Baba/ Mama taifa ajaye ni yule atakayewapatia wananchi katiba mpya

Mzee wa Twitter

JF-Expert Member
Nov 5, 2023
1,278
2,041
Hakika wakati umefika wa kuambiana ukweli Hayati BABA wa TAIFA Mwl. Nyerere ameifanyia Makubwa Nchi hii kiasi cha LEGACY yake kuendelea kusimama kileleni.

Mwl. Nyerere ameipigania Nchi hii mpaka kupata UHURU wake Tukio ambalo haliwezi kufanywa tena na RAIS mwingine. Mpaka sasa hajatokea RAIS aliyeweza kuwafanyia Watanzania Jambo au TUKIO zito ambalo litakumbukwa na Wananchi Kama wanavyokumbuka Nchi yao Kuwa HURU kupitia Juhudi za MWL. NYERERE.

Marais wengi waliofuata baada ya HAYATI Mwl. NYERERE wamekuwa wakijenga majengo km vile Zahanati Barabara Madaraja ya Juu na Chini vitu ambavyo ni vya kawaida kwa RAIS yeyote anaweza kuvifanya.

Vitu hivyo haviwezi kamwe kuwafanya Wananchi wawakumbuke waliovijenga kwani ni vitu vya kawaida sana kifupi hivyo vitu haviwezi kuwa Legacy ya Mtu.

TUKIO PEKEE kwa sasa ili iwe Kumbukumbu ya kukumbukwa milele ikiwa sambamba na ya UHURU wa NCHI yetu ni KUWAPATIA WANANCHI KATIBA MPYA Mbadala wa KATIBA iliyopo KATIBA iliyopitwa na WAKATI KATIBA iliyojaa VIRAKA KATIBA yenye MAPUNGUFU mengi kwani ina zaidi ya MIAKA 58.

KIU ya WANANCHI kwa sasa ni UPATIKANAJI wa KATIBA MPYA hivyo RAIS atakayeweza kufanya HIVYO hakika Atakumbukwa MILELE Kama ilivyo kwa HAYATI Mwl. NYERERE.

Kitu pekee kinachomfanya Hayati BABA wa TAIFA Akumbukwe sio Barabara wala Hospital au Vyuo ni UHURU wa NCHI.

Mheshiwa Rais Mstaafu kikwete alijaribu kuwapatia WANANCHI KATIBA MPYA lakini hakufanikiwa
RAIS atakayefanikiwa hakika LEGACY yake itakumbukwa Milele. WANANCHI wanataka KATIBA MPYA.

Sent from my SM-A145R using JamiiForums mobile app
 
Katiba mpya ni kabla ya Uchaguzi wowote.

Na haipewi kama peremende au chakula Cha msaada,

Haitokani na hiari ya kiongozi yeyote,

Ni takwa la wananchi Walio bosses wa viongozi.

Amen
 
Katiba mpya ni kabla ya Uchaguzi wowote.

Na haipewi kama peremende au chakula Cha msaada,

Haitokani na hiari ya kiongozi yeyote,

Ni takwa la wananchi Walio bosses wa viongozi.

Amen
Upo sahihi lakini kwa mfumo uliopo bila kiongozi kutaka haipatikani kumbuka Magufuli alisema sio kipau mbele chake Watu walimfanya nini?

Mama badala ya kuendeleza walipoishia tena akiwa Makamu Mwenyekiti wa Bunge la Katiba yeye anataka watu wasomee katiba iliyopo kwanza mmemfanya nini?

Sent from my SM-A145R using JamiiForums mobile app
 
Upo sahihi Mkuu.

KATIBA NDIO NGUZO YA HAKI KWA TAIFA HILI.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Huyu wa Kizimkazi alionesha nia ya kuandika katiba mpya lkn sasa ni rasmi ameikwepa.

Bila kuchapana na kuuana
tusahau kuhusu upatikanaji wa katiba mpya
 
Back
Top Bottom