mahololelo
Member
- Oct 11, 2011
- 32
- 5
Wadau nawarudisha nyuma kidogo turejee kwenye hoja ya fao lakujitoa ambalo Serikali imeamua kuliondoa miongoni mwa mafao yanayotolewa na mifuko ya hifadhi ya jamii, mijadala mbalimbali ilifanywa na washikadau lakini mpaka sasa hakuna taarifa njema kwa sisi wahanga juu ya fao la kujitoa.
Mapendekezo ya serikali ni kuanzisha fao la kukosa ajira ambalo malipo yake hayana tija kwa wafanyakazi wanaotoka kwenye sekta zisizo na ajira ya kudumu au ajira za mikataba ya muda mfupi, hivyo basi rai yangu ni kwa wale wote ambao tunaona umuhimu wa fao hili kiuchumi baada ya ajira kukoma tutumie uzi huu kumuomba Mh.Rais,Dkt J.P.Magufuli atuangalie kwa jicho la pili ili tuweze kujiajiri pindi ajira zinapokwisha.
Ninayo imani kuwa mh.rais atatusikia na kutufanya tuendelee kuwa walipa kodi kwa maendeleo ya Taifa.naomba kuwasilisha