Shigganza
Senior Member
- May 24, 2018
- 160
- 412
Baada ya kuusikiliza kwa umakini mkutano wa Mdude Chadema na waandishi wa habari hivi, mambo yafuatayo ni dhahiri:
1. Mpaka sasa bado akili ya Mdude haijawa sawa kumwezesha kutaja watuhumiwa kwa hoja zaidi ya mihemko na hisia zake na Chadema za siku nyingi kwa Serikali. Baadhi ya Mambo yanaonesha kukosekana kwa utimamu wa Afya ya akili yake ni kitendo cha yeye mwenyewe kukiri "bado akili halijakaa vizuri " pamoja kukosa kumbukumbu kuhusu mkasa uliomkuta.
2. Kauli ya Katibu Mkuu wa CCM kwamba kuna mahala Taifa liliacha wajibu wake wa kuandaa viongozi imejidhihirisha, Mdude ameulizwa na Mwandishi wa habari kuhusu matumizi ya maneno makali na ya kutukana kupitia kwenye makala zake anazoandikaga kwa Rais, akajibu yeye hajui tofauti ya maneno yanayoonesha kutukana, kukosoa kumbuka huyu ni kiongozi wa oganizesheni ya mafunzo na itikadi KANDA ya Nyasa na hapa ndipo naona ni kwa namna gani Bavicha kama chombo kinachopaswa kuandaa vijana kimaadili ikiwemo kuheshimu viongozi wa kitaifa haijatimizanwajibu wake n.k
3. Kuna mkanganyiko mkubwa kuhusu ukweli wa kile alichokisumulia mfano alizimia kwa siku tatu alipoamka akawa anahisi njaa (akaomba apatiwe soda na bisukuti), anaeleza alikuwa anapigwa na chupa za bia kwa maelezo yake ya awali akiwa hospital, kitu cha kujiuliza mbona hana michubuko yoyote usoni? Mara alimsimamisha bodaboda akaenda kusimama umbali mfupi kama MITA 100!!!
4. Mkanganyiko mwingine ni alipozimia watekaji walimziba mdomo kwa bandeji na solotepu na kisha walimfunga pingu mkononi na kumpiga miguuni. Hapa unajiuliza hawa watekaji walikuwa binadamu au majini maana kwa kawaida mtu hufanyiwa vitu hivyo akiwa mzima ili kumdhibiti sasa kwa aliyezimia unakuwa unatafuta nini?
5. Jambo la mwisho wakati anazungumza kuna wakati alikuwa anatoa sauti ya kilio PASIPO kutoa MACHOZI wataalamu wa masuala ya saikolojia tukio hilo wanaweza kulitafsiri kuwa hakuwa na uhusiano wa mwonekano wake wa nje na ndani zaidi ya kuigiza.
Miongoni mwa posti alizowahi kuchapisha ni hii hapa.