Azam ni kama wameshindwa kazi ya kurusha matangazo ya mpira

Twin Tower

JF-Expert Member
Jan 13, 2023
2,133
2,987
Naangalia hapa mchezo wa Dodoma jiji FC vs Mashujaa huu muonekano wa picha zao ni tatizo sana.

Hata game nyingi za mikoani wameshindwa kabisa kuwa na coverage nzuri.

Wao kama wadhamini sio lazima warushe kila mechi, ama wajadiliane na vilabu vitafwe viwanja kadhaa vya kutumika katika ligi nao wawe na camera za kutosha.

Kwa sasa wanafanya bora liende. Inaudhi sana.
 
IMG_1068.jpg
 
inawezekana hujui masuala ya utangazaji wa mpira kwa tv,standard ya kutangaza mpira kwa televisheni ni kamera 7 kila mechi na azam wanatumia kamera 7 kila mechi sasa sijakuelewa tatizo lako ni lipi
 
Nikiwa kama mtaaalam wa picha shida ni viwanja vibovu taaaa hakuna za maana inalazimika kufunga kamera angle mbili pili taa hafifu hazijazunguka uwanja km ulaya hivyo ni ngumu kuuwa vizur NB sifanyi azam ni maoni yangu km video, photographer
 
inawezekana hujui masuala ya utangazaji wa mpira kwa tv,standard ya kutangaza mpira kwa televisheni ni kamera 7 kila mechi na azam wanatumia kamera 7 kila mechi sasa sijakuelewa tatizo lako ni lipi
Wala sio saba zile ni tatu changamoto ni viwanja sambamba na taa hafifu halafu game za mikoani kama sio simba au yang wanatumia sd formàt nadhan
 
Back
Top Bottom