Azam Tv yapewa leseni ya kuonesha chaneli za ndani bure

Nimemsikia Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano Atashasta Nditiye bungeni leo anasema tayari Azam wamepata leseni ya kuwa MUX wakiungana na akina Startimes Ting na Digitek...nadhani sasa ule ubabe wa soko wa mchina kutoonyesha chaneli za FTA bila malipo unaenda kukoma...hawa jamaa kwa ubora nadhani vingamuzi vyao vitanunulika sana. Hongereni Azam kwa hatua hiyo muhimu angalau tuone chaneli za ndani kwa ubora maana hivi visimbuzi vingine ubora hamna kabisa wengine mara wazime mara wawake...kama hao wengine wanaojinasibu wakubwa ubora picha zina ukunguukungu...

WITO WANGU KWENU AZAM...Mtuletee ving'amuzi vya maana na vya HD viwe na options lukuki ikiwezekana hata kuweka flash na kufanya gaming humo humo dunia ishaendelea fanyeni utafiti vizuri mje na kitu konki...wakenya waje wajifunze Tanzania. Heko!View attachment 1097133
Unataka niambia kuanzia sasa azam atasimika minara ya terrestrial?
 
Eti inabidi azam tutumie antenna za Mina? Mbona jamani awamu hii jamani tunarudi nyuma mambo mengi ? Yaani turudi analogy?
 
Nadhani ulikuwa miss informed sheria iko wazi kabisa ving'amuzi vya DSTV,ZUKU na AZAM ni SUBSCRIPTION DECODERS ambazo leseni zao haziwaruhusu kubeba local FTA kwa sababu wao ni business bent companies...wakati ving'amuzi vya MUX(Multiplex Operators) ambavyo ni TING,STATIMES,DIGITEK na CONTINENTAL ndivyo kwa mujibu wa sheria vinaruhusiwa kubeba local channels na leseni zao hawa ni gharama kubwa sana zaidi ya Milioni 800 wakati wale wa awali kina dstv leseni yao ni bei chee...kwa hiyo hayo makundi mawili kila mtu ana masharti yake ya leseni hivyo huwezi kuingilia masharti ya leseni ya mwenzako na ukamharibia biashara wakati yeye leseni yake analipa zaidi kuliko wewe.......ndicho walichokuwa wanafanya kina DSTV hapo zamani kwa kuzibeba FTA za local huku wakijipatia watazamaji wengi na kuvuna faida, na waliizuia TCRA kuwazuia waziondoe kwa sababu waliipeleka serikali mahakamani....sasa watu wanapotosha....kwenye biashara kila mmoja anapaswa kula share yake kwa usawa bila kuathiri mwingine kufanya biashara.....sasa AZAM baada ya kuona MUX kunalipa ndio nae kajiongeza kupata leseni kubwa kama wenzake wa TING,Star nk ili apate wateja zaidi....changamoto moja ni kwamba watanzania wengi huwa hatupendi kusoma sheria kanuni na miongozo ili kujielemisha juu ya masuala mtambuka yanayotuhusu....haya yote yamo kwenye tovuti ya TCRA na sheria zake zote zimo mle wazi TUSOME TUSOME TUSOME!!!
Asante kwa maelezo mengi sana lakini kwa wenye uelewa mdogo tunataka kujua ni kwa nini ilitugwa kanuni inayowalipisha hawa million 800 na wengine kidogo!? Hoja hapa ni kuwa tunajitungia vikanuni na vijisheria vingi vingi lakini visivyokubalika kwingineko duniani na hata waliovitunga hawavielewi. Kuwekana sawa kuna hukumu ilitolewa (na Mahakama ya Afrika kama sikosei) kuwa sheria iliyopitishwa na Bunge letu wenyewe ilikuwa inakiuka haki za binadamu.
Swali jepesi sheria za Kenya, Uganda, Rwanda nk zinaruhusuje hizo local channels zao kuonekana Azam
/DSTV na hapa zisiruhusu wakati sote ni Jumuiya ya Afrika Mashariki!?
 
Nimemsikia Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano Atashasta Nditiye bungeni leo anasema tayari Azam wamepata leseni ya kuwa MUX wakiungana na akina Startimes Ting na Digitek...nadhani sasa ule ubabe wa soko wa mchina kutoonyesha chaneli za FTA bila malipo unaenda kukoma...hawa jamaa kwa ubora nadhani vingamuzi vyao vitanunulika sana. Hongereni Azam kwa hatua hiyo muhimu angalau tuone chaneli za ndani kwa ubora maana hivi visimbuzi vingine ubora hamna kabisa wengine mara wazime mara wawake...kama hao wengine wanaojinasibu wakubwa ubora picha zina ukunguukungu...

WITO WANGU KWENU AZAM...Mtuletee ving'amuzi vya maana na vya HD viwe na options lukuki ikiwezekana hata kuweka flash na kufanya gaming humo humo dunia ishaendelea fanyeni utafiti vizuri mje na kitu konki...wakenya waje wajifunze Tanzania. Heko!View attachment 1097133
kingamuzi cha MENGI CHA DIGITEK hakionyeshi channel yeyote, kwenu wenye navyo mnaona kitu?
 
Ndo maana wabunge walisema tusubirie kwanza wakalazimisha kuzima analogia ili.mchina auze startimes harakaharaka
 
Asante kwa maelezo mengi sana lakini kwa wenye uelewa mdogo tunataka kujua ni kwa nini ilitugwa kanuni inayowalipisha hawa million 800 na wengine kidogo!? Hoja hapa ni kuwa tunajitungia vikanuni na vijisheria vingi vingi lakini visivyokubalika kwingineko duniani na hata waliovitunga hawavielewi. Kuwekana sawa kuna hukumu ilitolewa (na Mahakama ya Afrika kama sikosei) kuwa sheria iliyopitishwa na Bunge letu wenyewe ilikuwa inakiuka haki za binadamu.
Swali jepesi sheria za Kenya, Uganda, Rwanda nk zinaruhusuje hizo local channels zao kuonekana Azam
/DSTV na hapa zisiruhusu wakati sote ni Jumuiya ya Afrika Mashariki!?
Sheria za Tanzania si lazima zihusiane na za EAC hata za bara na visiwani si zote zinahusiana kuna masuala ya muungano na yasiyo...

Kuhusu kesi unayoizungumzia haihusiani kabisa na ving'amuzi inahusu online regulations na kuna uzi humu JF umeandika hilo suala.
https://www.jamiiforums.com/threads...i-kutumika-hadi-mahakama-itoe-uamuzi.1438510/
Suala la ving'amuzi ni jingine ufafanuzi nilioutoa hapo unajitosheleza ili kufahamu zaidi unaweza kusoma kanuni zimo kwenye website ya TCRA www.tcra.go.tz
OVA
 
Nakubaliana na wewe, sheria tunazo lakini mara nyingi hazitekelezeki dalili kwamba zina utata.
Na rais wetu mpendwa ni shahidi pale anaposema wazi kuwa kuna milolongo mirefu mpaka inakimbiza wawekezaji. Hebu nielimishe labda inakuwaje TBC inaonekana Azam wakati nayo ni local channel!? Unajua sisi wengine hatuelewi na hatuna uwezo wa kufunga ving'amuzi saba kama vile tuna maonyesho!
 
Asante kwa maelezo mengi sana lakini kwa wenye uelewa mdogo tunataka kujua ni kwa nini ilitugwa kanuni inayowalipisha hawa million 800 na wengine kidogo!? Hoja hapa ni kuwa tunajitungia vikanuni na vijisheria vingi vingi lakini visivyokubalika kwingineko duniani na hata waliovitunga hawavielewi. Kuwekana sawa kuna hukumu ilitolewa (na Mahakama ya Afrika kama sikosei) kuwa sheria iliyopitishwa na Bunge letu wenyewe ilikuwa inakiuka haki za binadamu.
Swali jepesi sheria za Kenya, Uganda, Rwanda nk zinaruhusuje hizo local channels zao kuonekana Azam
/DSTV na hapa zisiruhusu wakati sote ni Jumuiya ya Afrika Mashariki!?
Kweli mkuu chanel zote za Kenya ikiwemo KBc kwenye dstv zinapatikana
 
DSTV waliniambia kama mwezi mmoja uliopita kwamba TCRA wangeweza kuwaruhusu kurudisha STARTV muda wowote ILA naona muda unakwenda bila lolote kufanyika.
Nakuhakikishia hilo halitakaa litokee unless huyo star TV ajibadilishe kuwa subscription channel kama wasafi TV ndio ataweza kuingia dstv vinginevyo haiwezekani...channel zinazotakiwa kuingia dstv Zuku na azam ni zile za kulipia tu isipokuwa tbc1 na tbc3 ambazo ni must carry channel kama sheria inavyosema...walikudanganya haitatokea hata tcra walilitolea ufafanuzi kwamba kama unataka kuona local FTA channels nunua moja kati ya visimbuzi vya MUX na sio hivyo vya wenye hela....na FTA zinafaa kuonekana bure bila malipo kama ilivyokuwa enzi za analojia wakati tukitega antenna kuelekea bomani/halmashauri kupata signal.......enzi za oyaah!! Toka nje kazungushe bomba....poa!!...enhe hapo hapo hapo... hapohapo usigusee!!...poa weka jiwe kaza kamba fresh....
 
Unataka niambia kuanzia sasa azam atasimika minara ya terrestrial?
That's it na tayari ameshaanza ku roll out within 7 good months kwa mujibu wa deputy minister wa mawasiliano kazi itakuwa imekamilika na maeneo mengi nchini watakuwa wanaona FTA fresh
 
Hivi hamna njia ya kudisable TBC isipatikane kwenye king'amuzi..maana inafanya king'amuzi changu kinakuwa kizito:D:D:D:D:D
Impossible waachie wanafamilia wengine waitazame kuna mambo mazuri tu mle wanafamilia yako watakuwa wanapenda kuyaona labda kama wewe ni mseja.
 
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye amelieleza Bunge leo Jumanne Mei 14, 2019 kuwa kituo cha televisheni cha Azam jana Jumatatu kimepokea leseni ya kuonyesha chaneli za ndani bure.

Pia, Nditiye amesema katika kipindi cha miezi saba watajenga mfumo wa kurusha chaneli hizo, hivyo wananchi wanapaswa kuvuta subira.

Naibu waziri ametoa kauli hiyo akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, aliyehoji ni kwa nini Azam wananyimwa haki ya kuonyesha channel za ndani bure.

"Je, Serikali haioni kuwanyima haki hiyo wakati wengine wamepewa ni kukiuka ibara ya 18 ya katiba ambayo inatoa haki ya kupata habari, lakini hata Rais wetu anatumia Azam kurusha matangazo yake hivyo tungejitangaza hadi nje," ameuliza Shangazi.

Katika swali la msingi, Mbunge wa Nyamagana (CCM), Stanslaus Mabula, aliuliza Serikali iwapo haioni kupitia TCRA kuwafungia local channels (chanel za ndani) baadhi ya ving'amuzi ikiwamo Azam TV, DSTV na vingine imewanyima wananchi fursa ya kupata habari.

Naibu waziri amesema Serikali inatambua umuhimu wa wananchi kujua mambo yanayoendelea, hivyo imetoa leseni zenye masharti tofauti.

Amesema kwa sasa matangazo ya umma yanarushwa na TBC1 na TBC3 maarufu safari channel.

Kwa mujibu wa Nditiye, kampuni zinazomiliki ving’amuzi vya DSTV, Zuku na Azam hayakustahiki kutoa huduma ya kubeba chaneli za ndani zisizolipiwa kutokana na masharti ya leseni zao.

Amesema Serikali imefanya jitihada ya kukaribisha maombi ya leseni ya kubeba maudhui ya chaneli za ndani kutoka kwa wanaohitaji kutoa huduma ikiwamo kampuni hizo ili ziweze kupata leseni stahiki.

Mwananchi

===================
MY TAKE

Ni wakati sasa ule ubabe wa soko wa mchina kutoonyesha chaneli za FTA bila malipo uende ukikoma...hawa jamaa kwa ubora nadhani vingamuzi vyao vitanunulika sana.

Hongereni Azam kwa hatua hiyo muhimu angalau tuone chaneli za ndani kwa ubora maana hivi visimbuzi vingine ubora hamna kabisa wengine mara wazime mara wawake...kama hao wengine wanaojinasibu wakubwa ubora picha zina ukunguukungu...

WITO WANGU KWENU AZAM...Mtuletee ving'amuzi vya maana na vya HD viwe na options lukuki ikiwezekana hata kuweka flash na kufanya gaming humo humo dunia ishaendelea fanyeni utafiti vizuri mje na kitu konki...wakenya waje wajifunze Tanzania. Heko!
Hivi haya maswali na majibu huwa wanayaandaa wa kuuliza na wa kujibu?
 
sio sheria zote zina tija.Mambo mengine yanatokana na urasimu tu.mim sidhani kama kipindi kile wanachukua maamuzi yakuvifungia hivyo vingamuzi kulikua hakuna option nyingine au mazungumzo ambayo hayatamwathiri mwananchi wa kawaida.kwasababu katika hayo maamuzi yaliyokua yamefanyika mwathirika amebaki kua mwananchi wa kawaida sio Azam wala Dstv.

Back
Top Bottom