Baada ya Walimu kutolewa katika zoezi la Sensa Vijana wachukua chao na Kusepa.

Mchokozi

JF-Expert Member
Feb 9, 2012
215
29
Habari nilizozipata na kuzifanyi uchunguzi zinaonyesha kuwa baada ya Walimu walio wengi kuondolewa katika zoezi la Sensa na kuwaweka vijana waliomaliza Chuo na wengine Form sita na St Kayumba wengi wao wamechukua chao na Kusepa na sasa wasimamizi wa wakuu wanahangaika kupigia waalimu walio waacha ili waje kuziba pengo. Ama kweli ile hadithi ya SIZITAKI MBICH HIZI ili hali unazitaka.................Source vituo vya sensa na wasimamizi wakuu.
 
Duh! Kama ni kweli basi hii movie ya Sensa kiboko! Na kule kanda ya kaskazini mkoani Manyara jamii ya Watindiga na Wahadzabe nao wamesema ahesabiwi mtu hapa mpaka wapate kitoweo cha nyama ya PundaMilia ndipo nao watashiriki zoezi la kuhesabiwa! Hii nchi inavituko mpaka tufikie uchaguzi wa 2015 iko shughuli pevu.
 
Zoezi hili wamekosea sana kuwatenga waalimu! Ninakuwa na mashaka sana na anuani na uhakika wa kupatikana kwa baadhi ya hawa watakaoshiriki kuhesabu.

Ninaamini na nitasimamia, wamekosea kuwatoa walimu kwenye zoezi hili, wapo baadhi nina hakika kwa kutokuwa na cha kupoteza kwenye zoezi, wanaweza kufanya wanavyojua ili kupata hiyo posho. Hii inaweza kufanya hata na walimu lakini kupunguza hofu hii wangewachukua wanaodhaminika
 
Nami natafuta sababu nigome bana.mie bila kunilete pweza wakati wanakuja kuhesabu basi makalani watarudia getini.hahahaha.udhaifu ni ugonjwa.
 
Habari nilizozipata na kuzifanyi uchunguzi zinaonyesha kuwa baada ya Walimu walio wengi kuondolewa katika zoezi la Sensa na kuwaweka vijana waliomaliza Chuo na wengine Form sita na St Kayumba wengi wao wamechukua chao na Kusepa na sasa wasimamizi wa wakuu wanahangaika kupigia waalimu walio waacha ili waje kuziba pengo.Ama kweli ile hadithi ya SIZITAKI MBICH HIZI ili hali unazitaka.................Source vituo vya sensa na wasimamizi wakuu.
machozi,hebu niambie,hao walimu wanrespond vipi??na kuhusu malipo,semina inakuwaje???
 
machozi,hebu niambie,hao walimu wanrespond vipi??na kuhusu malipo,semina inakuwaje???

Watajaza data feki na kuziwasilisha, .........nenda kituo cha Tambaza Secondary na Mabibo Secondary kupata japo kwa ufupi
 
Hilo sio la ajabu. Bado tunasubiri zoezi zima likamilike ndipo tathmini ifanyike ili Serikali yetu tukufu itupatie picha halisi ya zoezi zima lilivyofanyika kwa ufanisi ndipo methali ya Usiache mbachao kwa msala upitao tuweze kuifanyia kazi kama ni ya kweli au ni misemo tu ya Wahenga wetu.
 
Habari nilizozipata na kuzifanyi uchunguzi zinaonyesha kuwa baada ya Walimu walio wengi kuondolewa katika zoezi la Sensa na kuwaweka vijana waliomaliza Chuo na wengine Form sita na St Kayumba wengi wao wamechukua chao na Kusepa na sasa wasimamizi wa wakuu wanahangaika kupigia waalimu walio waacha ili waje kuziba pengo.Ama kweli ile hadithi ya SIZITAKI MBICH HIZI ili hali unazitaka.................Source vituo vya sensa na wasimamizi wakuu.

Hao Form VI na St. Kayumba wanajua kwamba Bongo kila kitu ni DILI!

Ama kweli, mdharau mwiba mguu huota tende!
 
hilo sio la ajabu. Bado tunasubiri zoezi zima likamilike ndipo tathmini ifanyike ili serikali yetu tukufu itupatie picha halisi ya zoezi zima lilivyofanyika kwa ufanisi ndipo methali ya usiache mbachao kwa msala upitao tuweze kuifanyia kazi kama ni ya kweli au ni misemo tu ya wahenga wetu.
serikali inayonyemelewa na mauti mipango yake huishia kwenye makaratasi tu.
 
....wenyeviti wa mitaa nao wana mgomo...kisa hawajapitishiwa mgao wa fedha....kaazi kweli kweli
 
unajua hakuna cha Binadamu muhimu kuliko mwingine hawa walimu nao walitaka kutingisha kiberiti Nawahakikishieni hata wagome tena tutaingia madarasani na kufundisha. Huku kwetu zoezi litaenda vizuri tu wao wasubiri kuja kuwauzia watoto wetu bagia na Ice-cream au kuwachotea maji.
Huwezi kugoma wakati shule zenyewe ni za Primary tena za kina Kayumba wakati unanyemelea sensa na Uchaguzi ukikosa ndo unalaumu serikali, MaDr waliwaponza ww ukigoma wenzako wanataka SENSA IPO NA HAITAHARIBIKA HATA WALIMU WASINGEKUWEPO
 
Habari nilizozipata na kuzifanyi uchunguzi zinaonyesha kuwa baada ya Walimu walio wengi kuondolewa katika zoezi la Sensa na kuwaweka vijana waliomaliza Chuo na wengine Form sita na St Kayumba wengi wao wamechukua chao na Kusepa na sasa wasimamizi wa wakuu wanahangaika kupigia waalimu walio waacha ili waje kuziba pengo.Ama kweli ile hadithi ya SIZITAKI MBICH HIZI ili hali unazitaka.................Source vituo vya sensa na wasimamizi wakuu......


...Is this FACT or just What you are Wishing It Should Have been?? If Only Wishes Were Horses.....!
 
Mi mwalimu niliachwa kwenye semina;waambie hao wasimamizi wanitafute no yangu 0987654321,wanipe semina siku moja lakini malipo ya siku saba(245,000/-).Nitafanya hiyo kazi kwa ukamilifu.itabidi wafanye hivyo maana wameshikwa pabaya.
 
Back
Top Bottom