Elections 2010 Baada ya zanzibar,ni lini slaa ataenda Lindi,Mtwara na Ruvuma?

TUNTEMEKE

JF-Expert Member
Jun 15, 2009
4,587
579
Jamani watanzania wengi wanaitaji kumuona dr slaa..km kuna mtu anajua ratiba ya dr,bas atufahamishe lin ataenda huko lindi,mtwara,ruvuma.najua ruvuma alienda songea na mbinga masharik tu,vp kuhusu mbinga magharibi ambako nasikia chadema inanguvu na vp kuhusu tunduru na Namtumbo..chadema musijidangaye kuwa maeneo haya hayana kura za dr.zipo kura nying sana..shime chadema mpeleken dr maeneo haya.
 
sijaamini kuwa dr.slaa kavuta wazanzibar kiasi kile..........kweli huyu ni mtu wa watu..........kachukue kura zingine huko mwandishi wa thread anakosema kuna kura zetu sis chadema
 
PROF BAREGU mpeleke DR wa ukweli huko kusini kuna mavuno mengi ambayo yatawashangaza. KUNA MKONO WA MUNGU katika mtumishi huyu!
 
sijaamini kuwa dr.slaa kavuta wazanzibar kiasi kile..........kweli huyu ni mtu wa watu..........kachukue kura zingine huko mwandishi wa thread anakosema kuna kura zetu sis chadema

Hivi kumbe mtu ukienda kusikiliza sera unahesabiwa ushampigia kura unaemsikiliza? nilikuwa sijui mwenzenu kweli humu JF kuna ujuzi wa hali ya juu.
 
Tukubali tukatae dr.slaa anatisha , hatumpendi kwasababu ya ushabiki wa kichama bali kwasababu ya utashi mkubwa wa kiasiasa, ucungu alionao juu ya nchi yetu na jinsi anavvyo ji risk kupata data za uchafu unaofanywa na watu wachache waliojinufaisha na kuwafanya watanzania wengine kuwa maskini wa kutupwa
 
Hivi kumbe mtu ukienda kusikiliza sera unahesabiwa ushampigia kura unaemsikiliza? nilikuwa sijui mwenzenu kweli humu JF kuna ujuzi wa hali ya juu.

Kuweza kuwashawishi watu kuhudhuria mkutano wako ni hatua kubwa. SI YA KUBEZA.
 
Kuweza kuwashawishi watu kuhudhuria mkutano wako ni hatua kubwa. SI YA KUBEZA.

Uko sahihi, huoni CCM wanavyohangaika kutafuta watu wa kuhudhuria mikutano ya JK hawawapati hadi wanakodisha watu kutoka sehemu zingine na kuwapakia kwenye malori. Mikutano ya Dr Slaa watu wanaenda wenyewe.
 
Dr. Slaa alishalitolea maelezo kwenye mdahalo wa ITV Jumamosi kwamba anasikitika hataweza kufika katika majimbo yote kwa muda mfupi uliopo wa kufanya kampeni. akasema pamoja na kufanya mikutano hadi 11 kwa siku bado ameweza kufika majimbo yasiyozidi 150 mpaka sasa, na mengine imebidi aahirishe kutokana na tatizo la usafiri, nadhani kwa watu makini watamuelewa kwa kushindwa kufika katika maeneo yao, ala kaahidi kufika hata baada ya uchaguzi.
 
Hata hivyo ameshafika Ruvuma. Tumpigie kura ili afikie Lindi, Mtwara na hata Mafia akiwa Rais wa JMT.
 
Ni kweli wengi tungependa kushauri Dr Slaa ni lazima afanye kila linalowezekana angalau afike mikoa yote kwani kwa kutofika baadhi ya mikoa hii italeta hoja kwa mafisadi kuwa hiki ni chama cha baadhi ya mikoa, bahati mbaya huko ambako hajafika ni kanda (Southrn zone) ambako kama umasikini huko ndo baba yake! Prof. Baregu kazeni buti tufike Lindi, Mtwara na Ruvuma tukachukue kura zetu na kujiweka sawa.
 
Hivi kumbe mtu ukienda kusikiliza sera unahesabiwa ushampigia kura unaemsikiliza? nilikuwa sijui mwenzenu kweli humu JF kuna ujuzi wa hali ya juu.

Sasa yule amabye hapati wasikilizaji unategemea atapataje kura??? Wingi wa watu ni dariri za kukubalika ndiyo maana CCM wanasomba watu na malori ili waonekane wanakubalika.
 
Kwa nini kashindwa kutembelea majimbo yote?
Muda,hela au kukata tamaa kwa baadhi ya majimbo?
 
Ni kweli wengi tungependa kushauri Dr Slaa ni lazima afanye kila linalowezekana angalau afike mikoa yote kwani kwa kutofika baadhi ya mikoa hii italeta hoja kwa mafisadi kuwa hiki ni chama cha baadhi ya mikoa, bahati mbaya huko ambako hajafika ni kanda (Southrn zone) ambako kama umasikini huko ndo baba yake! Prof. Baregu kazeni buti tufike Lindi, Mtwara na Ruvuma tukachukue kura zetu na kujiweka sawa.

Huko kusini hakuna Ukristo. Asilimia kubwa ni aislam na yeye Slaa ametumwa na kanisa.Pole sana Slaa kwa pigo la kukosa watu kule Zanzibar.
 
nakubaliana na mtoa hoja wa kwanza. ni vema slaa aende mikoa hiyo ya kusini.
 
Back
Top Bottom