Elections 2015 Baada ya Pinda kutangaza nia, Membe afunguka

uukiondoa siasa za kuchafuna, Membe anafaa sana kuongoza hii nchi. Jamaa yupo poa sa


==> Ur mentally dwarfed like Membe...ur IQ is too low
just to see the REALITY...

👊👙 Hafai, hata kidogo, let me be as clear as possible...hakuna mtu MUONGO sana, MNAFIKI, na mwenye KUONA ALL PEOPLE ARE STUPID BUT ONLY HIMSELF KNOWS THE BEST...kumbe yy ndio hajui chochote....HE IS NOT PRESIDENTIAL MATERIAL AT ALL...he SOUNDS to local & Nasty..!! Mkurupukaji sana huyo...

Huoni hapo kaulizwa kiswali tu..Kuwa wajumbe wa CCM wamepokea rushwa ili yeye asichaguliwe..hivyo si chama cha RUSHWA...cheki alivyo jibu...HYPOCRITE ni mbaya sana...!!
 
Hawa marais ambao Membe anadai wamekuwa connected na dunia kutokana kuongoza wizara kwa mambo ya nje ndio wanaotuchafulia nchi, mfano mzuri ni JK ameshindwa kupunguza umaskini, uchumi wa Tz umezidi kuporomoka, saraf ya Tz ndo ivyo tena, ajira imekuwa kama ndoto lakini ukimtathmini JK na safari za nje tokea amekuwa rais utagundua ni rais wa kwanza ulimwenguni anayeongoza kupanda ndege kwenda huko duniani lakini wananchi wake njaa na umaskini umekithiri hata mlo 1 kwa siku ni shida kwa watanzania walio wengi.

Ni bora kabisa mara hii kupata rais asiye na harufu za mambo ya nje kama Membe ni yale yale tu. Na ukweli ni kwamba huyu Membe inavyoonekana tayari wanataka kurithishana urais na JK labda kuna makato huko watakuwa wanapeyana sasa hii pia haikubaliki.
 
Nukuu muhimu
1-
"Nilikuwa ni mjumbe pekee niliyepigwa vita na makundi yote. Mabilioni ya pesa yalichangwa na kuagiza wajumbe wasimchague Membe. Mlishuhudia jinsi kina (jina tunalihifadhi walivyonitukana, lakini kati ya wajumbe 2011, nilipata kura 1,455 na kushika nafasi ya sita."


2- ("Hapa akimsema PM...")
"Chama chetu sasa kiwe na utaratibu utakaowabana watu fulani wasigombee kutokana na nyadhifa zao. Kama uko kwenye nafasi ya kufanya uamuzi, unawaadhibu hawa, halafu unajitokeza kugombea, kunakuwa hakuna objectivity (hali ya kutotenda haki)"

Uamuzi wa Kamati Kuu ya CCM wa kuwadhibiti kwa mwaka mmoja makada wake sita waliobainika kukiuka kanuni kwa kuanza mapema kampeni za urais, unaweza kuwa uliwakera wengi, lakini si Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe, ambaye ni mmoja wa ‘waliofungwa kufuli'.

Membe anaona adhabu hiyo ilikuwa mwafaka na kwamba laiti uamuzi huo usingefanywa mapema, "ingekuwa vurugu tupu".
"Sijui nchi hii ingekuwa wapi kama watu wangeachwa bila ya kuwekewa ‘gavana'," alisema Waziri Membe kwenye mahojiano maalumu na gazeti hili yaliyofanyika kwenye ofisi za wizara hiyo jijini Dar es Salaam wiki iliyopita.

Membe pamoja na makada wengine, Frederick Sumaye, Edward Lowassa, William Ngeleja, Stephen Wasira na January Makamba walibainika kukiuka kanuni za uongozi na maadili za CCM kwa kuanza kampeni za kutafuta kuteuliwa na CCM kugombea urais.

Kwa mujibu wa taarifa ya CCM iliyotolewa baada ya kikao cha Kamati Kuu, makada hao walikiuka kanuni za uongozi na maadili za CCM kwa mujibu wa Toleo la Februari 2010 Ibara 6 (7) kwa baadhi yao kufanya vitendo vinavyokiuka maadili ndani ya jamii.

Bila ya kueleza ni jinsi gani vurugu hizo zingefanyika, Membe alisisitiza kuwa vurugu ingekuwa kubwa kama chama hicho kisingechukua hatua mapema.

"We angalia, kuna makundi mawili. Hili kundi letu (la walioanza kampeni mapema wakaadhibiwa) na hili jipya la hawa ambao wameanza kujitokeza sasa, ingawa najua nao watadhibitiwa tu. Hawa wasingedhibitiwa, ingekuwaje?" alihoji Membe.

Wakati CCM inawaita makada hao kwa ajili ya kuwahoji, tayari baadhi walishaanza kufanya sherehe na kualika wenyeviti wa mikoa ambao walieleza misimamo yao juu ya mgombea urais wanayemuunga mkono, wengine kuzunguka kwenye hafla mbalimbali kwa ajili ya harambee na wengine kuzigawa jumuiya za chama hicho, hasa Umoja wa Vijana (UVCCM), huku baadhi ya vikao vikiripotiwa kutawaliwa na malumbano yaliyosababishwa na misimamo tofauti kuhusu mgombea urais wa CCM.

Hata hivyo, Waziri Membe (61) hakusita kukosoa muundo wa vyombo vya uamuzi vya CCM ambao unawapa fursa baadhi kushiriki katika kuadhibu wanaotaka nafasi fulani na baadaye walioadhibu kujitokeza kuwania nafasi hiyo akisema utaratibu huo unawaonea wale ambao hawana fursa ya kuwadhibiti wengine.

"Chama chetu sasa kiwe na utaratibu unaowabana watu fulani kugombea kutokana na nyadhifa zao. Kwa mfano, uko kwenye nafasi ya kufanya uamuzi, unawaadhibu hawa halafu baadaye unajitokeza wewe. Huwezi kuchuja halafu ukajitokeza wewe (kugombea). Kutakuwa hakuna objectivity (haki)," alisema bila ya kuweka bayana watu waliohusika katika kuadhibu na baadaye wakajitokeza kuwania urais.

"Tuwe na utaratibu kwenye chama kwamba wanaowabana watu fulani, wasigombee na hasa wale walioshiriki uamuzi ule na wengine walioko kwenye nafasi za uamuzi… Kamati Kuu na hata (Halmashauri Kuu) Nec na Kamati ya Maadili, nao wasije kujitokeza baadaye na kutangaza nia. Vinginevyo hatutawaelewa," alisema.

Pamoja na kusifu kitendo cha Kamati Kuu kudhibiti makada mapema, Membe anaona muda umefika kwa CCM kuruhusu wanachama wake wanaowania urais waanze harakati zao sasa.

"Huu ndiyo msimu wenyewe," anasema Membe ambaye alizungukwa na wasaidizi wake wakati wa mahojiano hayo.
"Kinachotakiwa sasa ni chama kitoe guidelines (miongozo) kwa wagombea. Kiseme wanapaswa kufanya moja, mbili, tatu…. Chama kiruhusu, lakini wagombea wasivuke mipaka hiyo iliyowekwa."

Kuhusu ndoto yake

Waziri Membe, ambaye alikuwa makini kutotamka waziwazi uamuzi wake wa kugombea urais mwakani, alisema amekuwa na ndoto siku nyingi na alianza kuipima ndoto yake hiyo katika uchaguzi wa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM mwaka 2012 alipogombea nafasi hiyo kupitia kundi aliloliita "la kifo".

"Ningeweza kuingia Nec kupitia nafasi ya wilaya ambako kwa vyovyote sikuwa na mpinzani. Lakini niliamua kwa makusudi kupima kukubalika kwangu ndani ya CCM. Katika kujipima huko, nikaamua kugombea nafasi hiyo katika ngazi ya taifa. Sasa kuna watu waliojua ndoto yangu na wakataka kunidhibiti. Wakatumia mabilioni kuniharibia ili kuhakikisha sipiti. Waliamini kwamba ningeangushwa, nisingeweza kurudi tena hapo kuomba nipitishwe," alisema Membe.

"Kwangu ilikuwa ni vita kuu... nilikuwa kwenye kundi la kifo. Sikufanya kampeni, sikutumia hela wala ushawishi wowote, lakini niliwashinda watu 26. Katika kundi lile (la watu 32), mimi ni mgombea pekee ambaye si mjumbe wa sekretarieti na wala sikuwa mjumbe wa Kamati Kuu. Sikwenda mikoani kutafuta kura wala sikutoa chochote."

Membe anaongeza kusema: "Nilitaka kupima kama uadilifu wangu ungeweza kunipa nafasi ya uongozi ndani ya chama. Nilikuwa mjumbe pekee aliyepigwa vita kali na makundi yote. Mabilioni ya fedha yalichangwa na wajumbe kuagizwa wasimchague Membe. Mlishuhudia jinsi kina (jina tunahifadhi) walivyonitukana, lakini nikashika nafasi ya sita. Kati ya kura 2011, nilipata kura 1,455 sawa na asilimia 77."

Alipoulizwa haoni kama mabilioni hayo ya fedha yaliyochangwa kwa ajili ya kuhonga wajumbe, yanadhihirisha kwamba chama hicho kimetawaliwa na rushwa, Membe alikuwa nadhifu katika kuisafisha CCM.

"Mkutano mkuu uliondokana na kashfa ya rushwa kwa ajili yangu. Ni fact (ukweli) kwamba wale watu waligawa rushwa, wajumbe walichukua wakatafuna, lakini hawaku - comply (hawakufuata masharti ya watoaji rushwa)," alisema.

Makundi ya urais

Kila wakati uchaguzi mkuu unapokaribia, CCM hugawanyika katika makundi kulingana na mtazamo wao kwa wagombea urais kwa tiketi ya chama hicho, kiasi cha kutishia kusambaratika. Hali hiyo huwafanya baadhi kuona kuwa ni bora mgombea asiye na makundi ndiye apitishwe kukinusuru chama kusambaratika. Lakini Membe ana mtazamo tofauti.

"Asiwadanganye mtu. Hakuna mgombea urais duniani asiyekuwa na makundi na akitokea mgombea huyo (asiye na makundi), basi ni dhaifu. Kuwa na makundi ni potision (msimamo). Makundi katika uchaguzi ni muhimu kwa kuwa yanamtofautisha mgombea mmoja na wengine. Kimsingi, makundi ndiyo msimamo wa mgombea.

"Mfano kama ni suala la ushoga, uko wapi; kama ni ufisadi, uko kwenye kundi gani. Huwezi kuwa katikati. Ukiwa katikati maana yake ni kwamba nusu unaunga mkono ushoga na nusu hauutaki. Utakuwa hueleweki.

"Kama kuna mambo huyataki, hayo ndiyo yanayo - define (yanayoelezea) kundi lako. Mfano kama (Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Joseph) Warioba anataka serikali tatu na mimi nataka serikali mbili, haya ndiyo makundi yetu. Wote ni CCM, lakini tuna makundi tofauti."

Sifa za urais

Kuhusu mtazamo wake juu ya sifa za mgombea, Waziri Membe alisema urais ni taasisi nyeti mno watu kuigombea. "Mtu huwezi kusema nagombea urais ili nitekeleze ilani ya chama. Lazima uwe na mambo ya msingi kabisa ya kuwaambia watu kwa nini unataka urais. Huwezi kugombea urais eti kwa sababu una hela za kuwapa watu ili wakuchague," alisema.

"Tunaweza kuweka sifa 100 au hata 300 za urais, lakini sifa za msingi kabisa za kiongozi huyo ni uchapakazi wake hapo alipo na siyo zamani. Pia tunaangalia uadilifu wake na anachotaka kutufanyia Watanzania. Mgombea urais lazima uende beyond (mbali na) ilani ya chama. Hata mbunge na diwani hutekeleza ilani ya chama! Sasa kwani ni lazima utekeleze ilani ya chama ukiwa Ikulu? Lazima ueleze utafanya nini.

Atagombea urais mwakani?

Membe amesema ana ndoto ambayo bado anaitafakari kuona maana yake. "Ndoto ziko za aina mbili; ile ya mtu kulala akaota na ikabainika kuwa ya kweli na ndoto ambayo ni people driven (inayotokana na maoni ya watu).

Akifafanua alisema, ndoto inayotokana na ushabiki wa watu ni ya kujipima na katika siasa mtu hawezi kujipima mwenyewe. Unahitaji timu kwa ajili ya utafiti wa uwezo wako na changamoto unazoweza kukumbana nazo katika hiyo ndoto, alisema.

"Hata wakati unapopata ushauri wa watu hao, bado haujaoteshwa. Ni process (mchakato). Hukurupuki tu. Huwezi kusema unataka, halafu uje uharibu nchi ya watu. Si suala la haki ya kikatiba. Mtu unaulizwa kwa nini unagombea, unajibu ‘ni haki yangu ya kikatiba'. Ah! Wewe mpuuzi? Ni lazima upate watu wa kukushabikia.

"Nchi ya watu milioni 45, ina watu wengi wenye akili sana, hivyo lazima ujiulize ‘why me? ( kwa nini mimi?)Wewe una nini zaidi mpaka uitake nafasi hiyo. Kusubiri kuoteshwa ni pale wenzako wa kweli wanaposema wamepima kukubalika kwako."

Alipoulizwa kama tayari ameshaunda timu inayofuatilia na kuchunguza ndoto yake hiyo alijibu, "Ipo na nadhani mwezi ujao itaniletea majibu".

Waziri Membe tayari ametangaza kutogombea tena ubunge katika Jimbo la Mtama mwaka 2015 na alipoulizwa anapanga kufanya nini baada ya hapo alijibu: "Tofauti na wengine, kwangu ubunge siyo kazi ya kudumu. Nilishawaambia kwamba sitagombea tena na nimewapa ruksa watu kuanza kujipitisha jimboni kwangu, sina tatizo nao."

Waziri wa Mambo ya Nje na urais

Kwa miongo miwili, watu walioshika nafasi ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, ndiyo waliopitishwa kugombea urais kwa tiketi ya CCM na wakashinda. Benjamin Mkapa alishika wizara hiyo kabla ya mwaka 1995 kuwa Rais na baadaye mrithi wake, Jakaya Kikwete alishika wizara hiyo kwa miaka 10 na sasa ni Rais.

Hata hivyo, Membe hadhani kama kushika nafasi hiyo ni kujihakikishia urais... "Siyo ajabu Waziri wa Mambo ya Nje akashindwa urais, lakini marais wengi sana duniani wametokana na nafasi ya uwaziri wa mambo ya nje. Kama nilivyowaambia, mimi ni waziri wa 13 kushika wizara hii, lakini si wote wamekuwa marais."

Hata hivyo, alisema waziri anayeshika wizara hiyo ana sifa za ziada kutokana na ukweli kuwa anakuwa na uzoefu katika masuala ya uongozi na itifaki katika ngazi ya kimataifa.

"Sifa ya kiongozi wa nchi ni kuwa connected to the world (kuwa umeunganishwa na dunia). Smart people (watu makini) hawachagui kiongozi ambaye hayuko connected," alisema na kuongeza kuwa kutokana na kuongoza wizara hiyo anakutana na viongozi mbalimbali duniani, wawekezaji, wafanyabiashara na kufahamu kwa kina masuala ya ushirikiano.

"Rais huendi kujitambulisha kwa wenzako, lazima uwe unajua baadhi ya mambo. Haiwezekani wewe kila kitu unajifunzia Ikulu, kuapisha viongozi, kusoma hotuba, kukaribisha wageni ujifunze kwenye kipindi chako cha uongozi. Sasa hizo ndizo kazi za kila siku za waziri wa mambo ya nje," alisema.

"Kazi zangu zote mimi (Wizara ya Mambo ya Nje) ni maagizo ya Rais na wizara hii ni idara ya Rais. Ni mkono wa Rais, hivyo ukiwa hapa una picha nzuri ya uongozi wa nchi. Lakini kama nilivyosema hata hivyo, siyo automatic (moja kwa moja), chama kinapaswa kukuchagua na watu wakukubali."



cc: pasco
Mytake:
Huyu mtu ana uwezo mkubwa sana,
ingawa wapo wengi wenye sifa, lakini kiukweli simuoni mtu mwingine CCM anayemkaribia huyu mtu.

sosi: Kizitto Noya mwananchi.co.tz.



Hawa marais ambao Membe anadai wamekuwa connected na dunia kutokana kuongoza wizara kwa mambo ya nje ndio wanaotuchafulia nchi, mfano mzuri ni JK ameshindwa kupunguza umaskini, uchumi wa Tz umezidi kuporomoka, saraf ya Tz ndo ivyo tena, ajira imekuwa kama ndoto lakini ukimtathmini JK na safari za nje tokea amekuwa rais utagundua ni rais wa kwanza ulimwenguni anayeongoza kupanda ndege kwenda huko duniani lakini wananchi wake njaa na umaskini umekithiri hata mlo 1 kwa siku ni shida kwa watanzania walio wengi.

Ni bora kabisa mara hii kupata rais asiye na harufu za mambo ya nje kama Membe ni yale yale tu. Na ukweli ni kwamba huyu Membe inavyoonekana tayari wanataka kurithishana urais na JK labda kuna makato huko watakuwa wanapeyana sasa hii pia haikubaliki.
 
[Sio kuleta fikira za jaha, eleza ni sifa zipi alizonazo zinazokufanya umkubali kufaa kuwa rais. Mambo ya kusema 'moyo wangu tu unampenda' hayawezi kukubalika. Mimi nampenda Peter Kayanza Pinda kutokana na sifa zifuatazo: Aliweza kuongoza wizara ya serikali za Mitaa na Tawala za mikoa katika kipindi cha wamu ya Tatu. Boss wake wa awamu ya Tatu alidelegate kazi. His hands were off, his eyes on. Huyu Boss wake wa sasa mswahili, anasema hiki anafanya kile. Hajiamini. Anafanya kazi ya kuviziana na hataki mawazo tofauti. Hamtaki mtu anayeweza kum overshine. Ni kiongozi mwenye huruma kwa wanyonge. Kitendo cha kutoa machozi mbele ya Bunge ni in depth feeling kwa wahanga wa mauji ya kikatili ya Albino. Hata Rais Bill Clinton alimwaga machozi uwanja wa ndege alipokuwa akipokea maiti za Wamarekani waliouwawa kwenye mashabulizi ya balozi za Marekani Dar es Salaam na Nairobi mwaka 1998. Viongozi wasioweza kuonyesha hisia za uchungu hata watu wakifa sio majasiri bali wana mioyo ya kikatili. Hisia za huruma au za kikatili hazifichiki. Pinda ni mkweli. Aliposema 'Zanzibar sio nchi' alisema kile kinachoelezwa kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa maneno mengine alikuwa anailinda Katiba aliyoapa kuilinda mbele ya Raisi aliyemteua. Jambo hili JK ameshindwa kutekeleza. Pinda ni shupavu kuliko JK mara 100.QUOTE=Tume ya Katiba;10485355]Subiri ndugu yangu utaona, Membe ana sifa zote za kuwa rais na ndiye anayetufaa kwa sasa.
[/QUOTE]
Nimekukubali sana,Membe hawezi kulingana hata kidogo kwa sifa nzuri alizonazo PINDA, Pinda anauwezo mkubwa sana kumzidi hyo Membe na ndio maana JK anamkubali sana PINDA zaidi ya MEMBE
 
Katika uongozi wa sasa, aina ya kiongozi wa kumrithi JK naona bado sijaona anayefaa coz we will need someone who can do a real transformation of how we work.. JK tried but we need someone to take it to the next level..Sasa kwa Membe bado sana!!!


Yes mkuu, LIKE EVERY OTHER CANDIDATE, WE EXPECT MORE THAN POLITICS FROM HIM. WE EXPECT A COMPLETE ROAD-MAP OF HOW WE GONNA REACH THE NEXT LEVEL FROM ALL CANDIDATES!
THE WORLD IS CHANGING EXPONENTIALLY AND SO MUST OUR NATIONAL LEADERSHIP!

 
Huyu nayee mropokaji tu!!

Kuna mtu humu kasema eti "...jamaa yupo poa sana" 2005 vijana woooooote walimshobokea JK! Matokeo yake ni setbacks and disappointments tu!!!
 
Hivi wahariri wa mwananchi (kwenye picha wanaonekana wanne inawezekana walikuwa zaidi) hawakuwa na kazi nyingine wagawane majukumu maswali yao wampe mmoja akamhoji? Na huo muda kulikuwa hakuna kazi wizarani hadi waziri anatumia ofisi kuongelea mambo yenye maudhui ya kichama?
 
MAELEZO YA MGOMBEA WA BAVICHA TAIFA FRANCIS BONIFACE MARWA

UTANGULIZI

Ndugu zangu watanzania, awali ya yote niwashukuru sana, ninyi nyote mtakaobahatika kukutana na huu ujumbe wangu mahususi ndani ya mitandao hii ya Kijamii, magazetini ama kupitia chombo kingine chochote kile cha habari ambacho nitaweza kumudu gharama zake ili kuifanikisha azma hii ya kuwafikishieni ujumbe wangu, juu ya nini hasa kimenisukuma kuingia katika kinyang'anyiro hiki cha kuiwania nafasi ya "Mratibu wa Hamasa" BAVICHA ngazi ya Taifa.

Natambua macho yote ya watanzania ndani ya mipaka ya Taifa letu, yameelekezwa kwenye chaguzi za Chama chetu zinazoendelea Nchini kote hivi sasa, ama wapo wanaozitakia mema, na wapo wanaozitakia shari, ili kesho wapate jambo la kuupotoshea umma, kupitia majukwaani, na vijiwe vyao vya kahawa, uji, Draft na Pool table.

Kutokana na hayo yote, na mengine mengi zaidi, ndio sababu wengi wetu hususani sisi vijana, tumechukua maamuzi magumu ya kuomba nafasi za uongozi ndani ya Taasisi hii pendwa kuliko zote Nchini, ili tupate fursa za kuitetea na kuilinda kama mboni ya Jicho.

Baraza letu la Vijana (BAVICHA), ni moyo wa Chama hiki, na hii ndio sababu, upo ulazima wa kuijenga na kuiimarisha BAVICHA na iwe imara, yenye misimamo isiyoyumbishwa na dola, tena yenye maamuzi magumu kwa maslahi ya Chama na wazalendo wa Taifa hili kwa ujumla wao, ambao ndio walipa kodi.

NIMEFANYA NINI NDANI YA CHAMA

Nimeichukua rasmi Kadi ya Chama mwaka 2001 huko kwetu Serengeti Mara, mwishoni mwa mwaka 2009 kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa nikiwa Shuleni Kidato cha Pili, nikachaguliwa kuwa Katibu Mwenezi wa Chama ndani ya Kata yangu. Baada ya kukabidhiwa majukumu hayo ya kuibeba dhamana ya Chama, licha ya kwamba nilikuwa Shuleni, nilijituma kadri ya uwezo wangu kukijenga na kukieneza Chama ndani na nje ya kata yetu, kupitia michezo ya Shule za Sekondari, kwa kukutana na watu Sokoni, minadani na hata pia kupitia Vikundi rika vya Maendeleo huko vijijini, ambavyo huko kwetu Mara tunaviita "Saiga".

Uchaguzi ulipotangazwa rasmi, tukawaandaa wagombea wetu, na tukaingia msituni kupambana, baada ya uchaguzi, tukashinda wenyeviti wawili wa vitongoji kati ya watatu waliopo kijijini kwetu, cha kushangaza, CCM wakashinda nafasi moja ya kitongoji, ila wakamtangaza Mwenyekiti wa Kijiji kigumashi, jambo lililonikera sana, haijawahi kunitokea.

Baada ya uchaguzi huo wa Serikali za mitaa, ikafata zamu ya uchaguzi wa Serikali Kuu, madiwani, wabunge na Rais. Hapa sasa, ilikuwa ni patashika nguo kuchanika, kwa kuwa walitunyang'anya nafasi ya Mwenyekiti wa Kijiji kwa mabavu, ikabidi tuwaandae vijana wenzetu kuhusu namna ya kukabilisna na uchaguzi Mkuu uliokuwa mbele yetu ili kuhakikisha kwamba Diwani wetu wa CHADEMA anashinda nafasi hiyo.

Licha ya kwamba ilikuwa ndio mara yetu ya kwanza kuwasimamisha wagombea wa CHADEMA ndani ya Kata yetu na Jimboni kwetu tangu Nchi ipate uhuru, lakini nadhibitisha hili hadharani kwamba, Kata yetu ya Nyansurura ambayo mimi ndiye Kiongozi wa Chama mwenye dhamana ya Uenezi, ni miongoni mwa Kata 6 pekee zinazoongozwa na CHADEMA kati ya Kata 28 za Jimbo la Serengeti huko Mkoani Mara.

Jimboni kwetu (Serengeti) nako pamoja na kwamba ndio uliokuwa mwanzo wa kumsimamisha mgombea wa CHADEMA kwa nafasi ya Ubunge, nilikuwa miongoni mwa vijana walioshiriki kikamilifu katika kumpambania mgombea wetu, mpaka hatua ya mwisho. Nafarijika sana kutamka kuwa, pamoja na masahibu mengi tuliyokumbana nayo katika kipindi chote cha uchaguzi, tulifanikiwa kupata kura 19,700 ambazo ni sawa na 41% ya kura zote, ili hali mgombea wa CCM akatangazwa kigumashi kwa 54% ya kura zote, huku mwenzetu wa CUF akipata 5% ya kura zote.

Licha ya kwamba mpaka leo hii sikuwahi kukata au kukatishwa tamaa na mtu yeyote yule, lakini nimeendelea kuwa mwaminifu, mtiifu, mwadilifu, mjukumikaji katika shughuli zote za kichama popote pale zinapotokea ndani ya mipaka ya Nchi yetu, na hata wakati mwingine nimeendelea kuwa msiri sana kwenye mambo muhimu na nyeti ya Chama chetu, tena mambo yanayohitaji vikao maalumu vya Chama ili kuyazungumza, ili kuilinda heshima na hadhi ya Chama chetu, maana ninaamini kuwa wasakatonge watabana sana ila mwisho wao utakapofika wataachia.

Nje ya Jimbo na Katani kwetu, nimekuwa miongoni mwa vijana wenye nia na moyo wa dhati katika kukipigania Chama masaa 24. Ninaendelea kushiriki harakati zote za kukijenga na kukieneza Chama hiki, kila ninapokutana na harakati hizi ndani ya Nchi yetu.

Ninaendelea kushiriki Mikutano mbalimbali ya kukijenga Chama, nimekuwa nikishiriki katika midahalo, matamasha na makongamano mbalimbali yaliyofanyika Nchini kwa ajili ya kutoa elimu kwa watanzania, juu ya mchakato wa Katiba mpya unaoendelea Nchini hivi sasa, mchakato ambao Chama changu ni miongoni mwa Taasisi zinazoitetea Rasmu ya Tume ya Jaji Warioba, yenye maoni ya wananchi yaliyokusanywa kwa mujibu wa Sheria.

Nitaendelea kukitetea, kukijenga na kukilinda Chama hiki kama Mboni ya Jicho, popote nitakapokuwa, iwe ndani au nje ya mipaka ya Nchi yetu.

NITAFANYA NINI NDANI YA BAVICHA TAIFA NA CHAMA KWA UJUMLA

Sote tunatambua kuwa, CHADEMA bila Mabaraza haya ya BAVICHA, BAWACHA na WAZEE tena yaliyo imara, ni sawa na Bunge la Katiba bila Tundu Lissu, Halima Mdee na Jussa Ladhu wa Zanzibar.

Kwa kushirikiana na Viongozi wenzangu wa Baraza na Chama kwa ujumla, tutakwenda kuangalia namna bora ya kukitafutia wigo mpana kitengo hiki cha hamasa Nchini, ili huduma iweze kuwafikia walengwa kwa haraka na wepesi zaidi, tofauti na ilivyo sasa kwa mfano kwamba, mtu wa Uhamasishaji aliyeko Makao Makuu ya BAVICHA Taifa, ndiye atakayefika Songea, Pemba, Mwanza, Tabora, Lindi au Tarime, ndipo huduma ya hamasa iwafikie wananchi wa eneo hilo husika.

Hapa namaanisha nini, namaanisha kwamba, kwenye kitengo hiki cha hamasa ndani ya BAVICHA Taifa, tutafanya ugatuaji wa madaraka kutoka Makao Makuu ya Baraza na kukasimisha mamlaka hayo katika ngazi zote za uongozi wa Chama, kuanzia Taifa, Kanda, Mikoani, ndani ya Wilaya/Majimbo, Kata/Shehia, Matawi na Misingi.

Utaratibu huu mpya nitakaokwenda kuuanzisha,utafanikiwa kwa kutoa elimu kwa watu maalumu watakaoteuliwa na wataalamu wa mafunzo ya Chama kwa kushirikiana na Baraza, ili kusudi, baada ya wao kupata mafunzo hayo kutoka kwa wataalamu wa mafunzo wa Makao Makuu ya Chama, nao watapelekwa kwenye Kanda.

Baada ya watu wa Kanda kupata mafunzo hayo ya Uhamasishaji, nao watapelekwa Mikoani, ili kusaidia kutoa elimu kwa watu wa Wilaya/Majimbo, nao watu hawa wataipeleka elimu hii ya hamasa kwa watu wa Kata zao, na hawa wa Kata watakwenda kutoa elimu ngazi ya Matawi na hawa wa Matawi nao, watatusaidia kuipeleka elimu hii ya hamasa kwa watu wa ngazi ya msingi.

Ndugu zangu watanzania, yapo mengi naamini kwa kushirikiana nanyi, naamini nitayafanya, ila kikubwa zaidi, natambua ni uaminifu, uwazi, uwajibikaji, uadilifu, heshima na utii wa kanuni na taratibu za Chama chetu, zilizoainishwa katika Katiba yetu ya Chama.

Nihitimishe kwa kuwatakia kila la kheri ninyi nyote mnaoendelea na chaguzi za ndani ya Chama, sio tu kwa wale wa ngazi za Wilaya/Majimbo, hata pia ninyi wa chaguzi za ngazi za Mikoa.

Ahsanteni sana!!!

Francis Boniface Marwa, Mgombea wa nafasi ya Mratibu wa Hamasa BAVICHA Taifa 2014. 0785881009/0767881009 01/09/2014. *****************

Aluta Continueeee........
 
Membe ni dhaifu sana kuliko wagombea wote ccm. Anabebwa na familia za wakubwa...anatoa rushwa aliwapeleka baadhi ya viongozi Wa vyio vikuu china, safari ile iliratibiwa na jamaa ambaye alishakuwa kiongozi TAH..SO. Huyu bwana aligombea ubunge akanguka chino pu! Nasikia 2015 anautaka ubunge,lakini nafasi hakubaliki kwenye like jumbo hata kidogo. Haya nayajua vizuri Kwa sababu shughuli za nyingi ziko kwenye maeneo Yale.

Niseme pia Mh.Pinda kutoa kwake machozi hazarani siyo udhaifu. Barani Africa kunaKeneth Kaunda alikuwa na hisia kali,alipotembelea vijijini na kuona umasikini watu wake walionao aliangua kilio. Machozi ya karibu yanadhirisha kiwango cha hisia ya mtu,pamoja na upendo wa kiongozi kwa watu wake.

Pinda ni makini na hili kundi la Mh.Membe linamuogopa sana.Hivi majuzi ulifanyika kikao cha diaspora,walipo sikia kuwa Pinda yupo pale katika harakati zake za kuelekea ofisi kuu ya nchi 2015,waliamua kukimbia mwaliko ule.
 
mimi namjua,anaitwa joka la mdimu,..halili ndimu lakini ukichuma lazime likugonge!


Nyabhingi bwana:)...Kumbe bado unakumbuka yale maneno ya aliyekuwa Mbunge wa jimbo Mchinga Ndg. Mundhiri Mundhiri.

Lakini baadae kilichotoea Joka la Mdimu likamshikisha adabu kwa kumtengenezea zinga la kiunzi/zengwe la kufa mtu. Inasemekana Joka la Mdimu lilijenga mkakati wa kumtafuta na hatimaye kupandikiza mpinzani chipukizi wa kumgaraza Mundhiri tu kwenye kura za maoni ile 2010.
Na matokeo yake ubunge wa jimbo Mchinga ukawa historia kwa Mundhiri. Na mpaka leo unaambiwa Mundhiri na Joka la mdimu ni uhasama wa ule wa 'bifu' la kufa mtu kwani ni watu ambao hawatazamani macho kwa macho wala kukutana kwenye hadhara moja huko kwao Lindi, huku Mundhiri akiwa ni majeruhi kwani mdomo ulimponza.
 
Mkuu Sikumbuki kama Bara wameshawahi kutoa rais wa Zanzibar
Hata mimi sikumbuki lini Mzanzibar aliwahi kuwa rais wa Tanganyika. Bali ninachokifahamu sheria isiyoandikwa kuwa urais wa Tanzania ni kupokezana kati ya mtanganyika na Mzanzibar. Hivyo basi huu ni wakati wa Mzanzibar kuwa rais wa Tanzania.
 
Katika uongozi wa sasa, aina ya kiongozi wa kumrithi JK naona bado sijaona anayefaa coz we will need someone who can do a real transformation of how we work.. JK tried but we need someone to take it to the next level..Sasa kwa Membe bado sana!!!


Hapo kwenye nyekundu; huyo Jakaya wako unaesema he tried, my foot what did he try to accomplish? The dude has had no vision during his tenure and only succeeded to log in millions of astronomical miles in the process ballooning our external debt!!! In a sane country the dude could be impeached for abuse of office.
 
Tunataka kiongozi mwadirifu hatutaki watu wanaogombea sababu gesi imepatikana .........

Kama kweli tunataka kiongozi mwadilifu basi sio ndani ya ccm cause huko hayupo hata 1, kwangu mimi nataka kiongozi kwanza kweli awe mwadilifu na mchapa kazi wa kweli na visionary leader na awe mtu mwenye msimamo wa mambo mbalimbali, pia awe mtu wa ku-take action kwa wazembe! Ndani ya ccm mtu wa hivyo sijamuona bado.
 
Back
Top Bottom