Baada ya Nigeria kukataliwa kujiunga na BRICS+, yatuma maombi kujiunga na G20

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,115
49,838
Nigeria ilituma maombi ya Kujiunga BRICS na Kukataliwa Kwa sababu za Kisiasa.Sasa imetuma maombi ya Kujiunga na G20 kundi la Mataifa yenye Uchumi mkubwa Duniani.

Je watakubaliwa au watachinjiwa tena baharini? Tusubirie tuone.

Mwisho Hivi hizi blocks Huwa na faidia ipi? Kwa mfano uanachama wa Ethiopia utaisaidia vipi kimaendeleo?

=========

NIGERIA: Nigeria is considering applying to join the G20 group of major economies

President Bola Tinubu’s spokesman Ajuri Ngelale said on Sunday that the government was weighing the risks and benefits of membership before making a decision on whether to submit an application.

“While Nigeria's membership of the G20 is desirable, the government has embarked on wide-ranging consultations with a view to ascertaining the benefits and risks of membership," Mr Ngelale said in a statement.

President Tinubu has travelled to Delhi to attend the group's summit at the invitation of the Indian Prime Minister Narendra Modi.

Mr Ngelale earlier said that Mr Tinubu’s attendance at the G20 summit was to seek foreign investment in Nigeria, mobilise investors and strengthen bilateral agreements with other countries.

Currently, South Africa is the only African member of the G20.

Daily News
 
Mimi nikafikiri Nigeria wamekataa wenyewe kumbe walikataliwa. Kuhusu Ethiopia nao kukubaliwa ni lazima wameona kuna faida kubwa kwao. Ardhi yao wanaweza kuibadilisha na kuwa ya kilimo. Hapo akija mchina kwa viwanda na Brazil kwa kilimo basi hapo wanaangalia maslahi pia.
 
kwamba Ethiopia na Nigeria , ni bora Ethiopia?
Hapana
Sina maana hiyo wala mimi sio niliewakataa Nigeria
Nigeria wana uchumi mkubwa zaidi na ni taifa kubwa ila kijiografia labda
Hawajaweka sababu za Nigeria kukataliwa labda wewe unaweza kutuongezea
 
Kwa mtazamo wangu!

Hapo Ethiopia kapigiwa debe na Mchina.

Ikumbukwe Mchina kaweka mizizi mirefu ya kiuchumi Ethiopia. Ethiopia anatekeleza miradi mingi kupitia mikopo yenye riba kubwa kutoka China.

Mchina anampelekesha Ethiopia anavyotaka, na kaona amuweke karibu huko BRICS ili amdhibiti vizuri.

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Kwa taarifa yako INDIA ni moja ya washirika wakubwa wa West, lakini yupo Brics
Ukiongea ushirika, kila nchi iko na ushirika na West. Ndio maana China anafanya biashara kwa kiasi kikubwa sana na Marekani. Kwahiyo shida sio ushirika, shida ni itikadi.

Wote unaowaona hapo BRICS, itikadi zao zinapingana na itikadi za magharibi. Kushirikiana kibiashara na nchi za magharibi haibadili ukweli kuhusi misimamo yao!
 
Back
Top Bottom