Baada ya kusoma makala yake nikaisaka CV ya Njelu Kasaka

shabani

JF-Expert Member
Apr 3, 2009
309
221
MEMBER OF PARLIAMENT CV

GENERAL
SalutationHonourableMember picture
1264.jpg
First Name:Njelu
Middle Name:E.M.
Last Name:Kasaka
Member Type:Constituency Member
Constituent:Lupa
Political Party:CCM
Office Location:P.O. Box 12382, Dar es Salaam
Office Phone:+255 741 530227
Ext.:
Office Fax:
Office E-mail:nkasaka@parliament.go.tz
Member Status:Current Member
Date of Birth2 February 1942
EDUCATION
School Name/LocationCourse/Degree/AwardStart DateEnd DateLevel
University of Kentucky-USAM.Sc (Agric. Economics)19791980MASTERS DEGREE
University of Dar es SalaamB.A (Economics)19711974GRADUATE
University of Colorado-USADiploma in Economics1/1/19781/6/1978DIPLOMA
Mkwawa High School-IringaA-Level Education19691970HIGH SCHOOL
Tosamaganga Secondary School-IringaSecondary Education19651966SECONDARY
Sangu Secondary School-MbeyaSecondary Education19671968SECONDARY
Kipembawe Primary SchoolPrimary Education19571960PRIMARY
Chunya Middle SchoolPrimary Education19611964PRIMARY
EMPLOYMENT HISTORY
Company NamePositionFromTo
Iringa/Tabora RegionsRegional Commissioner19982000
Ministry of Agriculture and CooperativeDeputy Minister19941998
CRDB BankChief Manager19901994
CRDB BankRegional Manager I-Iringa19851990
CRDB BankRegional Manager II-DSM/Iringa19811985
CRDB BankRegional Manager III-Mtwara19761980
CRDB BankRegional Representative-Tabora/Mtwara19751976
CRDB BankProject Officer III19741975
POLITICAL EXPERIENCE
Ministry/Political Party/LocationPositionFromTo
CCM Political Commettee-Iringa & Tabora RegionsMember19982000
CCM-Chunya DistrictCCM Publicity Secretary19921997
CCM Political Commettee-Mbeya RegionMember19921997
CCM Regional Executive Committee-MbeyaMember1992To date
CCM-Chama Cha MapinduziMember1977To date
TANUMember19731977
SPECIAL SKILLS
Skill Name or DescriptionYears ExperienceAcquired Through
JKT2Makutupora
Project Appraisal1IFM-Dar es Salaam
Small Industry Financing1Hyderabad-India
Small Farmer Credit Administration1Washington, DC
Cooperative Development1Cooperative College-Moshi
Commercial Banking1Nairobi-Kenya

alikuwa na haki ya kuandika alichokiandika katika gazeti la RAIA MWEMA.

=====

Njelu Kasaka
JE KATIBA ILILYOPENDEKEZWA ILIPITA KIHALALI?

WIKI tatu baada ya Bunge Maalumu la Katiba (BMK) kumaliza kazi yake, yameibuka mambo mengi ambayo kwa kiwango kikubwa yameiabisha Tanzania. Bunge Maalumu la Katiba lilimaliza kazi yake wiki mbili kabla ya kuadhimisha kumbukumbu ya kifo cha Mwalimu Julius Nyerere kiongozi aliyeiletea Tanzania heshima kubwa kutokana na tabia yake, mwenendo wake, msimamo wake kuhusu rushwa, maonevu kwa raia, ukombozi wa Afrika na uhuru wa binadamu popote duniani. Mwalimu Nyerere alijitahidi kwa kiwango kikubwa kuwaelimisha na kuwaambia ukweli Watanzania kuhusu maisha yao na kuhusu nchi yao.

Bunge Maalumu limemaliza mchakato wa kupata Katiba Mpya huku zikiibuka tuhuma lukuki kuhusu udanganyifu uliofanyika katika kupitisha Katiba hiyo mpya kwa mujibu wa sheria. Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta, alitangaza Katiba kupita kwa ushindi mwembamba wa kura mbili upande wa Zanzibar ambako kulikuwa na wasiwasi wa kukosekana theluthi mbili. Upande Tanzania Bara haukuwa na matatizo.

Mara baada ya kupitishwa kwa Katiba Inayopendekezwa, imebainika kwamba kuna kura tatu zenye utata. Katika kura hizo tatu zenye utata, moja inadaiwa kuwa ni ya marehemu, nyingine ni ya mjumbe wa NCCR-Mageuzi ambaye amejitokeza hadharani na kusema hakushiriki kupiga kura kwenye Bunge Maalumu la Katiba. Kura ya tatu inayoibua maswali mengi ni ya Zakia Meghji ambaye inadaiwa aliingia Bunge Maalumu la Katiba kama mjumbe kutoka Tanzania Bara lakini akapiga kura kama mjumbe kutoka Zanzibar.

Madai haya yakithibitika yanaashiria kulikuwa na udanganyifu katika kupitisha Katiba Inayopendekezwa. Kitendo hicho kinazusha maswali kwa nini Bunge Maalumu la Katiba lidanganye? Linamdanganya nani na kwa faida ya nani?

Wabunge wa Bunge Maalumu walikuwa Dodoma kuwakilisha wananchi wapatao milioni 50 wa Tanzania. Rais Jakaya Kikwete aliwateua ili wawawakilishe mamilioni ya Watanzania wenzao ambao hawakwenda Dodoma. Wadau wa mchakato wa Katiba ambao hawakwenda Dodoma ni wananchi na Rais Kikwete mwenyewe. Kwa mtazamo huu kama kulikuwa na kudanganya, Bunge Maalumu lililenga kuwadanganya wananchi na Rais aliyeliteua. Lakini mchakato wa Katiba ulifuatiliwa na dunia pia. Kwa hiyo mlengwa mwingine katika udanganyifu huo ni dunia.

Kwa hiyo, ukitaka kupata jibu la sehemu ya pili ya swali la pili kwamba wajumbe walifanya udanganyifu kwa faida ya nani, jibu lake ni kwa faida ya wajumbe wenyewe. Kwa wajumbe wanaowadanganya wananchi wenzao, Rais na dunia, lazima manufaa yanayokusudiwa yawalenge wajumbe wenyewe.

Maelezo haya yanatupeleka katika kujibu swali la kwanza, kwa nini Bunge Maalumu la Katiba lilidanganya. Nafikiri wajumbe walifanya hivyo ili kumwonyesha Rais, wananchi na ulimwengu kwamba wajumbe hao walikuwa na uwezo wa kukamilisha mchakato wa Katiba Mpya licha ya upinzani na lawama nyingi kutoka kwa vyama vikuu vya upinzani, taasisi za kijamii na baadhi ya wananchi.

Lakini ukichunguza kwa undani, udanganyifu ulifanyika ili kutetea msimamo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilichokuwa kimetangaza wazi kwamba hakitakubali Katiba ya muundo wa serikali tatu katika Muungano. Mpaka hapa inaonekana wazi kwamba chombo kinachotuhumiwa kufanya udanganyifu ni Bunge Maalumu la Katiba, lakini ikumbukwe pia kwamba baadhi ya wajumbe wa BMK walikuwa ni mawaziri, maspika na wanasheria wakuu wa serikali.

Ni wazi udanganyifu katika jambo kubwa kama hili hauwezi kufanyika bila ya serikali kujua. Kwanza kabisa Mwenyikiti wa BMK Samuel Sitta ni waziri katika Serikali ya Muungano. Uwepo wa viongozi wa serikali katika BMK unatupeleka kwa mshirika mwingine katika udanganyifu ambaye ni serikali. Serikali haiwezi kuzikwepa tuhuma hizi kwa kuzingatia muundo wa Bunge Maalumu la Katiba.

Kwa hiyo, wahusika katika udanganyifu ni BMK pamoja na serikali na walengwa ni wananchi na dunia. Udanganyifu si kitendo kizuri popote duniani na ubaya wake unakuwa mkubwa zaidi unapotendwa na kiongozi. Madhara yatokanayo na kitendo hiki ni mengi. Mosi, ni uwezekano wa Katiba kupitishwa visivyo halali na Katiba yenyewe kupoteza heshima ya kuwa Katiba halali. Pili, wananchi kukosa imani na viongozi wao na pia serikali yao.

Tatu, dunia kukosa imani na viongozi wa Serikali ya Tanzania na serikali yenyewe. Viongozi wanapowadanganya wananchi wao ni ishara kwamba wako tayari, wakipata mwanya, kumdanganya mtu mwingine yeyote. Kiongozi mdanganyifu haaminiki popote na hasa katika nchi zilizoendelea.

Nne, kutokana na udanganyifu kufanywa na viongozi na serikali, Tanzania inapoteza heshima na hadhi iliyokuwa imejijengea miaka ya nyuma hususan kipindi cha utawala wa Mwalimu Nyerere na miaka iliyofuatia. Heshima ya nchi huletwa na heshima, hadhi na uaminifu wa viongozi wa nchi husika. Nchi haiwezi kuheshimika iwapo viongozi wake wanajulikana kama ni watu wasioaminika na wanaojihusisha na vitendo vya kukiuka sheria na maadili. Tano, viongozi wanapofanikisha jambo kwa njia za udanganyifu, tabia hujengeka kwa viongozi kuendelea kutumia njia hizo katika kufanikisha mambo mengine mbalimbali wanapokwama.

Siku moja nilikutana na mchina ambaye amekaa muda mrefu hapa Tanzania. Aliniambia wazi kwamba hakuna mtu anayefuata sheria katika Tanzania. Kila jambo hutegemea mhusika ana hadhi gani katika jamii, uwezo wake kifedha au uhusiano wake na watu wenye madaraka serikalini. Mchina huyo alisema hakuwa na imani kabisa na matamshi ya viongozi kwa kuwa huwa hayatekelezwi na yasipotekelezwa hakuna mtu wa kuwauliza au kuwachukulia hatua yoyote wahusika.

Inaonekana hapa Tanzania viongozi kudanganya wananchi linaanza kuwa ni jambo la kawaida na viongozi hawaoni aibu kufanya hivyo. Lilipozuka suala la ufisadi wa EPA viongozi wakubwa tu serikalini walisimama hadharani na kusema Dk. Wilbrod Slaa alikuwa mzushi na mwongo. Vielelezo alivyowasilisha bungeni vilielezwa kuwa ni vya kughushi. Lakini kadiri muda ulivyosonga mbele na ushahidi zaidi kupatikana ilidhihirika kwamba zaidi ya shilingi bilioni 133 zilichukuliwa kifisadi kutoka Benki Kuu ya Tanzania.

Kuna matukio mengi tu ambayo yametokea katika miaka ya hivi karibuni yenye sura kama hii. Hivi sasa tuna madai ya wizi au ufisadi wa fedha za Tegeta Escrow Account ya IPTL (Independent Power Tanzania Limited) ya shilingi bilioni 200. Maelezo ya serikali ni yale yale ya kukataa na kusema fedha hizo siyo za serikali.

Hoja hapa siyo kwamba fedha ni za serikali au za mtu mwingine. Kinachozungumzwa ni fedha kuchukuliwa visivyo halali na watu wasio husika. Hoja ya msingi ni kwamba ufisadi au wizi umefanyika ambavyo ni kosa la jinai hata kama fedha si za serikali. Lakini hatua za awali za serikali ni kuonyesha kwamba hakuna kitu kibaya kilichofanyika katika kuchukuliwa kwa fedha hizo. Kwa kufanya hivyo, viongozi wa serikali na serikali yenyewe wanajiweka katika mazingira ya kuhoji ukweli wao na uaminifu wao katika suala zito kama hili.
Mpaka sasa baadhi ya nchi washirika wa maendeleo zimeanza kuzuia misaada kwa Tanzania kwa sababu ya fedha za IPTL.

Kuzuiwa kwa misaada tafsiri yake ni kwamba wahisani wanahoji ukweli na uaminifu wa viongozi wa Serikali ya Tanzania. Iwapo itathibitika baadaye kwamba fedha hiyo ilichukuliwa visivyo halali ni wazi tukio hilo litazidi kushusha hadhi ya viongozi wetu na kuiaibisha Tanzania katika macho ya ulimwengu.

Moja ya sifa muhimu za binadamu ni kuona aibu. Swali linakuja kwa nini viongozi wanafanya mambo ya kuiabisha Tanzania na kujiaibisha wao wenyewe? Tukae tunajua kwamba watu wa mataifa mengine wataendelea kutudharau siyo kwa sababu ya uafrika wetu, bali kwa sababu ya vitendo vyetu visivyoendana na uaminifu na ukiukwaji wa maadili.

Kuhusu Katiba mpya ni wazi imeandikwa miaka 53 baada ya kujitawala Tanganyika na miaka 50 baada ya Mapinduzi ya Zanzibar. Wakoloni hawapo wala sultani hayupo. Ni Katiba yetu wenyewe inayolenga Watanzania kujitengenezea mkataba wa namna nzuri ya kujitawala ili kujiletea maendeleo ya haraka kwa ustawi wa wananchi wote.

Inashangaza kuona Katiba yenye malengo mazuri kama haya ambayo inatungwa na Watanzania wenyewe, inapitishwa katika mazingira ya kutatanisha. Kipindi hiki Watanzania wengi wana uelewa mpana wa nini maana ya uhuru, maendeleo, demokrasia, haki za binadamu na mienendo ya kisiasa ulimwenguni. Kwa nini kupitisha Katiba kwa mtindo ambao mwisho wa siku tunapata fedheha badala ya heshima?

Walimwengu wanatutazama na kutufanyia tathimini hata kama hawasemi. Tanzania kwa hadhi iliyokuwa imefikia katika siasa za Afrika, haipaswi kutiliwa shaka katika jambo la kisiasa kama la kuandika Katiba mpya. Nchi hii ilishafikia mahali ambapo inapaswa kufanya mambo yake kwa uwazi, uhakika na uaminifu na hivyo kuendelea kuwa mfano wa kuigwa na nchi nyingine ambazo bado hazijaonja mifumo ya utawala bora. Si tu kwamba Tanzania iwe ni nchi ya mfano kwa amani na utulivu katika Afrika, bali iwe pia ni nchi ya mfano kwa utawala bora.

Katiba ikipitishwa na tuhuma lukuki nani atakuja kujifunza kutoka kwetu? Tanzania lazima iwe kama mke wa Kaizari ambaye hakupaswa kutiliwa shaka katika mwenendo wake. Kitendo cha kutilia shaka upigaji kura kupitisha Katiba Inayopendekezwa tayari kimekwishaondoa uhalali wa Katiba mbele ya watu wengi ndani na nje ya Tanzania.
Najua viongozi wetu wengi wanaweza wakapuuza maoni kama haya lakini waelewe, hawawezi kufuta ukweli huo katika nyoyo za watu.

Tusipojirudi Tanzania itazidi kupoteza heshima yake Afrika Mashariki, Afrika na duniani kote. Kiongozi kudanganya wananchi msingi wake ni ubinafsi. Maradhi ya ubinafsi yanalitafuna Bara la Afrika. Bara hili lina historia tofauti na mabara mengine duniani. Viongozi wa Bara la Afrika wanahitaji kufanya kazi ya ziada kurejesha heshima yake kutokana na kupitia katika enzi za utumwa na ukoloni.

Kutokana na madhila ya utumwa na ukoloni, Waafrika walipoteza heshima yao karne nyingi zilizopita na kufikia hatua ya kufikirika kwamba mtu mweusi si binadamu kamili. Mtu mweusi, imepata kusemwa, ameumbwa kutofuata wala kutii sheria.

Tungetazamia baada ya kujitawala kazi ya viongozi iwe ni kufuta mawazo hayo potofu. Kufuta kwake siyo kwa kulalamika kwenye majukwaa bali kutenda mambo kama binadamu walioelimika na kustaarabika. Binadamu aliyestaarabika hutenda mambo yake kwa kuzingatia haki, ukweli, uaminifu na kufuata sheria. Binadamu huyu anathamini binadamu wengine hata kama hawana elimu na uwezo kama yeye wala utajiri kama wa kwake.

Moja ya malengo ya kujitawala ilikuwa ni kurejesha heshima na utu wa mwafrika. Kwa namna gani? Kwa kuendesha serikali zetu za kiafrika kwa ubora ulio sawa au kwa njia bora zaidi kuliko hata binadamu waliotuweka utumwani. Leo miaka zaidi ya 50 tangu nchi nyingi za kiafrika zipate uhuru, bado lengo hilo halijafikiwa kikamilifu kutokana na uendeshaji hafifu wa serikali za nchi hizi.

Ukiukwaji wa haki za binadamu, ukiukwaji wa sheria na taratibu za uchaguzi, matumizi mabaya ya fedha za serikali, ufanisi duni katika idara nyingi za serikali, usalama mdogo wa raia, njaa na umasikini, ni baadhi ya mambo yanayompunguzia hadhi na heshima mwafrika. Ubinafsi bado umetanda na kuwafanya viongozi wengi wa kiafrika kusahau moja ya malengo muhimu yaliyosababisha kuusaka uhuru.

Basi viongozi wa Tanzania kama sehemu ya Afrika, waelewe kwamba wamebeba dhamana kubwa ya kuhakikisha Tanzania na Watanzania wanapata hadhi na heshima wanayostahiki mbele ya macho ya walimwengu. Kutenda mambo ya kiserikali katika mazingira tatanishi hakuleti heshima kwa Tanzania wala kwa viongozi wenyewe.

Katiba mpya imependekezwa lakini mchakato wake utumike kujifunza mambo yanayoweza kuwa ya manufaa kwa Tanzania siku zijazo. Ni kweli kumekuwa na washindi katika mchakato wa kuandika Katiba mpya, lakini tujiulize ni kwa gharama gani kwa sifa ya Tanzania na kwa sifa na uaminifu wa viongozi wake?

- See more at: Raia Mwema - Je, Katiba Inayopendekezwa ilipita kihalali?
 
Hawa ndio watakiwi, hawaipendi nchi, ni wasaliti. Mungu atawalipa mema siku si nyingi.
 
Crdb ni benki ya ushirika na maendeleo vijijini ni chombo cha fedha kinachotoa mikopo kwa maendeleo vijijini pia hutoa huduma za kibenki pamoja na ushauri wa kitaalam ni chombo cha fedha kinachotoa mikopo kilichopitishwa na bunge July 1984
 
CRDB ni bank ya zamani sana, ilikuwa inaitwa Co-operative and Rural Development Bank kwa kifupi CRDB na ilipobinafisishwa mwaka 1996 ndio ikatumia kifupi chake cha CRDB 1996 Ltd,

Huyu mzee alifanya kazi CRDB kweli kama CV yake inavyoonyesha
 
Crdb ni benki ya ushirika na maendeleo vijijini ni chombo cha fedha kinachotoa mikopo kwa maendeleo vijijini pia hutoa huduma za kibenki pamoja na ushauri wa kitaalam ni chombo cha fedha kinachotoa mikopo kilichopitishwa na bunge July 1984

Siku hizi ni "CRDB Bank" wala siyo "Co-operative and Rural Development Bank-Benki ya Ushirika na Maendeleo Vijijini" Ilikwisha badirika ikabakiza kifupi chake tu. Huwezi kuona popote pale kwenye document zao kirefu cha CRDB as before. Ni sawa na NBC vivyo hivyo kwa sababu siyo benki ya Taifa tena.
 
Kwa Mtanzania yeyote mwenye upeo kiddogo tu wa kufikiri hali halisi ndio hiyo! Tuendako kama hakutatokea muujiza kuna giza nene. Bunge lianzalo keshokutwa lianze na swala la katiba iliyopitishwa na CCM kuwa je ilipatikana kihalali na inastahili kupigiwa kura? Mchezo mchafu alioucheza Sitta utaigharimu sana nchi yetu siku zijazo na watakaoumia ni vijana na watoto maana wao ndio taifa la kesho
 
Crdb ni benki ya ushirika na maendeleo vijijini ni chombo cha fedha kinachotoa mikopo kwa maendeleo vijijini pia hutoa huduma za kibenki pamoja na ushauri wa kitaalam ni chombo cha fedha kinachotoa mikopo kilichopitishwa na bunge July 1984

Huu ni wimbo huu...enzi zile...Thanking YOU
 
Tarehe 11/01/1971 ikiitwa TANZANIA RURAL DEVELOPMENT BANK (TRDB), soon ikawa CRDB na sasa ni CRDB (1996) BANK PLC.

Wakuu hii thread hasa mchango wa ndugu yetu huyu ukisomwa na mhs Mkapa, mhs Mwinyi, mhs Kikwete, mhs Cleopa Msuya, mhs Aboud Jumbe, mhs Malecela, mhs Warioba, mhs Salim, mhs Pinda/Lowasa, na waheshimiwa wengine wa Chama tawala, nafikiri nafsi yao itwasuta! Kwa yule aliyenda mema nafsi yake itakuwa na furaha na kufanya siku ya kusoma waraka huu ajisikie huru na salama moyoni mwaka. Amen!!
 
CRDB BANK ilianzishwa 1996, hiyo iliyoandikwa kwenye CV nafikiri sio hii ya hapa Tanzania.
shida kubwa, kubwa, kubwa, kubwa, kubwa,......... ya vijana wa Tanzania ni kutojifunza, na hivyo kutokuwa na taarifa za kutosha, LAKINI kwenye mijadala wamo! Sawa usijadili kuhusu kitu usichokuwa na taarifa nacho eeeh!
 
Back
Top Bottom