Baada ya muda mrefu kukataa kuoa sasa sina budi kukubali kuja kuoa siku za usoni

Loading failed

JF-Expert Member
Sep 14, 2023
1,945
5,849
Baada ya kukataa sana kuoa huku nikidai kuoa ni anasa na ni gereza kwa mwanaume, hasara kwenye maisha ya mwanaume, na ajira ya faida kwa mwanamke. Sasa naona sina budi kukubaliana na kuoa nafsi yangu inaniamuru sana nitafute mwanamke mwingine wa kitofauti sana ni oe na nitulie niachane na maswala ya ujana sasa.

Kweli najua wanawake wanazingua sana maana hata sasa na wanawake kadhaa na nimejifunza mengi sana kwao.

Nimetendwa sana na kudharauliwa na baadhi yao ila sasa acha tuu nije kuoa. Ndugu zangu nimegundua kuoa ni jambo jema sana japo sishauri muoe, wewe sikiliza nafsi yako. Nafsi yangu inaniambia ni oe.

Naombeni maombi yenu nije kupata mke mwema huko ni endako, sikatai tena kuoa mimi nimejigundua kuoa ni wito mmoja wapo niliowekewa hapa duniani.

Kila jioni nikitoka mihangaikoni na kurejea nyumbani, kila usiku nikishtuka usingizini na kila asubuhi ni kiamka lazima nione ndani kwangu kuna kitu kimepungua ambacho ni mwanamke.

Hakika nimepungukiwa na mwanamke ndani ya nyumba yangu sasa acha nitafute mmoja anayejielewa niweke ndani haijalishi atanipitisha magumu kiasi gani ila nitamchukulia kama chombo dhaifu kisicho na nguvu na nitatumia akili kuishi nae, isipo kua asichepuke tuu maana sito msamehe akichepuka na nikithibitisha.

MWENYEZI MUNGU NITANGULIE NA UNIPE MKE MWEMA ILA ASIWE AMESHA ZAA NA MWANAUME MWINGINE . AMINA
 
Kuoa hakukwepeki, huwa ni suala la muda tu.

Ni kweli kwenye kuoa kuna matatizo lakini pia upande mwengine una mazuri yake ikiwemo watoto kuishi chini ya mwamvuli wenu, kujulikana umeoa unaheshimika na jamii kwamba haufanyi umalaya (hata kama unaufanya)

Kuna ndugu yangu alikuwa na 38 hajaoa, kila tukikutana kwenye events za kindugu hata sisi wadogo kwake tuna wake zetu basi ikawa nongwa akaamua nae avute jiko tu.

Kuoa ni sehemu ya kuwa kwenye jamii
 
Kuoa hakukwepeki, huwa ni suala la muda tu.

Ni kweli kwenye kuoa kuna matatizo lakini pia upande mwengine una mazuri yake ikiwemo watoto.

Kuna ndugu yangu alikuwa na 38 hajaoa, kila tukikutana kwenye events za kindugu hata sisi wadogo kwake tuna wake zetu basi ikawa nongwa akaamua nae avute jiko tu.

Kuoa ni sehemu ya kuwa kwenye jamii
Kuna kwepeka vizuri tu
 
Kuoa hakukwepeki, huwa ni suala la muda tu.

Ni kweli kwenye kuoa kuna matatizo lakini pia upande mwengine una mazuri yake ikiwemo watoto kuishi chini ya mwamvuli wenu, kujulikana umeoa unaheshimika na jamii kwamba hauzini nje ya ndoa (hata kama unazini)

Kuna ndugu yangu alikuwa na 38 hajaoa, kila tukikutana kwenye events za kindugu hata sisi wadogo kwake tuna wake zetu basi ikawa nongwa akaamua nae avute jiko tu.

Kuoa ni sehemu ya kuwa kwenye jamii
unamaana gani unaposema kuoa hakukwepeki? Kwani usipooa utakufa au nidhambi? Kutokuoa ni maamuzi ya mtu binafsi kama maamuzi mengine, kuna jamaa yangu hataki kusikia kabisa maswala ya ndoa na anawatoto wa 4 ambao amezaa na wanawake watatu tofauti ila mpango wakuoa hana....
 
Mke wako mtarajiwa SA hiv yuko kwa muhuni anainyonya
Inaweza ikawa kweli au siyo kweli usinijaze hofu kinamna. Mungu ndiye atakaye amua. Na ikimpendeza akinipa bikra ni jambo la kushukuru ila akinipa huyo unaye mtaja wewe sito muhukumu kwa namna yeyote zaidi ya kuanza kurasa mpya, jambo kubwa ni asiwe amezaa na mwanaume mwingine basi inatosha na kipindi chote awapo na mimi asinisaliti nikajua maana sito samehe na ikiwezekana Mungu aniepushe na kusalitiwa
 
Back
Top Bottom