Ayoub Lakred ni kipa mzuri lakini ana tatizo moja kubwa sana ambalo sio zuri kwa kipa

1979Magufuli

JF-Expert Member
Feb 20, 2023
438
1,752
Ni kipa mzuri kwa sababu rekodi zake kule F A Rabat zinajulikana, naona amesifiwa sana tangu alipopangua penati vs Wydad, hata hivyo Ayoub licha ya uzuri wake golini lakini ana tatizo kubwa ambalo asiporekebishwa atakuja kuigharimu timu.

Mwangalieni Ayoub vizuri, ana tatizo katika upigaji wa mipira mbele, anaweza kupiga mbelee juu ukaenda nje au akadhamiria kupiga ndefu juu lakini mpira ukakataa ukaenda ndefu chini na ukamkuta adui, hilo ni tatizo kubwa alilokuwa nalo, lingine hajui kuanzisha mpira pale anaporudishiwa na beki, ukimrudishia mpira Ayoub ana kitete cha kumwanzishia beki wake, wakati mwingine hadi adui amsogelee ndio anapiga mpira, akikutana na adui mjanja anampokonya mpira kizembe na anafunga.

Makosa hayo huwezi kumkuta Diarra wa Yanga, ana control na anajua kupiga mipira mirefu, Manula naye anaweza kupiga ndefu ila hana control kama Diarra, otherwise muda wa kusema Ayoub ni kipa wa ukweli tuendelee kusubiri, ndumba nyingi hapa bongo.
 
Umeamua tu kutafuta vujikasoro. Ayub ni kipa mzuri.
 
Mkuu weka na list ya makipa wengine ambao hawana footwork nzuri kama lakred au umeamua tu kumsifia diara kwa kuangalia tu udhaifu wa lakred
Mbona hujasema kuwa diara asipojitahidi kusave penalt kama alivyofanya lakred atakuja kuigharimu timu..!
 
Jamaa hua unajifanya mjuaji mno Ayubu kwenye mechi ya Wydad hakufanya makosa hayo ulio elezea.. Foot work yake iko vizuri kilichokua kina mgharimu labda ni maneno ya mashabiki lakin kama ataendelea kuwapuuza naona atafanya maajabu.
 
Mkuu weka na list ya makipa wengine ambao hawana footwork nzuri kama lakred au umeamua tu kumsifia diara kwa kuangalia tu udhaifu wa lakred
Mbona hujasema kuwa diara asipojitahidi kusave penalt kama alivyofanya lakred atakuja kuigharimu timu..!
Kwani Diarra hasave penalty?
 
Back
Top Bottom