Baada ya Rais kuzungumza juu ya Dowans, Mjadala Ufungwe?

Albert Msando

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
1,019
171
WanaJF,

Sina mamlaka ya kuzuia mtu au chombo chochote kuzungumzia Dowans. Lakini nimeshawishika kujaribu kuweka jamvini kauli za watu/viongozi na vyombo mbalimbali kuhusu suala la DOWANS. Zimetolewa kauli nyingi kiasi kwamba yote tunayochangia yamekuwa yakijirudia bila kutusaidia kufika mahali tukakubaliana nini cha kufanya. Natambua ni vigumu kufikia muafaka wa nini cha kufanya ili hakuna ugumu kuona ni wapi nguvu zetu zinapotea bure! Si vigumu kung'amua usanii unaoendelea na sisi tunabaki kuwa watazamaji!!

Hawa ni baadhi ya waliozungumzia DOWANS pamoja na vyombo mbalimbali;

1. Mh. Werema - Mwanasheria Mkuu wa Serikali - Walipwe hakuna jinsi ya kukwepa kulipa

2. Mh. Pinda - walipwe, tuheshimu maamuzi ya ICC

3. Mh. Wassira - Raisi asilazimishwe kuongelea Dowans

4. Mh. Mwakyembe - kesi ya Dowans mwanafunzi wa mwaka wa kwanza sheria angeshinda.

5. Mh. Sitta - DOWANS ni genge la wahuni watatu.

6. Mh. Ngeleja - walipwe hatuna jinsi ya kuwepa. Tumeshauriwa na Rex Attorneys tulipe.

7. Mh. Nkulo - Tanesco ilipe Hazina haina fedha

8. Kamati Kuu ya CCM - Kulipa ni uungwana

9. Baraza la mawaziri - kimya!!

10. UVCCM - serikali isilipe Dowans

11. Mh. Mkono - nitasaidia angalau deni lipungue au lisilipwe.

12. Mheshimiwa Jakaya Kikwete - tumewaachia wanasheria wa TANESCO na Serikali.

13. Mh. Malima - tusilipe

14. Wakili Fungamtama - tulipe

15. Msajili Mahakama Kuu - wanaweza wakakubaliana kulipana nje ya mahakama

16. Kamati ya Wabunge wa CCM - Dowans isilipwe. Kuna Mbunge ndiye mmiliki!

Hao ni baadhi ya ambao nawakumbuka kwamba walitoa maoni/mapendekezo/mawazo yao kuhusu malipo ya Dowans!! Kama kuna kauli ambayo nimeisahau au sijaiweka vizuri tafadhali changia ili kuboresha!

WanaJF, je kauli ya Mheshimiwa Jakaya Kikwete ni mpya au ngeni? Je kauli yake ya leo inafuta kauli nyingine zote zilizowahi kutolewa hapo awali? Tunatakiwa tuichukuliaje kauli hii ya Mheshimiwa Jakaya Kikwete?

Tukumbushane yafuatayo;

1. Mheshimiwa Jakaya Kikwete ndiye aliyekuwa Mwenyekiti ya Kamati Kuu ya CCM na ndiye alieyongoza kikao cha kamati ya wabunge wa ccm kama sikosei. Vyombo hivyo viwili vilitoa misimamo tofauti!!

2. Mheshimiwa Jakaya Kikwete ndiye aliyewateua wengi wa waliotoa matamko ya kuchanganya hapo juu.

3. Mwanasheria Mkuu wa Serikali alishasema tulipe sasa hivi ameachiwa hilo suala pamoja na wanasheria wa tanesco ambao ndio walioshindwa kesi hiyo hiyo!

WanaJF, mwananchi wa kawaida ashike lipi aache lipi? Tunawasaidiaje? Humu jamvini kuna thread kibao za Dowans. Tumetoa hasira zetu zetu humo, tumetukana, tumelaumu, tumeshutumu nk. mwisho, halafu ikawaje?

Mheshimiwa Jakaya Kikwete amesema, suala hilo liko mikononi mwa wanasheria wa serikali na tanesco!!

Saa tuanzie kujadili hapo! Vinginevyo itabaki hadithi aliyotufundisha babu!!
 
Back
Top Bottom