake kwa kila mteja (Katika 500, anachukua 100 tu).....

Na nyie Wezi na Vibaka kwa kutumia jina la YESU, mtashangaa Makanisa yenu yanakuwa tupu.....

LOOSERRRRRRR!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Mchungaji%2BMstaafu%2BAmbilikile%2BMasapile%2B%2528kushoto%2529%2Bakimpa%2Bdawa%2BWaziri%2Bwa%2BNchi%2BOfisi%2Bya%2BWaziri%2BMkuu%2B%2528Sera%2Bna%2BUratibu%2529%252C%2BWilliam%2BLukuvi%2Bna%2BRosemary%2BNyerere%2Bmwishoni%2Bmwa%2Bwiki%2Biliyopita..jpg

Pichani: Waziri William Lukuvi na Rosemary Nyerere, wakipata dawa kwa Babu bila mkaruzo....

Weee sasa nenda kawaambie hao nao kuwa hawana akili.

++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

WAKATI mamia ya watu wakiendelea kumiminika kupata tiba ya dawa ya magonjwa sugu kwa mchungaji wa KKKT katika Kijiji cha Samunge, Wilayani Loliondo, jana ilikuwa zamu ya Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye (pichani) kupata kikombe cha babu huyo.

Hatua ya Sumaye ni mwendelezo wa uwazi kwa viongozi wanaokwenda Samunge siku za karibuni tofauti na awali ambao baadhi ya vigogo walidaiwa kwenda kupata tiba hiyo kwa kificho.Lakini, kama ilivyokuwa kwa aliyekuwa Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa ambaye alifika Samunge, Loliondo siku tatu zilizopita na kunywa kikombe cha Babu, jana Sumaye naye alifika kijijini hapo kunywa kikombe hicho.

Akiongozana na watu kumi wa familia yake, Sumaye alifika kijijini Samunge saa 7 mchana ambapo alipokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Loliondo, Elias Wawalali ambaye kwa kutumia njia maalumu ya viongozi alipelekwa moja kwa moja kwa Mchungaji Mwasapile na kunywa dawa hiyo.
 
nashindwa waelewa hao wanaompinga babu nawafananisha na wale wenye makanisa waliokimbiwa na waumini wao kwenda kupata tiba cha msingi ni uponyaji tu hasa na kwababu hana ushawishi pata kikombe nenda zako hamna amia kanisa ili wala nenda kanisa lime baki na imani yako tu
 
habari zilizoandikwa katika magazeti na kusikika katika redio na televisheni siku kadhaa zilizopita zilieleza kwamba babu wa loliondo ameoteshwa na mungu dawa ya kuwatibu watu magonjwa sugu.

5. nabii wa uongo hugeuza au kupinga baadhi ya maneno ya mungu. babu wa loliondo ni miongoni mwa wale wanaopinga ubatizo wa kibiblia wa maji mengi. Badala yake anatetea ubatizo wa watoto wadogo, jambo ambalo halimo katika biblia. Yesu aliwabariki watoto, hakuwabatiza. Mtawatambua kwa matunda yao! Sio hilo tu anapinga pia agizo kuu la yesu katika marko 16:15-18. Katika mistari hiyo watumishi wa mungu wameagizwa kwenda ulimwenguni mwote kuihubiri injili na kuweka mikono juu ya wagonjwa ili wapate afya. Yeye babu kwa ukaidi alionao toka 1991, badala ya kutoka na kwenda katika miji na vijiji (kama yesu alivyofanya - mt 9:35) ili kuwahubiri wenye dhambi na kuwapoza wagonjwa (walioko shinyanga, kigoma, rukwa, namibia nk nk), eti ameamua kujenga makao ya kudumu huko huko porini. Hataki kutoka, halafu anasema mungu amemtuma. Mungu hawezi kupingana na neno lake.

"aonywaye mara nyingi akishupaza shingo, atavunjika ghafla..." mithali 29:1.

uufffff!!!!!!
 
Kwa kutumia Biblia unaweza ku-justify the un-justifiable ukiwa na mind ya kupotosha....Nimeweka post yenye kuhoji ambayo inahitaji neno zaidi ya kutoa maneno tu

JE UNA DEVINE REVELATION KUWA BABU HAJAPATA MAONO YA KIMUNGU?? Au unaongea kama Mafarisayo waliokuwa wakitumia Torati kupitezea ukweli wa Yesu kuwa mwana wa Mungu na kuja kutekeleza jukumu la ukombozi

Kama HUNA DEVINE REVELATION (kikata maneno kikuu) better keep quite mpaka watakaopata Reveleation waje

https://www.jamiiforums.com/jf-chit...asiri-wa-kimaono-wa-kupinga-tiba-ya-babu.html

Mediaman wewe ni Mwongo:
1. Wewe ndiye uliyeanzisha thread nyingine isemayo: Siri Imefichuka! Babu wa Loliondo ametumwa na shetani. Ukweli ni kuwa hakukuwa na siri yoyote isipokuwa mahubiri yako ukitumia maandiko kama unavyopenda yasupport hoja yako. Na hapa unakuja na thread nyingine eti Babu wa Loliondo yupo hatarini ... Hatari gani? Kichwa cha habari yako hakina tofauti na vichwa vya magazeti ya alasiri na dar leo au na magazeti ya udaku. Kichwa kingine habari nyingine.
2. Hapa unasema: Wachunguzi na wataalam wa masuala ya kiroho wamegundua kuwa ndoto hiyo ni ya uongo.Je, wewe ndiye mchunguzi huyo? Habari yako haina reference hata moja ya mchunguzi wa mambo ya kiroho na taarifa yake inasemaje? Ninachoona ni porojo zako zisizoenda shule na ambazo zina mwegemeo wa mafundisho ya Biblia yaliyo nusu nusu.
3. Kwa kutumia Yeremia 23:25-32, unajaribu kushawishi watu kuwa Mungu haoteshi watu ndoto kipindi hiki kwa vile ni makapi: Katika mistari hiyo, BWANA Mungu anazifananisha ndoto na makapi.Huu ni upotoshaji wa Biblia wa waziwazi. Petro katika Mdo 2:17 alimnukuu Nabii Yoeli na alisema : Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu, nitawamwagia watu wote Roho wa yangu, na wana wenu na binti zenu watatabiri; na vijana wenu wataona maono; na wazee wenu wataota ndoto. Je, andiko hili haliko kwenye Biblia yako? [Kwa bahati mbaya sana kama unaamini juu ya litera translation ... basi ni wazee ndo wanaota ndoto na hapo kwa babu ndo imefika].
4. Unasema: Vyanzo vingine vya habari kutoka nje ya nchi, vimethibitisha kuwa huyo babu wa Loliondo ni nabii wa uongo - Unaendeleza uongo wako kwa kusingizia vyanzo vingine kutoka nje ya nchi - vyanzo gani hivyo? Acha kutuzuga hapa? Kama una vyanzo sema nani na nani kasema nini kwa ushahidi upi?

Nasisitiza: Mediaman ni mwongo kwa vile anajitahidi kutafuta kuungwa mkono na watu ambao hawapo. Biblia inasema: Bali maneni yenu yawe Ndiyo, ndiyo; Siyo, siyo; kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa yule mwovu (Mat 5:37).
Na kwavile Mediaman umethubutu kusema uongo basi wewe ndiye mtumishi wa shetani. Yesu alisema: Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuuaji tangu mwanzo ; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo na baba wa huo. (Yon 8:44).
Nafurahia zaidi inavyosomeka kiingereza: (John 8:44) - You belong to your father, the devil, and you want to carry out your father's desire. He was a murderer from the beginning, not holding to the truth, for there is no truth in him. When he lies, he speaks his native language, for he is a liar and the father of lies.
 
MediaMan bado naendelea kutafakari some of the issues in your post naona havina muelekeo wa kuweka ukweli zaidi

Unapohoji mtu kupata uhalali kwa kuwa amebatizwa maji mafupi unamaanisha nini?

Didnt God use the lowly to perform great and mighty works?

Kati ya Babu Mvh. Mstaafu "aliebatizwa kwa maji mafupi" na yule Mwanamke Kahaba wa kwenye Biblia Mungu aliemtumia, ni nani mwenye uhalali wa kutumiwa na Mungu kwa context yako?

:embarassed2:

Au ulitaka afunuliwe Mwingira, Kakobe na wana-maji marefu ndio uamini?

Weka hoja nyingine lakini sio hizi maana Mungu hutumia wanaodharaulika kufanya mambo makubwa.......He is God and not MediaMan...and ofcourse thanks that he is not maana tungekoma
 
mtakitukana sana kibabu na mifano kibao na kujifanya mnajua sana biblia kuzidi hata watu wa roma walioitangaza biblia dunia hii.

Mtabwabwaja na kuchonga sana nye watu wa roho mbaya ..............

Ila ukweli ni kuwa kibabu kinadunda na mia yake kwa kila mteja (katika 500, anachukua 100 tu).....

Na nyie wezi na vibaka kwa kutumia jina la yesu, mtashangaa makanisa yenu yanakuwa tupu.....

Looserrrrrrr!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

mchungaji%2bmstaafu%2bambilikile%2bmasapile%2b%2528kushoto%2529%2bakimpa%2bdawa%2bwaziri%2bwa%2bnchi%2bofisi%2bya%2bwaziri%2bmkuu%2b%2528sera%2bna%2buratibu%2529%252c%2bwilliam%2blukuvi%2bna%2brosemary%2bnyerere%2bmwishoni%2bmwa%2bwiki%2biliyopita..jpg

pichani: Waziri william lukuvi na rosemary nyerere, wakipata dawa kwa babu bila mkaruzo....

Weee sasa nenda kawaambie hao nao kuwa hawana akili.

++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

wakati mamia ya watu wakiendelea kumiminika kupata tiba ya dawa ya magonjwa sugu kwa mchungaji wa kkkt katika kijiji cha samunge, wilayani loliondo, jana ilikuwa zamu ya waziri mkuu mstaafu, frederick sumaye (pichani) kupata kikombe cha babu huyo.

Hatua ya sumaye ni mwendelezo wa uwazi kwa viongozi wanaokwenda samunge siku za karibuni tofauti na awali ambao baadhi ya vigogo walidaiwa kwenda kupata tiba hiyo kwa kificho.lakini, kama ilivyokuwa kwa aliyekuwa waziri mkuu mstaafu edward lowassa ambaye alifika samunge, loliondo siku tatu zilizopita na kunywa kikombe cha babu, jana sumaye naye alifika kijijini hapo kunywa kikombe hicho.

Akiongozana na watu kumi wa familia yake, sumaye alifika kijijini samunge saa 7 mchana ambapo alipokelewa na mkuu wa wilaya ya loliondo, elias wawalali ambaye kwa kutumia njia maalumu ya viongozi alipelekwa moja kwa moja kwa mchungaji mwasapile na kunywa dawa hiyo.

Hata angeenda Obama sishangai
 
MediaMan bado naendelea kutafakari some of the issues in your post naona havina muelekeo wa kuweka ukweli zaidi

Unapohoji mtu kupata uhalali kwa kuwa amebatizwa maji mafupi unamaanisha nini?

Didnt God use the lowly to perform great and mighty works?

Kati ya Babu Mvh. Mstaafu "aliebatizwa kwa maji mafupi" na yule Mwanamke Kahaba wa kwenye Biblia Mungu aliemtumia, ni nani mwenye uhalali wa kutumiwa na Mungu kwa context yako?

:embarassed2:

Au ulitaka afunuliwe Mwingira, Kakobe na wana-maji marefu ndio uamini?

Weka hoja nyingine lakini sio hizi maana Mungu hutumia wanaodharaulika kufanya mambo makubwa.......He is God and not MediaMan...and ofcourse thanks that he is not maana tungekoma

Mungu anaweza kuwatumia wanaodharauliwa na watu sio wanaomdharau Mungu. Mungu ameagiza tubatizwe katika maji mengi wewe unajitungia ubaatizo wako, atakutumia wewe! Utatumiwa na "mungu" wa herufi ndogo. mungu wa dunia hii shetani anayemtumia babu sasa
 
Mediaman wewe ni Mwongo:
1. Wewe ndiye uliyeanzisha thread nyingine isemayo: Siri Imefichuka! Babu wa Loliondo ametumwa na shetani. Ukweli ni kuwa hakukuwa na siri yoyote isipokuwa mahubiri yako ukitumia maandiko kama unavyopenda yasupport hoja yako. Na hapa unakuja na thread nyingine eti Babu wa Loliondo yupo hatarini ... Hatari gani? Kichwa cha habari yako hakina tofauti na vichwa vya magazeti ya alasiri na dar leo au na magazeti ya udaku. Kichwa kingine habari nyingine.
2. Hapa unasema: Wachunguzi na wataalam wa masuala ya kiroho wamegundua kuwa ndoto hiyo ni ya uongo.Je, wewe ndiye mchunguzi huyo? Habari yako haina reference hata moja ya mchunguzi wa mambo ya kiroho na taarifa yake inasemaje? Ninachoona ni porojo zako zisizoenda shule na ambazo zina mwegemeo wa mafundisho ya Biblia yaliyo nusu nusu.
3. Kwa kutumia Yeremia 23:25-32, unajaribu kushawishi watu kuwa Mungu haoteshi watu ndoto kipindi hiki kwa vile ni makapi: Katika mistari hiyo, BWANA Mungu anazifananisha ndoto na makapi.Huu ni upotoshaji wa Biblia wa waziwazi. Petro katika Mdo 2:17 alimnukuu Nabii Yoeli na alisema : Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu, nitawamwagia watu wote Roho wa yangu, na wana wenu na binti zenu watatabiri; na vijana wenu wataona maono; na wazee wenu wataota ndoto. Je, andiko hili haliko kwenye Biblia yako? [Kwa bahati mbaya sana kama unaamini juu ya litera translation ... basi ni wazee ndo wanaota ndoto na hapo kwa babu ndo imefika].
4. Unasema: Vyanzo vingine vya habari kutoka nje ya nchi, vimethibitisha kuwa huyo babu wa Loliondo ni nabii wa uongo - Unaendeleza uongo wako kwa kusingizia vyanzo vingine kutoka nje ya nchi - vyanzo gani hivyo? Acha kutuzuga hapa? Kama una vyanzo sema nani na nani kasema nini kwa ushahidi upi?

Nasisitiza: Mediaman ni mwongo kwa vile anajitahidi kutafuta kuungwa mkono na watu ambao hawapo. Biblia inasema: Bali maneni yenu yawe Ndiyo, ndiyo; Siyo, siyo; kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa yule mwovu (Mat 5:37).
Na kwavile Mediaman umethubutu kusema uongo basi wewe ndiye mtumishi wa shetani. Yesu alisema: Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuuaji tangu mwanzo ; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo na baba wa huo. (Yon 8:44).
Nafurahia zaidi inavyosomeka kiingereza: (John 8:44) - You belong to your father, the devil, and you want to carry out your father's desire. He was a murderer from the beginning, not holding to the truth, for there is no truth in him. When he lies, he speaks his native language, for he is a liar and the father of lies.

Nenda kwanza shule ya uandishi wa habari ndio utaweza kuchambua post zangu na vichwa vyake.
 
Kwa kutumia Biblia unaweza ku-justify the un-justifiable ukiwa na mind ya kupotosha....Nimeweka post yenye kuhoji ambayo inahitaji neno zaidi ya kutoa maneno tu

JE UNA DEVINE REVELATION KUWA BABU HAJAPATA MAONO YA KIMUNGU?? Au unaongea kama Mafarisayo waliokuwa wakitumia Torati kupitezea ukweli wa Yesu kuwa mwana wa Mungu na kuja kutekeleza jukumu la ukombozi

Kama HUNA DEVINE REVELATION (kikata maneno kikuu) better keep quite mpaka watakaopata Reveleation waje

https://www.jamiiforums.com/jf-chit...asiri-wa-kimaono-wa-kupinga-tiba-ya-babu.html

Unasubiri Revelation ndio ujue kuwa shetani yupo. Pole sana
 
Mtoa mada ana kila dalili ya kuchanganyikiwa na kuijiona yeye ndiyo hasa anaejua ufunuo woote wa bibilia!!
Mchingaji anasema mungu kamwabia kupitia ndoto....mleta nada unatumia biblia kumwinua shetani!!!
Mwacheni mchingaji afanye kile alichoambiwa na Mungu. Nanyie anzisheni tiba itayotoka kwa Mungu kama hamuwezi kaeni kimya!!
Mshindwe na mwende motoni!
 
Mediaman wewe ni Mwongo:
1. Wewe ndiye uliyeanzisha thread nyingine isemayo: Siri Imefichuka! Babu wa Loliondo ametumwa na shetani. Ukweli ni kuwa hakukuwa na siri yoyote isipokuwa mahubiri yako ukitumia maandiko kama unavyopenda yasupport hoja yako. Na hapa unakuja na thread nyingine eti Babu wa Loliondo yupo hatarini ... Hatari gani? Kichwa cha habari yako hakina tofauti na vichwa vya magazeti ya alasiri na dar leo au na magazeti ya udaku. Kichwa kingine habari nyingine.
2. Hapa unasema: Wachunguzi na wataalam wa masuala ya kiroho wamegundua kuwa ndoto hiyo ni ya uongo.Je, wewe ndiye mchunguzi huyo? Habari yako haina reference hata moja ya mchunguzi wa mambo ya kiroho na taarifa yake inasemaje? Ninachoona ni porojo zako zisizoenda shule na ambazo zina mwegemeo wa mafundisho ya Biblia yaliyo nusu nusu.
3. Kwa kutumia Yeremia 23:25-32, unajaribu kushawishi watu kuwa Mungu haoteshi watu ndoto kipindi hiki kwa vile ni makapi: Katika mistari hiyo, BWANA Mungu anazifananisha ndoto na makapi.Huu ni upotoshaji wa Biblia wa waziwazi. Petro katika Mdo 2:17 alimnukuu Nabii Yoeli na alisema : Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu, nitawamwagia watu wote Roho wa yangu, na wana wenu na binti zenu watatabiri; na vijana wenu wataona maono; na wazee wenu wataota ndoto. Je, andiko hili haliko kwenye Biblia yako? [Kwa bahati mbaya sana kama unaamini juu ya litera translation ... basi ni wazee ndo wanaota ndoto na hapo kwa babu ndo imefika].
4. Unasema: Vyanzo vingine vya habari kutoka nje ya nchi, vimethibitisha kuwa huyo babu wa Loliondo ni nabii wa uongo - Unaendeleza uongo wako kwa kusingizia vyanzo vingine kutoka nje ya nchi - vyanzo gani hivyo? Acha kutuzuga hapa? Kama una vyanzo sema nani na nani kasema nini kwa ushahidi upi?

Nasisitiza: Mediaman ni mwongo kwa vile anajitahidi kutafuta kuungwa mkono na watu ambao hawapo. Biblia inasema: Bali maneni yenu yawe Ndiyo, ndiyo; Siyo, siyo; kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa yule mwovu (Mat 5:37).
Na kwavile Mediaman umethubutu kusema uongo basi wewe ndiye mtumishi wa shetani. Yesu alisema: Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuuaji tangu mwanzo ; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo na baba wa huo. (Yon 8:44).
Nafurahia zaidi inavyosomeka kiingereza: (John 8:44) - You belong to your father, the devil, and you want to carry out your father's desire. He was a murderer from the beginning, not holding to the truth, for there is no truth in him. When he lies, he speaks his native language, for he is a liar and the father of lies.

Wewe kwenye post hii umeandika Ndiyo Siyo Ndiyo Siyo - ongea pointi !
 
Mtoa mada ana kila dalili ya kuchanganyikiwa na kuijiona yeye ndiyo hasa anaejua ufunuo woote wa bibilia!!
Mchingaji anasema mungu kamwabia kupitia ndoto....mleta nada unatumia biblia kumwinua shetani!!!
Mwacheni mchingaji afanye kile alichoambiwa na Mungu. Nanyie anzisheni tiba itayotoka kwa Mungu kama hamuwezi kaeni kimya!!
Mshindwe na mwende motoni!

Afadhali umetambua kuwa babu kaambiwa na mungu kupitia ndoto. mungu anayeandikwa kwa herufi ndogo ni shetani. Pole sana
 
Back
Top Bottom