Azzan: Nitajiuzulu ikibainika nauza dawa za kulevya

Hiyo ni kweli kabisa....Lakini siamini Polisi wa Tanzania, nao wanahusika. The best way......... China au Hong Kong kuna askari wao.......wtafutwe wakalimani tu, Chinese -- Swahili language, waende huko gerezani halafu hiyo riport itolewe. Ukiingiza polisi wa bongo tu kila kitu kitatibuka.


Hii issue polisi wa Tanzania wakae pembeni mkitaka ukweli ujulikane .Polisi wa kimataifa wakawahoji hao wafungwa na kuahidi kwamba hawatatoa taarifa zao kwa serikali .Sababu wakienda polisi wa kibongo wataanza kuwatisha sijui baba yako ni nani ,jina la mama yako ,unakaa wapi . Kwa kuhofia usalama wao na familia zao hawatatoa ushahidi . LAKINI wakiweka condition ya kuwatunzania siri watatoa ushahidi
 
hapa hakuna kitu; hawa jamaa ni hatari sana, police wanatakiwa kuwakamata wote waliotaja mapema ili wasifiche ushahidi waonyeshe mtiririko wa account zao walinganishe na biashara wanazozifanya hapo TRA na mkaguzi wa mahesabu hashiriki na waangalie kwenye mtandao wa simu zao na e mail mawasiliano yao

Hivi mtu akimtaja mama yako anazini na babu paroka unataka jamii nayo imhukumu bila uthibitisho wa tuhuma zenyewe? Na utamlazimisha baba yako atoe talaka kwa maneno yasiyo na uhakika? Kama mliweza kuyakubali maneno yaliyoandikwa na mtu ambaye ameshindwa kujitaja kwa nini myakatae maneno ya mhusika ambaye amediriki hata kwenda kwenye vyombo vya sheria?
 
“amejilisalimisha” kwenye ofisi za jeshi la polisi na kulitaka jeshi hilo lifanye uchunguzi dhidi ya tuhuma zilizoelekezwa kwake, ili hatua nyingine na ikibidi sheria, vichukue mkondo wake.


Azzan amesema alienda mwenyewe kutoa taarifa katika Kituo Kikuu cha Polisi Kati, jijini Dar es Salaam.
Polisi gani? Hawa waliokamatwa na meno ya tembo kisarawe juzi usiku?au wale waliokamatwa na bangi kule rombo?au hawa wanaofanya uchunguz wa bomu la Arusha?itakua ni wale waliodakwa wakitaka kumpa mtu kesi ya kichwa kule morogoro ndio wanaotakiwa wafanye uchunguzi dhidi ya mbunge wa CCM.
Anyways, jamaaa amewaangukia sasa nanyi msimtupe mwana CCM mwenzenu fanyeni uchunguzi.......
 
Safi sana.
Polisi naomba mchukue hatua zifuatazo haraka.
1.Chukueni maelezo ya marmo.
2.China is our dear friend,pelekeni askari wakawahoji hao wafungwa.
3.Huyo azan atoe vithibitisho kuonyesha mali anazomiliki zimepatikana kwa njia harari na aweze kuthibitisha pasipo shaka.

Mkuu Marmo alishahamishiwa Ujerumani, after all hiyo barua imeandikwa na wafungwa walioko magereza za Hong Kong. China hawafungi, wananyonga wauza/wabeba sembe; bahati tu wale walikamatiwa Hong Kong ambako sheria ni laini kidogo km huku Tz.
 
Hii issue ishakuwa serious!

shinikizo la damu lisije mpata mtu tu na kila ki2 kupotea!

Ubovu wetu Tanzania huwa tunajua kupiga kelele weeee, hakuna hatua zinachukuliwa! Subiri usikie kimetokea KITUKO kingine kesho au kesho kutwa tuu na hii habari ya SEMBE na Mh Mbunge itapotea kama ambavyo (JAPO INAUMA) tumezoea kuona SCANDALS zinazohusisha WAKUBWA hapa nchini zikipotea........
 
Kama kweli unajiamini basi nenda kajitete kwa Polisi wa Hong Kong sio hawa wa hapa kwetu ambao mshawanunua siku nyingiiii....


Iddi+Azzan.jpg
 
Kwa jinsi anavyo haha kutafuta kujisafisha, inatiashaka kwanini anatumia nguvu kubwa na mna hii kujaribu kuuaminisha umma kwamba yeye ahusiki na biashara hiyo.
 
LAKINI hivi tunahangaika sana wakati JK anayomajina ya wazee wa unga si aseme tu kama jina hilo lipo kwenye listi ya majina aliyonayo
 
Kila mtu utasema anauza unga. Basi tukubaliane freeman mbowe na dr slaa nao wanafanya biashara ya mihadarati. Wanatumia ofisinyao pale kinondoni ufipa kuficha madawa hayo. Pia bilicanaz club ndo hutumika kama sehemu ya kukutana kwa wale wageni wa kutoka nje ya nchi. Inasadikika kuwa mbowe ni agenti mkubwa kwa nchi za ukanda mwa afrika mashariki na ya kati

Hujitambui. Kaolewe.
 
Kama JK alimuokoa mtoto wake huko China kwa kuweka nchi rehani leo hii nani atamtaja Azzan??
JK kama ana uwezo amwage mboga tuone Azzan kama hajamwaga ugali hadharani.
Wanatuzuga wananchi tu hawa lao moja.
 
Hii issue polisi wa
Tanzania wakae pembeni mkitaka ukweli ujulikane .Polisi wa kimataifa
wakawahoji hao wafungwa na kuahidi kwamba hawatatoa taarifa zao kwa
serikali .Sababu wakienda polisi wa kibongo wataanza kuwatisha sijui
baba yako ni nani ,jina la mama yako ,unakaa wapi . Kwa kuhofia usalama
wao na familia zao hawatatoa ushahidi . LAKINI wakiweka condition ya
kuwatunzania siri watatoa ushahidi

mkuu, jeshi la polisi ulimwenguni kote lina miiko ya aina moja. kwanza uelewe kuwa hatuna jeshi la polisi la kimataifa. sasa sijui hilo unalopendekeza unalitoa wapi. ila majeshi ya polisi ulimwenguni kote yanashirikiana
 
Anasema hahusiki kabisa na biashara hiyo na yuko tayari kupigwa hata risasi hadharani ikibainika anajihusisha na hiyo biashara.
Anasema jana alijipeleka mwenyewe polisi na kuwaomba wafanye uchunguzi wa kina kuhusiana na tuhuma hizo.
Anasema anahisi ni njama za wapinzani wake kisiasa kuelekea kinyang'anyiro cha ubunge 2015.
Yetu macho,kazi imeanza.
Na wale wengine waliotajwa kwenye barua ile ni kwa sababu wanataka kuogombea urais au ni wabunge wa Majimbo yepi. Ingekuwa vizuri wangeji-organize wote waliotajwa waende polisi, kisha wajiridhishe ikiwa huko Singapore kuna watanzania waliofungwa kwa ajili ya sembe? Ikibainika ndiyo, wahusika waliosababisha hao vijana kufungwa huko ni akina nani kama siyo wao.
 
Back
Top Bottom