Baada ya ukweli wa Erick Kabendera kubainika, wote walionituhumu kuhusika nimewasamehe kwani Mungu amewasamehe. Msirudie tena!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,513
113,643
Wanabodi,

Kwa vile sisi binadamu tuna uwezo tofauti, na sio watu wengi wanajitambua uwezo wao katika kitu kinachitwa "self realization", ikitokea unajitambua, na unapokasirika kwa kutotendewa haki, kwa kutwishwa misalaba ambayo sio yako, na ukiumia na kulaani watesi wako, na unajua nini kitawatokea pale Mungu anapoamua kukutua msalaba huo, then sauti ya Mungu inakuingia, na hapo hapo unakumbuka na kuwasamehe watesi wako, kabla karma haijaanza kuwafanyia kazi.

Naomba nitoe pole sana kwa mwandishi wa habari za uchunguzi, Erick Kabendera kwa anayopitia, na hayuko peke yake katika hayo, kuna wengi wengine pia wanapita katika mapito kama hayo japo ni kwa njia tofauti tofauti, yote haya ni mapito tuu na kuna siku yatafika mwisho na yatapita.

Toka kukamatwa kwake na polisi na kushikiliwa mahabusu kwa miezi 7, msalaba wa kukamatwa huko nilibebeshwa mimi. Eti ni mimi Pascal Mayalla ndiye niliyesababisha kukamatwa kwa Erick Kabendera, kwasababu ya zile makala zangu za uzalendo humu JF.

Hizi ni Baadhi ya Makala Zangu Kuhusu Uzalendo, wale wenye muda, pitieni halafu mnieleze wapi nimemponza mtu yoyote?






















Japo nilijifanya mgumu na sijali, kwasababu kiukweli kabisa, makala zile wakati zinaandikwa hazikuwa na lengo la kumchomea mtu yoyote, popote, na wala sikuwahi kuwafahamu waandishi wa makala hizo. Na mpaka sasa ninapoandika leo, bado siwafahamu waandishi wowote wa makala hizo, lakini kwa upande mwingine, kwa vile kuna mwandishi wa habari, Erick Kabendera, amekamatwa katika mazingira ya kutatatisha. Baada ya askari waliotumwa kumkamata kukataa kujitambulisha, hivyo kudhaniwa ni wasiojulikana na Erick akawagomea kuwafungulia, ndipo wakamfanyia utekaji kwanza; kwa kutekwa na kufichwa kusikojulikana kwa muda siku mbili za mwanzo, huku serikali wakitupiana mpira, mara ni polisi, mara ni immigration, na kosa lake mara ni uraia ila full kujiuma uma!.

Ila baada ya kufikishwa mahakamani ndipo kukaibuka uhujumu, utakatishaji fedha na magenge ya uhalifu. No one was sure axactly what is it, hivyo any reasonable man lazima ujiulize, "what if ni kweli mwandishi ni yeye?", "what if ni kweli zile makala zangu ndizo zimeiamsha serikali na kuichochea kumtafuta anayeandika?", "what if ni kweli mwanzo alitumiwa wasiojulikana ili wampoteze kama Azory Gwanda na Ben Saanane lakini baada ya Erick kuunguza picha, ndipo ikashindikana, na kuamua kumtafutia mashitaka yoyote ya kumbambikia just to silence him? Then japo nilikuwa najikaza kisabuni, lakini automatically nilianza kujihisi, na kila siku Erick alipokuwa akifikishwa mahakamani naumia, "what if sababu ni mimi?".

Kila uzi wowote kumhusu Erick Kabendera ukipandishwa humu JF lazima humo ndani ya uzi, lazima nilikuwa natajwa as a "snitch". Kila mateso aliyokuwa anakutana nayo Erick Kabendera, na mimi yalikuwa yananiumiza psychologically. Kwanza nikawa sichangii uzi wowote kuhusu jambo lolote kwa Erick Kabendera.

Mimi ni story teller, kwa wapenda nyuzi fupi, ishieni hapa, na kwenda kule kwenye hitimisho, wapenda mastory ya JF, tuendelee hapa
Wakati hayo yakiendelea, mimi nikawa nimepanga safari ya kuelekea Marekani, kumtembelea wife na family, during festive season, "wife wangu na baadhi ya watoto, wanaishi US, yeye ana Green Card, hivyo mimi nina an open multiple US Visa all the time. Ilipotokea Mkuu Max nae anakwenda US kupokea ile CPJ Human Right Award yake, nikampigia simu na kumuahidi kujumuika nae, nikaisogeza safari yangu ili uwiane na CPJ na nikapanga nitahamasisha Watanzania wa pale NY tumsindikize tumfanyie shamra shamra. Siku akirudi Bongo, akutane na surprice media attention pale Airport.

Ile guilt conscious ikaanza kuni hunt "what if sababu ni mimi?". Hapa nilipo tuu, mimi tayari niko blacklisted na "washenzi fulani" eti kuwa simpendi yule "jamaa" kule!, nikajiuliza: What if nitamsindikiza Max US, halafu yule "jamaa" akazidi kufura ?", hivyo Max akiishapokea award yake, huku wakataka kumkabendera?!, kama mimi nilikuwepo, halafu likatokea lolote, who will undestand?.

Max alinihangaikia kupata press accreditation, mimi US Visa yangu ni visitors, huruhusiwi kufanya any work related activity in US, masikini Max, akahangaika hadi nikapata US Media accreditaion na kulipia a working visa, you part with $ 600!. Everything was set, last minute, nampigia simu Max kumwambia siendi, hakuamini, akaniambia kama money related, yuko tayari kuni support all it takes, nikamwambia no! lakini sikumweleza sababu! Sababu ni ku-avoid undue attention! Kama Erick Kabendera ameshikwa kwa sababu ya mabandiko tuu ya JF, what about PPR Camera live from New York?. Nikaacha na kuishia kuhamasisha tuu.

Japo ni wengi humu wanampigania Erick Kabendera, ni wachache wanauguswa na mateso ya Kabendera, hata mimi mpaka nina ndugu zangu wa damu behind bars, lakini sijawahi kutoa machozi kuwalilia, tena kwa sisi wanaume, kuna ile pride ya male chauvinism kuwa wanaume hawalii machozi, lakini amini usiamini, hii video ya mama Kabendera ilinitoa machozi


Baada ya kupokea taarifa ya kifo cha huyu mama, by assumption Erick Kabendera anaonewa hivyo nikamkabili Mkuu

Lakini sasa baada ya Erick Kabendera kuachiwa huru hapo jana, na kuzijua sababu halisi za kukamatwa kwakwe, nimepata releaf kuwa chanzo sio mimi, hivyo sasa nimeutua rasmi msalaba huu, na kuwasamehe, wale wote walionituhumu mimi kuhusika na kukamatwa kwa Erick Kabendera.

Kwa sisi Wakristu, sala kuu ya Kikristo inaitwa sala ya "Baba Yetu", na ndani ya sala hiyo, kuna maneno yasemayo, "Utusamehe makosa yetu, kama sisi tunavyo wasamehe waliotukosea", Ukishamsamehe aliyekusea, hata Mungu anamsamehe, hivyo mmesamehewa ila msirudie tena kuwatuhumu watu kwa hisia tuu kwa vitu ambavyo hamna uhakika navyo!.

Tuhuma dhidi yangu, kumhusu Kabendera, zilianzia hapa
Niombe wasomaji wangu muelewe kuwa sina nia mbaya ninapojaribu kuja na uchambuzi wa namna hii. Lengo langu ni kuoneshana kuwa nchi yetu iko hatarini hasa pale taaluma moja ambayo Taifa linawategemea wanaposigana katika jamii nani anayeumia zaidi!

Nakumbuka siku za hivi karibuni gazeti la the Economist lilikuja na habari ambazo Mkuu Pascal aliziita kuwa ni habari za uongo dhidi ya Rais wetu wa Tanzania.

Gazeti hilo liliwahi kuja na habari kuwa "Rais wa Tanzania hapendi kukosolewa"

Gazeti hilo baada ya kuchapishwa Pascal Mayalla alikuja na bandiko la kupinga habari ile huku akionesha jinsi ambavyo sio kweli Rais wetu anapenda kukosolewa.

Alikwenda mbali zaidi akamnukuu Rais wetu kuwa aliwahi kuwaambia wanahabari kuwa yeye anapenda kukosolewe ila akosolewe kwa Staha na kwa hoja.

Pascal Mayalla kwenye andiko lake anatolea mfano kuwa yeye Pascal Mayalla ni moja ya wanahabari ambao waliwahi kumkosoa Rais na Rais alikubali kukosolewa kwa kumjibu huku akimtania.
Mkuu Hufi Leo, kwanza sikujitokeza kujibu tuhuma hizi kwa kuzipuuzia tuu kuwa kwa vile huu ni uongo na uzushi, uongo mwingine na uzushi ukiuupuuzia tuu utayeyuka na kupita tuu kama upepo hivyo nilipuuza kwa matumaini ni upepo tuu na utapita. Lakini leo baada ya kifo cha mama yake, nimeona nisiendelee kunyamaza hivyo ndio nimejotokeza leo na kukujibu in points format.

Hatua yangu ya kwanza, ni kutuma Salaam maalum kwa rais Magufuli.
Kisha baada ya hapo ndipo nageukia kujibu hoja zako kwa kupangua hoja kwa hoja.

  1. Kwanza lazima watu mjue kuwa andiko la Pascal kupinga habari ya the Economist ndio iliyoamsha watu na kuanza kufuatilia ni nani na yuko wapi anae ripoti habari hizo katika gazeti la the Economist?
  1. Hukuna uthibitisho kuwa ni andiko langu lilipelekea jarida hilo lifuatiliwe, hakuna uthibitisho wowote kuwa sasa jarida hilo linafuatiliwa na hakuna uthibitisho wowote kuwa Eric Kabendera ndie mwandishi wa makala mimi nilizokuwa nazileta humu.
  2. Hapa naomba nieleweke,hata watumishi idara nyeti walianza kufatilia gazeti ilo baada ya kusoma bandiko la Pascal Mayalla hapa JF, na ndipo wakaja kugundua kuwa kumbe mwandishi wa habari zile na nyeti kupitia gazeti lile ni ndugu yetu Erick Kabendera.
    Mimi sina uthibitisho wowote kuwa watu wa Idara nyeti walianza kufuatilia jarida lile baada ya bandiko langu humu jf, lakini kwa vile hata sisi humu jf hatujuani nani ni nani, its good to know that na pia sikuwahi kumjua mwandishi wa makala zile, I'm now learning from you.
  3. Kwanini walifuatilia,kiukweli kilichoandikwa na mwandishi huyo wa habari kilikuwa na ukweli wa 100%ingawa huyu Ndugu Mayalla alikipinga kwa lengo la kujipendekeza kwa msukuma mwemzake.
    Kwenye makala zangu nilikiwa naweka kila cha kweli na cha uongo, niliukubali ukweli na kuupinga uongo na sio kwa lengo la kujipendekeza kwa Msukuma mwenzangu. Kazi ya mwandishi wa habari ni kusema ukweli na kuandika ukweli, mimi ni mkweli, msema kweli na mwandika ukweli bila kujali ukweli huo utamfurahisha nani au kumchukiza nani.
  4. Je, Pascal Mayalla alijua tangu awali kuwa Kabendera ndie anayeandika habari nyeti na kuziripoti The Economist na alishindwa kumuita kama mdogo wake na kumpa onyo?
    Naendelea kusisitiza sikuwahi kumjua mwandishi ni nani, ila hata ningemjua, as long as anachoandika ni kweli, bado nisinge muita mwandishi yoyote kumuonya kwa kazi yake yoyote bali bado ningeendelea kukosoa au na mimi kuandika makala zangu kwenye magazeti yangu ninayoandikia. Hapa nilipo kuna waandishi wengi critical tunafahamiana na kuheshimiana, andiko lolote linajibiwa kwa andiko na sio kwa kuitana.
  5. Kimsingi kifungo cha Kabendera nadhani ni furaha kwa Mayalla kwani alimjua tangu awali na alishindwa kabisa kumuita na kumuonya ingawa wote wanatoka kanda ya ziwa.
    Hii ni personal opinion, kuna watu wenye roho za kishetani ambao wanafurahia binaadamu wenzao wanapopata matatizo, very unfortunately mimi sii miongoni mwa watu wa kundi hili, wanaonijua wananijua na wanaonisoma, wananisoma
  6. Je, Pascal alijua Erick akifungwa tegemezi wake watalia na kusaga meno na wengine watajitokeza mitandaoni wakimlilia kwa kukosa hata fedha ya kununua Dawa?
    Kwavile tangu mwanzo sikujua kama ni Eric Kabendera wala sikujua nini kitatokea, pia hili sikulijua.
  7. Nadhani yote aliyajua ndio maana tangu Kabendera awekwe korokoloni hajawahi jitokeza popote kulaani kukamatwa kwa kijana huyu zaidi inasemekana ndio kwanza anatafuta makala zote zilizoandikwa huko nyuma na kuzisoma na kuzifafanua kwa vijana wa idara nyeti ili kijana azidi kubanwa.
    Hili sii kweli
  8. Andiko la Mayalla dhidi ya kumtetea ndugu yake liko hapa JF linaudhi linaumiza kwani humo ndani anawataja wakosoaji wakubwa wa nchi hii ambao leo hii wamegeuziwa rangi ya unga wa ndere wao wanaita unga mweupe sasa huku wakila kuku kwa mirija.
    Ungeliweka hilo andiko
  9. Nasisitiza waandishi wa habari mtengeni Mayalla na waandishi wote wenye vinasaba vya ukabila na wanaoshindwa kusimamia taaluma badala yake wanaishia kujipendekeza kwa kuhofia uhai wao.
    Waandishi wa habari wenye akili, hawawezi kulifanya hili
  10. Natoa rai kwa Serikali ya Jamhuri kumwachia huru Kabendera. Tusipomdai kwa kiswahili tutawataka kwa kilugha, na hapo ndipo tutakapozuia kiongozi yeyote kuingia mkoa wa Kagera mpaka "omwana weitu mumutaishure."
    Nimeunga mkono rai yako na mimi pia nampa pole sana Erick Kabendera kwa mapito anayopitia.P
Mkuu Sifi Leo, sasa baada Erick kuachiwa, nakuomba kwanza upitie kwa makini hii document hapa chini
View attachment 1368540
View attachment 1368542

Baada ya kuipitia, na kwa vile hakuna yoyote aliyakuwa akijua Erick anashitakiwa kwa kosa gani, baada ya sasa kujua, ni vema ukawa mstaarabu kwanza kwa kuniomba msamaha kwa kunituhumu vitu ambavyo sio vya kweli, na pili ukaanzisha uzi mwingine na kunisafisha.

Kwa vile mimi ni Mzee wa kufundisha somo la Karma humu jukwaani, ukimtuhumu mtu yoyote kwa tuhuma za uongo, kwa kuamini kabisa kuwa anahusika na uovu fulani wakati kiukweli hahusiki, unakuwa exempted na adhabu ya karma kwa sababu wewe unaamini hizo tuhuma ni za ukweli kabisa. Hivyo wakati unapandisha uzi huu, kwa vile wewe Mkuu Sifi Leo, uliamini kabisa na kwa dhati kuwa mimi ndiye niliyemchongea Erick Kabendera, kwa sababu ya mabandiko yangu humu jf, kitu ambacho sii kweli, na kwa vile ulikuwa huujui ukweli by then, karma inakupa exemption kwa sababu uliamini kitu ambacho sii cha kweli ukidhani ni kweli, kwenye karma ukiamini kitu fulani kuwa ni kweli wakati sii kweli, unasamehewa.

Mfano kuna manabii wengi wa uongo, ambao wanamtumikia shetani, wakidhani ni Mungu, na shetani ni kweli anatenda miujiza ya kuponya, kutoa mapepo na kuwapa watu utajiri, "Jina na Yesu", hivyo hayo makanisa kufurika na waumini wakiamini kweli ni Mungu wa ukweli na yanayofanyika ni kwa jina la Yesu. Japo kiukweli hakuna chochote kinachofanyika kwa jina la Yesu, bali ni shetani ibilisi ame pose kama Mungu, na kutumia Jina la Yesu kufanyia miujiza, ila watu waamini, make believe, lakini kiukweli nguvu zinazotumika ni nguvu za giza. Karma inatoa msamaha kwa waumini wote hawa wanaomtumikia shetani kwa kuamini ni Mungu kwasababu wameaminishwa ni Mungu, wakifa, watasamehewa na kuingia peponi, kwasababu they are innocent victims, hawakujua kuwa wanayemuabudu na kumtumia ni shetani!.

Lakini akitokea mtu, akawaambia hayo yanayofanyika sio mafundisho ya Mungu, hivyo wanamtumikia shetani, wakiendelea kuabudu na kusali kwa manabii hao wa uongo, siku ya mwisho, hawatakwepa adhabu ya motoni, hawatasamehewa na watakwenda motoni kwasababu walijua.

Vivyo hivyo na kwako wewe, kwa vile wakati ukinituhumu hapa, you were innocent convinced it was me, na ukaamini, hakuna adhabu ya karma juu yako kwa tuhuma hizi kwangu, ila sasa umeujua ukweli, baada ya kuujua ukweli huu, sasa ni wajibu wako, kunisafisha, baada ya kuujua ukweli huu, usiponishafisha, hapa sasa ndipo adhabu ya karma itakapo kuja kuwa juu yako.

Sisi Wakristu wa kweli, tunaofuata mafundisho ya Mungu wa Kweli, na kufuata mafunzo ya Bwana wetu Yesu Kristo wa Kweli, tumefundishwa kusamehe hata saba mara sabini, hivyo mimi kwa upande wangu, niliisha kusamehe toka siku ile ya kwanza ulipopandisha bandiko hili kwa kulipuuza, kwasababu ulikuwa hujui utendalo. Pia nimewasamehe wale wote walionituhumu ni mimi kwa kuamini kuwa kweli ni mimi.

Hitimisho:
Hivyo kwa uzi huu, baada ya ukweli wa mashitaka ya Erick Kabendera kubainika, mimi nimewasamehe "Wale Wote walionituhumu mimi kuhusika na kukamatwa kwa Erick Kabendera, na kufuatia msamaha huo, pia "Mungu nae, amewasamehe" Hakuna tena adhabu ya karma kwenye kunisingizia mimi issue ya Kabendera, ila tafadhalini sana, msirudie tena kumtuhumu mtu mwingine yoyote kwa tuhuma ambazo hamna hakina nazo! Kauli huwa zinaumba, sisi wengine tunajijua kauli zetu na madhara yake, hivyo mkituudhi tusiposamehe.


Hivyo kwa upande wangu, uwe na amani kabisa, na wote mlionituhumu humu na kungine kote, muwe na amani, nimekusamahe na kuwasamehe wengine wote kwa roho safi na roho nyeupe, lakini ili karma isikushughulikie na wewe kwa upande wako, baada ya kuujua ukweli huu, do the right thing, hata kimoyo moyo tu, inatosha Mungu anasikia kila kitu hata usipozungumza, ile kuwaza tuu, is enough!

Ubarikiwe sana.

Paskali.
 
Wewe unapendeza sana ukiwa unaandika makala zako zile et za uzalendo, hapa unapojitetea kwangu mimi hata sijakuelewa, najua wewe ni Mwanahabari na pia ni Mwanasheria so kukwepa kwepa kwako ni raisi sana.

Si unajua ni Mungu tu anayejua yote?

Basi sisi tumekusamehe.

Ila kama kweli ulikuwa unajua unafanya nini tena kwa unafiki na kama bado umeleta uzi huu kinafiki. Hakika adhabu ya Mwenyezi Mungu iwe juu ya kichwa chako.
 
Pascal Mayalla,

P nimekusoma vyema ila naomba nisikuunge mkono katika hili mnililo ku quote hapa. Usidhani kuachiwa kwa Kabendera ndo waraka wa kuziondoa tuhuma zako.

Let me declare interest. Mimi ni shabiki/follower wa Pascal Mayalla kindakindaki. Hivyo basi naomba nikuambia P kuwa, kuachiliwa kwa EK sio kukufutia tuhuma. Kuachiwa kwake hakumaanishi ati ni kweli alifanya hayo makosa. Mwenye kujua kosa liko wapi ni mmoja tu au wawili. Aliyemkamata au aliyeitengeneza hiyo scenario. Hivyo, usikimbilie kujikosha. Tulia, wale wale waliokutuhumu wakuoshe wao wao.

Usituambie kuwa yale maneno ya EK ndiyo kweli yenyewe. Tumuachie yeye asiyefichwa kitu aamue. What I know is; Nothing is going to remain secret for ever. A day will come when the wall is going to tell the roof what happened in that room and the roof will tell the sky this truth and as we look up, all will see for themselves what happened that day and there will be no more secrets
 
EK kakiri makosa ya kubambikiwa na kesi ilikuwa ni fake hata wewe unajua. Waliokutuhumu kumchomea EK utambi hawajathibitishwa kuwa waongo bali EK alikiri makosa kununua uhuru wake.

Wale ambao hatukuamini kuwa una mkono kwenye hili saga sasa, kwa bandiko hili tunaanza kufikiri vinginevyo. Mara nyingine Pasco, kimya kinatunza heshima na ‘kuficha’ makosa!


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Bado hujakwepa karma,damu ya mama Kabendera iko juu yako na waliohusika kumbambikizia kesi Kabendera!Ili tukusamehe,nenda kamuombe msamaha kabendera na mpige picha na ulete hapa JF hiyo toba yako!

Lakini kuja hapa na kurahisisha tu kisa Eric kakiri basi ana hatia ya hayo makosa aliyoshtakiwa nayo ni aina nyingine ya kukwepa kuwajibika kwako!
 
Back
Top Bottom