Sina hamu na kisimbuz cha Azam tena, samahani hivi ni visimbuzi gani alivyo twambia Mwakyembe kuwa ni bure nikanunue hivyoNimewachoka hawa Azam na silipii hicho kingamuzi chao tena!!!
Wangeongezea channels za movie na documentaries kufidia zile local channels walizofungiwa lakini wao wanatujazia machannel za kiganda.
Local channels zimekuwa free, halafu wamepandisha bei. Mimi nilifikiri labda watapunguza bei.Na startimes wamependisha bei kisa bongo star search
Umeona mbali sana ! mimi ninalipa kifurushi cha elfu 28 lakini nimeanza kutafakari upyaNimekuwa nikijiuliza hichi kitengo hakina washauri au ni jeuri tu waliyonayo ndio inawafanya wasibadilike?, Azam media baada ya kupoteza chanel za ndani na pia baada ya kutoonyesha taarifa za Habari, mlitakiwa mjitafakari kuwa hadi sasa nshawapoteza wateja wangapi
Mlitakiwa mpunguze bei ya vifurushi vyenu kutoka 23k angalau bei ipungue hadi 15k ili kufidia chanel zilizopotea, ili kulinda biashara yenu mnatakiwa mpunguze bei ya hivyo vifurushi vyenu la sivyo mtajikuta mnaanza kupunguza wafanyakazi kwa ukata
Mtajikuta mnabakiwa na watazamaji wa ligi kuu na tamthilia ya Hurem maana ndio vitu vilivyobakia vyenye watazamaji, Ni swala la muda tu kama msipochukua hatua mapema mapato yenu yatapungua na mtajikuta mkipunguza wafanyakazi Badilikeni, la sivyo mda utaongea
Star times, utaingiliwa pia cause nawao wanastopisha kuonesha local channelsNalivunja dish Lao hawana maana nahamia star times.Kwanza wameshindwa rudisha local channels