Baba bora kwenye familia ni yule mwenye sifa zipi?

Kyenju

JF-Expert Member
Jun 16, 2012
4,621
1,706
Habari wanajf, ningependa leo tusaidiane kuzielezea sifa za baba bora ktk familia, mimi nitaelezea kidogo.

Kwanza baba bora ni yule anaye ijali kuipenda na kuitunza familia yake, lakini hii ni kama furushi lenye vitu vingi ambavyo kila kitu kinapaswa kushughulikiwa kwa namna yake.

Ngoja nielezee kipande hiki kinaonekana cha kawaida sana lakini ukikitendea kazi kitakuongezea sifa ya ubaba.

Kufuatana na mila na desturi za makabila mengi baba ndiye anayestahili kula vitu vizuri,
 
Ni yule anayefanya yafuatayo: anailisha familia, anailinda, anaitunza na kuipa upendo
 
Lakini kama baba utaifanya hii iwe kinyume, kwamba mkeo na watoto ndiyo wawe wa kwanza hii italeta mana zaidi.

Tuchukulie mfano wa chakula, acha mkeo na watoto ndiyo wale chakula na mboga nzuri, tena wao wawe ndiyo wa kwanza kujisevia alafu wewe uwe wa mwisho, pia kama chakula kimebaki kabla ya kujiongezea waulize kwanza watoto kama wameshiba, kadhalika mkeo kama hawajashiba wao kwanza ndiyo waongeze kisha wewe uwe wa mwisho. Wakati mwingine chakula kitaisha bila wewe kuongeza, usijali wewe ni baba.
 
... Mleta mada' kama nitakuwa nimekuelewa vizuri, una maana kwamba:
Baba bora ni yule anaye zijali,
kuzipenda, kuzitunza na kuziridhisha familia zake...., kuanzia nyumba kubwa hadi ndogo zote...
 
... Mleta mada' kama nitakuwa nimekuelewa vizuri, una maana kwamba:
Baba bora ni yule anaye zijali,
kuzipenda, kuzitunza na kuziridhisha familia zake...., kuanzia nyumba kubwa hadi ndogo zote...

Maana yangu ni kwamba, awe tayari kuiridhisha familia kwanza kabla yake mwenyewe.
 
baba bora ni yule anaejua watoto wamekula, kuvaa na afya bora, na pia asiye na mpango kando...
 
Ni yule anayejishusha na anahakikisha kila kitu nyumbani kwake kuko sawa, mwenye kuonyesha mifano kwa watoto akishirikiana na mkewe, mwenye kufundisha mengi kwa watoto na hata mkewe na mwenye kujali mawazo ya mkewe na kuyafanyia kazi.
 
1.kugharamia(kutunza)
2.kuongoza
3.kulinda

Kuna baba wengine ukiwaangalia hali zao za kiafya, pia ukaangalia afya ya familia zao utashangaa, maana watoto wamedhoofu lakini baba afya yake ni njema mno, kisa yeye ndiyo mtafutaji.

Mtu kama huyu afai kuitwa baba bora, ila na bora baba.
 
Umefanya nimkumbuke marehemu Baba...
He was real father,a dady...
Simpi Sifa za marehemu ila ni miaka 7 sasa tangu afariki...
Leo nikiwa na malaria thn nipo ndani ya daladala nazurura tu kutokea mjini...
Niseme tu angekuwepo labda ningekuwa nakunywa juice hv na nimepumzika chn ya uangalizi wake kwa cm au moja kwa moja...
Siku ambayo haku2mia gari yake, alinibeba mabegani kunipeleka hospitalini kuchoma sindano za masaa,kwani nimesumbuliwa na Pumu tangu utoto...
Ni yeye ambaye aliniaidi kunipa zawadi kama mingefikia mafanikio flani kielimu na ndivyo alivyofanya...
Sisahau mikwaju na Bakora alizonichapa babangu kila nilipokuwa nakosea,,leo nagundua ni mapenzi mazito aliyokuwa nayo babangu kwangu..
Ndo mana hata leo labda niko hv nilivyo..
Huyu ndo Baba bora kwa sehemu..
RIP DADY..
I miss you..
 
Back
Top Bottom