Babu Seya na Wanae kusota Jela Maisha!

Jamani wabakaji TZ ni wengi wengine. Wamebaka mpaka watoto wao. Naombeni ushahidi wa adhabu iliyowahi kutolewa kwao japo wa nne tu kati ya 2000. YAANI KWA BABU SEYA KUNA MKONO WA MTU ila wahusika wasisahau kuwa. ATAWALAYE KWA UPANGA HUFA KWA UPANGA
 
Hakuna ukweli familia ikabaka kuanzia baba mpaka watoto wa chini kabisaa, hizi ni hukumu za kipirato zinazoamuliwa na walio juu ya sheria, chuki binafsi za mapenzi zinazofanywa na wakuu wasio na huruma hata chembe, mwanadamu anageuka kuwa mungu mtu anaamuru fulani afungwe maisha na inakuwa hivyo, dhambi mbaya sana hii kuzima ndoto za mwenzako, na kumpa mateso ya maisha, kama walibaka yule mwalimu aliyekuwa anasemekana alikuwa anapewa hela ya kuwapa wale watoto ili waende kwa babu Seya yu wapi mbona aliachiwa huru? Mwlimu huyu alikuwa akifundisha pale Mbuyuni, inauma sana ukweli tunaujuwa na hawa mahakimu wenye kutekeleza amri za mabwana zao wanaowapa nafasi hizi wamekuwa ni watu wanaotoa hukumu kwa maagizo, shame on u stupid judges, taaluma yenu iko wapi kama mnafanyishwa kazi kwa remort? Kweli usije ukala cha mkubwa. Inauma sana
 
...Kwa kweli inatia huruma .. lakini je ni kweli majaji wote hawatendi haki?
 
Justice is justice though it's always delayed n' finally done only by mistake
 
“waheshimiwa majaji kwasababu jopo lenu katika hukumu yake lilikiri wazi wazi kuwa mahakama ya kisutu ilikosoea kurekodi ushahidi wa watoto wa dogo ambao walidai walitendewa vibaya na waomba rufaa(Nguza na Papii), na sheria za nchi zipo wazi kabisa zina sema endapo mahakama itabaini kuwa mahakama ya chini ilikiuka taratibu za kurekodi ushahidi wa watoto wa dogo, basi ushahidi ule wa watoto wa dogo uliotumika katika mahakama ya chini kuwatia hatiani washitakiwa, ushahidi huo wa watoto unafutwa na waomba rufaa au washitakiwa wanaachiriwa na pia maamuzi ya kesi mbalimbali yaliyokwisha kutolewa na mahakama hii; “Nafahamu ni kazi ngumu sana kuwashawishi nyie majaji kubadili uamuzi wenu mlioutoa katika hukumu ya Februali 2010 ambapo mliwatia hatiani wateja wangu, ila kwa uterezi huo wa kisheria niliouanisha unaonyesha katika hukumu yenu mlikubaliana na hoja yangu kuwa Mahakama ya Kisutu ilikosea kurekodi ushahidi watoto wadogo ,naamini mtatumia busara zenu na kufuata sheria inayosema wazi wazi kuwa endapo utaratibu wa kurekodi ushahidi wa mtoto utakiukwa basi ushahidi huo utafutwa na wateja wangu wataachiliwa huru, basi leo naiomba mahakama hii iwaachirie huru wateja wangu" MARANDO

Natamani sana ningepata majibu ya majaji hapa.
 
Sometimes huwa nahisi duniani ni nadra kupata haki! Anyway Mungu awasimamie iko siku atawanyooshea mkono.
 
Kuna watu hawaamini kuna siku ya kiama. Hawa jamaa wanatia huruma sana lkn waliopelekea mateso yao wajue siku hiyo kila goti litapigwa na machozi yao yatakuwa ya damu.
 
nimeamini kweli watu wamenunuliwa kuja hapa na kuwatetea wabakaji. Mahakama imejiridhisha ni wakosaji. Kelele za nini?
 
Nakubaliana na wewe 100%. Tena katika marais nilopata kuwaona wenye HURUMA, hekima na busara ni rais wetu wa sasa. Awahurumie hawa mabwana, wameshajifunza kama walikosea

Mnataka watu waliothibitishwa kunajisi na kulawiti waachiwe huru? I am so much against it. First of all imagine hao waathirika wangekuwa watoto wako au ndugu zako. Would you feel the same? Hao mabwana walitumia fedha yao kuwalaghai watoto wadogo. Serikali imewaweka wanakostahili ninyi mnawaonea huruma. Why? Je, hivi mnajua kama wale watoto wameathirika kwa kiasi gani? Hii iwe fundisho hadi hapo walawiti na wabakaji wote watakapotungiwa sheria ya kuwanyonga hadi kufa. Kama kulawiti kuzuri na walawitiane huko waliko. Kwa nini wanataka kutoka? That is where they belong.
 
Bila shaka kuna members wa
JF wapo Mahakama ya Rufaa wakifuatilia hukumu hii ambayo Watanzania
wengi wanaisubiri kwa hamu kubwa kusikia Babu Seya, Papii Kocha wako
huru,

I am +VEly thinking of these men to be FREE. Praise the Lord.

Amen.

--------------

jaman..apa ukwel uko wapi...kama wameonewa watanzania mnaushaidi gani..na wale wanaosema hawajaonewa wanaushaidi gani...naombeni nifafanuliwe apa kidogo tafadhal..na yeyote mwenye uelewa na hii kesi
 
Tunaomba Rais JK atoe msamaha kwa hawa watu kwenye maadimisho ya miaka ya 52 ya Uhuru chini ya kile kifungu cha "the prerogatives of a president". Kwani kwa hali hii hawa jamaa wanaweza sotea gerezani.:(
 
Hakuna ukweli familia ikabaka kuanzia baba mpaka watoto wa chini kabisaa, hizi ni hukumu za kipirato zinazoamuliwa na walio juu ya sheria, chuki binafsi za mapenzi zinazofanywa na wakuu wasio na huruma hata chembe, mwanadamu anageuka kuwa mungu mtu anaamuru fulani afungwe maisha na inakuwa hivyo, dhambi mbaya sana hii kuzima ndoto za mwenzako, na kumpa mateso ya maisha, kama walibaka yule mwalimu aliyekuwa anasemekana alikuwa anapewa hela ya kuwapa wale watoto ili waende kwa babu Seya yu wapi mbona aliachiwa huru? Mwlimu huyu alikuwa akifundisha pale Mbuyuni, inauma sana ukweli tunaujuwa na hawa mahakimu wenye kutekeleza amri za mabwana zao wanaowapa nafasi hizi wamekuwa ni watu wanaotoa hukumu kwa maagizo, shame on u stupid judges, taaluma yenu iko wapi kama mnafanyishwa kazi kwa remort? Kweli usije ukala cha mkubwa. Inauma sana

Wewe ndg yangu unatoka povu bure, kama ungekuwa na ushahidi kama wameonewa si ungeenda mahakamani kupeleka ushahidi! unashangaa baba na watoto kubaka! Hivi hujawahi kusikia baba kazaa/kutembea kimapenzi na mwanaye wa kumzaa????? kama hilo linawezekana, nini kinashindikana kwa babu seya kubaka na mwanaye.?!!! Funguka ndg yangu acha ushabiki wa kijinga
 
Back
Top Bottom