Baadhi ya Mataifa ya Ulaya na kampuni kubwa yakubali kununua gesi ya Urusi kwa Roubles

MTZ 255Dar

JF-Expert Member
Sep 25, 2018
1,114
3,768
Urusi inasema kwamba haitasambaza tena gesi kwa Poland na Bulgaria kwa sababu nchi zote mbili zilikataa kulipa kwa sarafu yake ya Rouble.

Umoja wa Ulaya umesema kuwa hatua hii ya Urusi ni sawa na hujuma.

Kulingana na ripoti ya Bloomberg, pia kuna nchi ambazo zimekubali matakwa ya Urusi. Hii inaashiria kwamba baadhi ya nchi za Ulaya zinaanza kumlegezea kamba Vladimir Putin.

Nini kimetokea?

Licha ya kuvamia Ukraine, Russia imeendelea kusambaza gesi katika nchi za Ulaya.

Hata hivyo, baada ya nchi za magharibi kuiwekea vikwazo vikali vya kiuchumi Urusi, Putin alitangaza kwamba nchi "zisizo rafiki" zitalipia kwa sarafu ya Urusi zitakaponunua gesi.

Kampuni ya nishati ya serikali ya Urusi ya Gazprom ilisema imekatiza usambazaji wa gesi kwa Poland na Bulgaria na haitarejesha huduma hiyo hadi malipo yafanywe kwa rubles.

Mwenyekiti wa Tume ya Muungano wa Ulaya (EU), Ursula von der Leyen alionya kampuni za Ulaya dhidi ya kutekeleza matakwa ya Urusi kwani zitakuwa zinakiuka vikwazo vya EU.


Nchi nne za Ulaya zimeanza kulipa kwa kutumia sarafu ya rubles

Duru za karibu za kampuni kubwa ya nishati nchini Urusi Gazprom zimeambia Bloomberg kwamba mataifa manne ya Ulaya yameanza kulipa kwa kutumia sarafu ya Rouble sili kusambaziwa gesi kulingana na mahitaji ya rais Putin.

Wakati huohuo mojawapo ya kampuni kubwa za nishati nchini Ujerumani imesema kwamba inajiandaa kununua gesi ya Urusi kwa kutumia mfumo ambao wakosoaji wake wanasema utakiuka vikwazo vya Muungano wa Ulaya.

Uniper imesema kwamba italipa kwa Yuro ambazo zitabadilishwa na kuwa Roubles, na hivyobasi kuafikia mahitaji ya Urusi kwa ununuzi wote wa bidhaa hiyo kufanywa kwa kutumia sarafu hiyo.

Kampuni nyengine za Ulaya zimeripotiwa kujiandaa kufanya hivyo huku kukiwa na wasiwasi kuhusu kukatizwa kwa bidhaa hiyo muhimu.

Uniper imesema kwamba haina chaguo bali kufanya hivyo lakini ikaongezea kwamba bado itaendelea kuheshimu vikwazo vya Muungano wa Ulaya.

Bloomberg ilinukuu duru ikisema kwamba kampuni 10 za Ulaya zimefungua akunti zao katika benki ya Gazprom.

Ni sharti kufungua akaunti hizo ili kuafikia mahitaji ya Urusi.

Ikijibu vikwazo vilivyowekwa na EU, Urusi inataka mataifa ya Ulaya yalipe kwa kutumia Ruble ili kuuziwa gesi hiyo kuanzia tarehe mosi mwezi Aprili.

Lakini lakini wanachama wa Muungano wa Ulaya walikataa kufanya hivyo , wakisema watakiuka vikwazo ilivyowekewa Urusi na nchi za Magharibi.
Je ni kiwango gani cha gasi ambacho Urusi husambaza Ulaya?

Mwaka 2019, asilimia 41 ya jumla ya gesi asilia iliyoagizwa kutoka nje ya EU ilitoka Urusi.

Iwapo usambazaji wa gesi ya Russia kwa Ulaya utasitishwa, basi Italia na Ujerumani ndizo zitaathirika zaidi kwa sababu nchi hizi mbili zinaagiza gesi nyingi zaidi.

Uingereza inaagiza asilimia tano tu ya gesi yake kutoka Urusi na Amerika haiingizi gesi kutoka Urusi hata kidogo.

Akiba ya gesi ya Poland imejaa asilimia 76, lakini Bulgaria ina asilimia 17 tu ya gesi iliyobaki.

Tatizo litatokea majira ya baridi ijayo, kwa hivyo ni muhimu kujaza hifadhi," alisema mchambuzi wa utafiti wa sera ya nishati Simone Tagliapietra.


Mbadala wa gesi ya Urusi nigani?

Bulgaria inasema kuwa inazingatia kuongeza usambazaji wa gesi kutoka Azerbaijan na pia inafanya makubaliano na Uturuki-Ugiriki.

Poland inajenga bomba jipya la kuunganisha hifadhi ya gesi ya Norway, ambayo itajengwa ifikapo Oktoba 2022. Mbali na hayo, nchi hiyo jirani pia inaongeza usambazaji wa gesi kutoka Lithuania.

Naibu waziri wa mambo ya nje wa Poland aliiambia BBC: "Tuna chaguo la kununua gesi kutoka Marekani na washirika wengine, zikiwemo nchi za Ghuba."

Ulaya pia inaweza kwenda kwa wauzaji bidhaa wengine waliopo kama vile Qatar, Algeria au Nigeria, lakini kuna matatizo ya kiutendaji katika kuongeza uzalishaji kwa muda mfupi.

"Ni vigumu kuona chaguzi nyingine za usambazaji wa gesi kwa sababu tuna mabomba haya makubwa yanayoleta gesi kutoka Urusi moja kwa moja hadi Ulaya," mchambuzi wa utafiti Ben McWilliams alisema.

Marekani imekubali kupeleka nyongeza ya mita za ujazo bilioni 15 za gesi asilia ya kimiminika (LNG) hadi Ulaya mwishoni mwa mwaka huu.


Rais wa Marekani Joe Biden

Lengo ni kutoa gesi ya ziada ya mita za ujazo bilioni 50 kila mwaka hadi angalau 2030.

Ulaya pia inaweza kuongeza matumizi ya vyanzo vingine vya nishati, lakini kufanya hivyo kutachukua muda na si rahisi hivyo pia.

"Utekelezaji wa nishati mbadala ni mchakato unaotumia muda mwingi na si suluhu kwa sasa," anasema Tagliapietra.

"Msimu wa baridi unaofuata tunaweza kufanya mabadiliko kwa kufungua mitambo ya kuzalisha umeme kwa kutumia makaa ya mawe, kama Italia na Ujerumani zinavyopanga kufanya katika dharura."

Umoja wa Ulaya umependekeza mpango wa kuondoa mafuta ya Urusi kutoka Ulaya kabla ya 2030 - ikiwa ni pamoja na kubadilisha usambazaji wa gesi na kuchukua nafasi ya gesi katika joto na uzalishaji wa umeme.

Je, upungufu wa mafuta utakabiliwa vipi?

Mtafiti wa sera ya nishati Ben McWilliams anasema ni rahisi kupata chaguo la usambazaji wa mafuta kuliko gesi, kwani mafuta kidogo yanatoka Urusi, "mengine yanatoka sehemu zingine."

Kwa upande mwingine, Amerika inaiomba Saudi Arabia kuongeza uzalishaji wake wa mafuta. Hata hivyo, Saudi Arabia hapo awali ilikataa ombi la Marekani la kutaka kuongeza uzalishaji ili kupunguza bei ya mafuta.

Saudi Arabia ndiyo mzalishaji mkubwa wa mafuta katika OPEC, Shirika la Nchi Zinazotoa Mafuta. Inajulikana kuwa karibu 60% ya biashara ya mafuta ghafi katika ngazi ya kimataifa inafanywa na OPEC.

Jukumu la OPEC katika kupanga bei ya mafuta ni muhimu sana. Kufikia sasa, hakuna mwanachama wa OPEC ambaye amekubali ombi lolote la kuongeza uzalishaji.

Urusi, hata hivyo, sio mwanachama wa OPEC. Lakini ili kuboresha mapato ya wazalishaji wa mafuta, amekuwa akifanya kazi na OPEC tangu 2017 chini ya jina la 'OPEC Plus'.

Marekani pia inazingatia kupunguza vikwazo vya usafirishaji wa mafuta vilivyowekwa kwa Venezuela. Venezuela ilikuwa muuzaji mkubwa wa mafuta kwenda Amerika, lakini sasa inauza mafuta yake kwa kiwango kikubwa kwa Uchina.

Je, ni vikwazo gani kwa mafuta na gesi ya Urusi?

Marekani imetangaza kupiga marufuku kabisa uagizaji wa mafuta, gesi na makaa ya mawe nchini Urusi.

Uingereza itamaliza utegemezi wake kwa mafuta ya Urusi mwishoni mwa mwaka huu na kupunguza uagizaji wa gesi wa EU kwa theluthi mbili.

Urusi ilionya kuwa vikwazo vyake vya mafuta vitakuwa na "matokeo mabaya kwa soko la kimataifa".

Bei ya mafuta na gesi imepanda tangu Urusi ilipovamia Ukraine.

Urusi ni nchi ya tatu kwa uzalishaji duniani baada ya Marekani na Saudi Arabia.

Urusi inauza nje takriban mapipa milioni 5 ya mafuta ghafi kila siku. Kabla ya kutangazwa kwa vikwazo, nusu ya hii ilienda Ulaya.

Takriban asilimia 8 ya mahitaji ya mafuta ya Uingereza yanaagizwa kutoka Urusi.

Utegemezi wa Amerika kwa mafuta ya Urusi ni mdogo. Mnamo 2020, karibu 3% ya mafuta ya Amerika yalikuwa yanatoka Urusi.

Kulingana na IEA, uzalishaji wa mafuta nchini Urusi ulipungua hadi mapipa laki saba kwa siku mwezi wa Aprili.

IEA inasema hadi mwisho wa Aprili, uzalishaji unaweza kufikia mapipa milioni 1.5 kwa siku na ifikapo Mei itakuwa takriban mapipa milioni 3.

Sababu ya hii ni kwamba tangu Machi, wanunuzi wa Ulaya wanatafuta njia mbadala ya Urusi na Marekani pia imepiga marufuku kabisa kuagiza mafuta ya Kirusi.

Urusi sasa italazimika kutafuta masoko mapya ya mafuta yake barani Asia au kwingineko, lakini ikiwa uzalishaji utaendelea kupungua, hatimaye itaathiri uchumi wake.

Nini kitatokea kwa gharama za mafuta?

Kutokana na vita hivi, watumiaji watalazimika kukabiliana na ongezeko la bili za umeme na mafuta. Nchini Uingereza, bei za mafuta zimedhibitiwa kwa kupunguza bei ya mafuta.

Hata hivyo, wakati kikomo cha bei yake inapoongezwa mwezi Aprili, bei ya mafuta itaongezeka kutoka pauni 700 hadi takribani pauni 2,000 mwezi wa Aprili.

Bei zikipandishwa tena katika msimu ujao wa vuli, bei ya mafuta itafikia takriban £3,000.

Bei ya petroli na dizeli pia imeongezeka nchini Uingereza. Sasa serikali imetangaza kupunguza ushuru wa mafuta, kwani wanye magari wanatatizika kumudu bei.

Kulingana na McWilliams, "Nadhani tuko katika ulimwengu ambapo ikiwa mafuta na gesi ya Urusi itaacha kwenda Ulaya, itabidi tugawanye vitu hivi ili tuvitumie."

"Sasa sehemu ya mazungumzo ni ikiwa tunaweza kuuliza watu waweke nyumba zao joto kwa digrii moja," McWilliams alisema.
 
Kuanzia mwaka ujao uchumi wa Russia utakuwa taabani ni vema waanze kujipanga mapema, inaonekana yale yale ya USSR ndio yanarudi.
 
Back
Top Bottom